Matukio ya Utekaji, Uuaji na Upoteaji wa Watu yanayoendela Nchini: Tanzania inalia, nani wa kuifuta machozi?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Juzi yake ilikuwa ni Salimu Mohammed Almas aliyepigwa risasi mchana kweupe akiwa njiani kwenye shughuli zake, Mbagala Dar es Salaam Tanzania

Jana yake akawa ni Ally Juma Suleiman aliyechukuliwa kwake Mtoni, Ugunja akapigwa na kujeruhiwa vibaya na hatimaye mauti yakamchukua siku mbili baadae

Leo ni Msichana Akwilina Akwilin Shirima, mwanafunzi wa chuo Kikuu akiwa kwenye safari kuelekea masomoni ndani ya daladala jijini Dar es Salaam

Na mote hakuna aliyewajibika wala kuwajibishwa kwa mauaji hayo. Na sasa swali ambalo mbiu ya mnyonge anauliza leo hii ni kama lile alilouliza kiongozi wa nafudhi nchini Tanzania, Abdul Nondo “NANI YUPO SALAMA TANZANIA HII?”

Kama kuna kitu ambacho wadau mbalimbali wanakubaliana ni kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hapana shaka yoyote inapitia katika kipindi kigumu mno katika historia yake ya nusu karne. Makundi ya kidini, kisiasa, asasi za kiraia na wanafunzi wanalia kilio kimoja cha haki zinazozidi kuminywa, cha uhuru unaozidi kukanyagwa!

Tukio la karibu kabisa lililo hanikiza vilio hivyo ni mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji cha Taifa, Msichana Akwilina Akwilin Shirima ambaye alijikuta muhanga wa mzozo ambao hakuulalia wala kuuamkia. Siku ya tarehe 16 Februari, siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mwanafunzi huyo alikuwa kwenye daladala kwa safari zake zinazoelezwa na familia na marafiki zake kwamba zilihusisha harakati za masomo

Njiani gari alilopanda likakutana na maandamano ya viongozi na wafuasi wa chama cha upinzani CHADEMA, wakielekea kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kikosi cha Jeshi la Polisi kikiwazuia wasifike huko.

Hapo ndipo risasi za moto ziliporushwa na moja wapo ikakifikia kichwa cha Akwilina na kuutawanya kabisa ubongo wake. Uhai wake ukawa umezimwa hapo, ndoto zake na wazazi wake zikawa zimekatishwa njiani kuelekea Bagamoyo, njiani kuelekea kwenye matumani.

Baba mzazi wa msichana hiyo, Akwilin Shirima anasema “Sina pa kwenda sina mbele wala nyuma, sasa nangoja kifo tu kama Akwilina wangu. Akwilina angeugua ningejua ni mgonjwa”

Lakini machozi ya wazazi wa Akwilina si pekee kumwagika ndani ya kipindi hiki kisichozidi mwaka mmoja ndani ya ardhi ya Tanzania Mwishoni mwa mwezi septemba mwaka jana, Bwana Ally Juma Suleiman aliyekuwa na umri wa miaka 50 alivamiwa nyumbani kwake Mtoni kisiwani Unguja na watu ambao yeye na familia yake walisema baadae kuwa ni vyombo vya usalama. Akiwa amepigwa na kufungwa pingu alipopatikana alfajiri yake alikuwa ameshajeruhiwa vibaya kiasi ya kwamba siku ya pili yake akapoteza maisha akiwa hospitalini Mnazi mmoja.

Mkewe Bi. Rehema Nasor anakumbuka mkasa wenye ulivyokuwa “Ilikuwa siku ya jumanne usiku, nikasikia kishindo kikubwa nje. Mara tukapigiwa hodi, kuchungulia nikakuta Askari wengi sana nje wana bunduki na wengine wana marungu na mapanga, kila aina ya silaha mkononi. Mume wangu alikuwa hajaamka alivyoshtuka akaniuliza; nini? Nikamwabia Askari. Akanyanyuka akanambia mke wangu buriani mie nishakufa”

Na nyuma ya tukio hili la Ally Juma Suleiman kulikuwa na mkasa wa mwanafunzi wa chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa jina Salmu Mohammed Almas, ambaye alipigwa risasi akiwa mtaani na kupoteza maisha papo hapo.

Lakini kinyume kidogo na wengine kwa huyu, Polisi walitaa kuthibitisha kuwa walimuua kweli lakini kwa kuwa alikuwa ni mtuhumiwa gaidi.

Kamanda Sirro anasema “Maana yake kama ni mtu alikuwa ni mwema, wakati Askari anamwambia simama nyanyua mikono juu ye anasema “Allahu Akbar” huku anamfuata. Mlitaka Polisi afanyaje akimbie?”

Madai hayo yalikanushwa vikali na familia ambayo ilikaa na maiti ya mtoto wao kwa Zaidi ya mwezi mzima walikataa kumzika hadi hapo jina lake litakapo safishwa.

Almas Mohammed Almas kaka wa marehemu anasema “Kimsingi mtu anapogundua kuwa amefanya makosa, kiungwana tu kwanza kama ni taratibu za kisheria au kinidhamu ni vema zichukuliwe kwa sababu kwa kufanya hivyo unaweza kuzuia pia wka wengine kufuata njia hiyo ambayo wao wamefanya”

Hata hivyo la marehemu Akwilina kwaa kuwa lake ni la karibuni Zaidi na kutokana na mazingira lilivyotokea limevuta hisia kali kutoka makundi mbalimbali ya haki za binadamu na kwa hiyo serikali pia imelichukulia hatua. Sio tu kwamba Rais Magufuli alituma salamu zake za rambirambi bali pia Mawaziri wake walitoa kauli mbalimbali, pamoja na kuitembelea familia ya Akwilina kitu ambacho hakijawahi kufanyika kwa wahanga wengine wa mauaji yanayoshukiwa kutendwa na vyombo vya dola.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alisema “Nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha la binti yetu, mdogo wangu ambaye hakuwa na hatia. Matukio kama haya naona yameanza kurujea tena kwa kasi”

Kauli hiyo ya Waziri Nchemba mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao imerudisha swali la MBIU YA MNYONGE kwamba “TANZANIA BADO INGALI SALAMA KIASI GANI KWA RAIA HAO NA MALI ZAO?”

Onesmo Ole Nguruma anayetokea Mwamvuli wa Asasi za Kiraia Nchini, ukiwa mtandao wa Walinzi wa haki za binadamu anasema “Kule Kibiti raia Zaidi ta 40 wamekufa, viongozi, Polisi Zaidi ya 10 wamepoteza maisha. Viongozi wa Siasa katika chaguzi zilizopita wamepoteza maisha. Zanzibar kule watu wanapoa wanakufa mfano matukio ya kupotea mwandishi Azury ambaye mpaka sasa tunakaribia siku 100 hajulikani alipo. Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, hivi karibuni kuuawa kwa Katibu wa CHADEMA. Yote haya si kiashiria kizuri kwa taifa ambalo limeonekana na kukubalika kama taifa lenye Amani kwa muda mrefu”

Lakini kauli hizi kavu kavu kutoka kwa Asasi za Kiraia na Wanaharakati wengine wa haki za binadamu, zinamaana gani kwenye ualisia? Je, zinaweza kuzuia au angalau kupunguza tu mwenendo wa uvunjwaji wa haki za binadamu unaosemwa unazidi kuimarika na katika kasi inayotajwa kuwa kubwa mno kwa taifa ambalo lilizoe kuwa kisiwa cha Amani katika kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati.

Adul Nondo kutoka Jumuiya ya Mwanafunzi nchini Tanzania anasema “Haki ya usalama wa raia hailindwi, watu wanatekwa, watu wanakufa. Huyo ambaye ni mwanafunzi anapigwa risasi bila hatia, Waziri yupo hajasema chochote zaidi ya kusema eti uchunguzi ufanyike na kwa haya yanayoendelea kutokea tunaomba Waziri Mwigulu ajiuzuru nafasi yake ya kisiasa kwa sababu ameshindwa kusimamia usalama na haki za raia wa Tanzania”

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema yanapotokea mambo kama haya, Serikali huamua kuchukua njia moja kati ya tatu; Ama kuyanyamazia kabisa kama ilivyofanya awali kwa Ally Juma Suleiman, au nipozungumzia ni kuyakanusha na kuyandosha njiani tu kama ilivyofanya kwenye lile swala maarufu la makundi yaitwayo Mazombi huko visiwani Zanzibar, Ama kuwageuza wahanga kuwa wakosaji kama wanavyodai wanaharakati kwenye swala la Salim Mohammed Almas

Hili sio tu kwamba linaondoa heshima kwa Serikali kwa jicho la kimataifa bali pia linapunguza Imani ya wananchi wake na hivyo kujenga msingi wa utawala wa kiholela.

Ndicho lilichoakisika hapa kwenye kauli ya mke wa Ally Juma Suleiman; “Mie naona Serikali haina haki kwa sababu watu waliokuja si raia wala ni watu wao wa Serikali kwa sababu hakuna raia mwenye bunduki, hivyo tunakosa Imani na Serikali maana ni dhulma kubwa imepita, wamemdhulumu vya kutosha”

DHULUMA KWA MTU MMOJA NI DHULUMA KWA WATU WOTE

Chanzo: Mbiu ya Mnyonge – DW Swahili
 
''Sina pa kwenda sina mbele wala nyuma, sasa nangoja kifo tu kama Akwilina wangu. Akwilina angeugua ningejua ni mgonjwa”-Baba mzazi Akwilina
 
''Sina pa kwenda sina mbele wala nyuma, sasa nangoja kifo tu kama Akwilina wangu. Akwilina angeugua ningejua ni mgonjwa”-Baba mzazi Akwilina
Kuna vitu vinatokea kwenyw maisha u ataman iwe ndoto tu,,

Kuna mambo tunafanyiana wanadamu zaid ya wanyama ,, inaumiza sana
 
Back
Top Bottom