Matukio ya watu kupigwa nondo jijini Mbeya

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,245
Habarini ndugu zangu.

Wapendwa, habari za jioni,

Kuna tukio limetokea kama dk 30 zimepita, tulivamiwa hapa karibu na nyumbani kuna duka la muaarabu na ana huduma ya tigo pesa, wamekuja majambazi wamepiga risasi juu na kuwajeruhi wauzaji wawili, moja amepigwa begani, na mwingine kwenye mbavu, na kisha kichukua kiasi cha hela ambacho mpaka sasa hakijajulikana.

Nami ningekuwa mmoja wa wale walijeruhiwa, sababu wakati wanavamia hao majambazi, nami niko karibu na hilo duka naelekea hapo dukani kupata huduma, nawaona kabisa wamekuja na pikipiki 2, aina ya Boxer na kutawanyika, kumbe walikuwa wanaandaa mazingira.

Hatua 10 ningezipiga, ningekuwa chini ya ulinzi wao, maana baada ya hapo, walianza kurusha risasi hewani, na kuanza kutawanyisha watu.Nilipokimbilia, anajua mungu na watu tuliokuwa nao kwenye hilo tukio.

Sikuweza kufanya lolote zaidi ya kusali na kusubiri wachukue pesa zao na kuanza kupeana pole.jiji la Mbeya ni jiji linalopatikana Nyanda za Juu Kusini katika zile kanda za nchi.

Jiji hili limekuwa likikua kwa kasi kila mwaka hasa katika sekta ya biashara na hiyo ni kutokana na kuwa mpakani na nchi kama Zambia na Malawi na vilevile ni jiji ambalo lipo katika barabara kuu iendayo nchi za Maghari kama vile DRC na Zimbabwe.

Sasa jiji hili limekuwa na matukio ya watu kupigwa nondo na watuhumiwa kuondoka na damu ambayo ito katika hiyo nondo na mtu huyo kapoteza maisha au mahututi.

Wiki hii kuna watu wawili ambapo mmoja ameuawa an mwingine amenusurika na wote ni madereva wa bodaboda katika kata ya Iwambi karibu na kiwanda cha bia TBL.

Tafadhali anayejua sababu ya watu kupiga nondo binadamu wenzao atujuze na sisi tusiofahamu na nawaomba wananchi wenzangu kuwa makini hasa usiku na kutoa taarifa endapo mtatambua kuwepo kwa vitendo hivyo vya hatari.

Ahsanteni
 
Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,402
1,601
Inasemekana, hizo nondo ambazo huwa wanaondoka nazo zikiwa na damu huwa wanaenda kutundikia nyama ya ng'ombe kwenye mabucha hivyo wateja wanakuja wengi. Inasemekana lakini
 
BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,245
Inasemekana, hizo nondo ambazo huwa wanaondoka nazo zikiwa na damu huwa wanaenda kutundikia nyama ya ng'ombe kwenye mabucha hivyo wateja wanakuja wengi. Inasemekana lakini

Daaaa ina maana tunakula damu za wenzetu?
 
SOGHOO

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
1,268
564
Zile nondo uakuta zimejikunja kwani ni zile za kutundikia nyama ile ktmt au hata ya ng'ombe mabuchani.

Ile tenda ya kuleta chuma chenye damu ya mtu inalipa sana, ila na wewe usije ukawadanganya ukaweka damu ya paka au mbwa wanajinsi ya kujua damu ya binadamu.
 
christmas

JF-Expert Member
Jul 21, 2011
2,687
1,231
huo ukatili niliwahi kuuskia kipindi cha nyumba na sasa umeibuka tena Mungu awalinde watu wa Mbeya
 
BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,245
Zile nondo uakuta zimejikunja kwani ni zile za kutundikia nyama ile ktmt au hata ya ng'ombe mabuchani.

Ile tenda ya kuleta chuma chenye damu ya mtu inalipa sana, ila na wewe usije ukawadanganya ukaweka damu ya paka au mbwa wanajinsi ya kujua damu ya binadamu.

Mmhh inalipa?!!Umejuaje angalia usije kuisaidia polisi.
 
LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,128
8,472
mbeya tena bado lakuchuna ngozi halija rudi likirudi na hilo basi hapo zama za mbeya zitakuwa zimekamilika.

fanya mpango ununue element mkuu .
 
NDAGLA

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
2,490
1,343
Sasa kama issue ni damu ya binadamu tu,kuna ulazima gani wa kumuua mtu?

Si unamtandika ngumi ya pua halafu unatega nondo yako ama unamchana na kiwembe tu.

Au inahitajika nondo iliyoua?
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,608
5,565
huo ukatili niliwahi kuuskia kipindi cha nyumba na sasa umeibuka tena Mungu awalinde watu wa Mbeya

watu walichunwa ngozi enzi hizo hukohuko mkoani Mbeya.

vikongwe na walemavu wa ngozi wanauawa kanda ya ziwa.

ekh!! Sipati picha kwanini haya mauaji hayamaliziki na bado tunaimba KUNA AMANI NA UTULIVU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
kumbambiyu

Member
Jul 29, 2015
32
4
fkra potofu na mawazo fnyu ya hawa wenzetu wa huko mbeya,, mbona mikoa mingne haya mambo hayapo,,!?? bas mm napata kuelewa kwa watu wanaotokea mbeya utawajua tu,, yan wapo abnormal sana,,,,,!!!
hv mbeya kunashda gan jaman!!!!???????
 
Kamanda wa Kweli

JF-Expert Member
Jul 13, 2014
1,422
769
fkra potofu na mawazo fnyu ya hawa wenzetu wa huko mbeya,, mbona mikoa mingne haya mambo hayapo,,!?? bas mm napata kuelewa kwa watu wanaotokea mbeya utawajua tu,, yan wapo abnormal sana,,,,,!!!
hv mbeya kunashda gan jaman!!!!???????

Nielezee kidogo mkuu utawajuaje na huo uabnormal uko vipi Wa hao watu Wa mbeya! Nielezee Tafadhali.
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
17,555
11,826
watu walichunwa ngozi enzi hizo hukohuko mkoani Mbeya.

vikongwe na walemavu wa ngozi wanauawa kanda ya ziwa.

ekh!! Sipati picha kwanini haya mauaji hayamaliziki na bado tunaimba KUNA AMANI NA UTULIVU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Mkuu Amani yetu ni ya Kisiasa tu.
 
JAKUGOTE

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
591
681
Sasa kama issue ni damu ya binadamu tu,kuna ulazima gani wa kumuua mtu?

Si unamtandika ngumi ya pua halafu unatega nondo yako ama unamchana na kiwembe tu.

Au inahitajika nondo iliyoua?dah! we jamaa in noma!!!!
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
17,555
11,826
fkra potofu na mawazo fnyu ya hawa wenzetu wa huko mbeya,, mbona mikoa mingne haya mambo hayapo,,!?? bas mm napata kuelewa kwa watu wanaotokea mbeya utawajua tu,, yan wapo abnormal sana,,,,,!!!
hv mbeya kunashda gan jaman!!!!???????

Mkuu watake radhi watu wa Mbeya haraka sana!!,mimi mwenyewe nimesomea Mbeya watu wa kule ni Wema kabisa,sema tu kuna Wahuni wachache ndio wanachafua jina la jiji la Mbeya,Ona Wahubiri wengi wanatokea Mbeya,Waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatokea Mbeya na Hata Hata kiuwingi wa Makanisa Mbeya inaongoza kwa Tanzania kuwa na Makanisa mengi.Kwa hiyo badilisha mtazamo wako juu ya watu wa Mbeya.
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
17,555
11,826
Nielezee kidogo mkuu utawajuaje na huo uabnormal uko vipi Wa hao watu Wa mbeya! Nielezee Tafadhali.

Sio kweli mkuu!,jamaa ameamua kuwapaka matope watu wa Mbeya,Hivi hao wahuni wachache ndo waharibu sifa ya Wana Mbeya wote??? ,Jamani Ssmaki mmoja akioza,unamtupa ili ubakiwe na wazuri.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom