Matukio ya Wanawake kuuawa na wenza wao pamoja na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi yanazidi kuongezeka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,589
2,000
Ripoti ya Haki za Binadamu inaonyesha kuwa matukio ya mauaji ya wanawake kuuliwa na wenzi wao kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa wivu wa mapenzi yaliongezeka zaidi mwaka 2020 ikililinganishwa na mwaka 2019.

Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa mwaka 2020 pekee walikusanya taarifa za matukio 32 ya vifo vya wanawake waliouwawa na wenza wao kwa sababu ya wivu wa mapenzi wakati mwaka 2019 matukio ya aina hiyo yalikuwa 12.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa vifo 23 vilithibitika kusababishwa na wivu wa mapenzi ambapo wanawake hao waliuwawa na wenza wao au wanaume waliowahi kuwa nao kwenye uhusiano kabla ya kuanzisha uhusiano mwingine.

Matokeo haya ni mwendeleo wa taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu mauaji baina ya wenza yanayosababishwa na wivu wa mapenzi.

Akiwasilisha ripoti hiyo mtafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi ameeleza kuwa takwimu walizopata mwaka 2020 ni zaidi ya mara mbili ya walizokusanya 2019 hali inayoashiria kuongezeka kwa matukio hayo.

Pamoja na mauaji zipo pia taarifa za wanaojeruhiwa hata kupata ulemavu kutokana na ugomvi ambao chanzo chake ni mapenzi.

Kando na hilo ripoti ilionyesha kuwa vitendo vya kujichukulia sheria mkononi bado vinaendelea ambapo mwaka 2020 watu 443 waliuwawa na watu wenye hasira pamoja na imani za kishirikina.

Ripoti inaonyesha kuwa kati ya hao, watu 112 waliuwawa kutokana na sababu za kishirikina ikiwa ni upungufu wa matukio 77 ikilinganishwa na idadi ya waliouwawa kwa sababu hizo mwaka 2019.

Akizungumzia hilo Wazambi aliwataka wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa ni hatari na unaweza kuathiri hata wasiohusika.

“Kuna haja ya kueneza uelewa zaidi kuhusu athari za kujichukulia sheria mkononi na kuhakisha tabia hii inakomeshwa.

Kuna haja pia ya kushughulikia changamoto ya rushwa katika mfumo wa haki jinai, ili kuimarisha imani ya wananchi kwenye mfumo huo,” amesema .

Chanzo: Mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom