kiboksi manyoya
JF-Expert Member
- Nov 16, 2016
- 377
- 311
Ukiingia bank utakuta kuna matangazo yanayozuia matumizi ya simu za mikononi ukiwa ndani,lakini wahudumu hasa ma-teller Mara nyingi hutumia simu kama vile utaratibu huo wao hauwahusu,limetokea tukio la askari kuvamiwa na kunyang'anywa kiasi kikubwa cha pesa Mara baada ya kutoka benki(jina kapuni) kuchukua pesa (mkopo),wale jamaa walimvamia alipoingia ndani ya GARI nao ghafla wakaingia huku wakimuonesha cha moto,wakatoka nae hadi nje mji kisha wakapanda pkpk wakasepa na pesa,lakini jamaa alikuwa na wasiwasi na teller aliyemhudumia kwani muda mwingi alikuwa anachat,baada ya kutelekezwa pale akarudi pale bank moja kwa moja kwa meneja na kumueleza situation ilivyotokea,kisha meneja kwa kuogopa kuharibiwa sifa,akaenda kwa yule teller akachukua cm yake,ktk kuichunguza zikakutwa msg walizokuwa wanatumiana na waharifu zikimuelezea wasifu na kiasi cha pesa alicho draw,yule askari akaombwa sana msamaha na yule meneja na kuahidiwa kwa maandishi kuwa pesa baada ya muda itarudishwa,baada ya SAA kama tatu salio likasoma,tuwe makini unapohudumiwa huku teller anachat mwambie kabisa nikiibiwa tutajuana.