Sekibuju
JF-Expert Member
- Jul 23, 2012
- 314
- 130
Wakuu Habari Zenu!
Nimechunguza katika awamu hii na zilizopita, naona kwa kipindi hiki cha Awamu ya tano matukio ya uporaji fedha katika mabenki au wateja wa benki kuporwa fedha wakitoka kuchukua fedha zao yamepungua au sikuyasikia kwa muda mrefu sana tofauti na awamu zilizopita.
Kupungua kwa matukio haya kwa upande wangu kunaniletea picha mbaya sana kwa vyombo vinavyohusika na usalama wa raia hususan kipindi hiki ambacho mtumishi ni rahisi kupoteza nafasi yake.
Mfano mdogo ni tukio la wafanyabiashara wa dhahabu mkoani Mwanza, jinsi polisi wasio waaminifu kushikiliwa, hii inaonesha hivi sasa watumishi wenyewe wanachomana au ma- reporter muongoni mwao. Kutokana na hali hii, kwa mtazamo wangu huenda ikawa ni sababu ya matukio hayo kupungua katika awamu hii.
Hii imenipa picha kuwa kuna baadhi ya watumishi ambao si waaminifu walikuwa wakihusika kupanga matukio hayo ambayo yamepoteza raia wengi wasio na hatia kutokana na wingi wa matukio hayo kipindi cha nyuma.
Huu ni mtazamo wangu, si lazima uwe sahihi kwako, na kama una mtazamo tofauti huu, nakukaribisha uuweke hapa niweze, huenda ukasaidia kupata kujua sababu nyingine tofauti na hii nnayohisi.
Sent using Jamii Forums mobile app