Matukio ya uchunaji ngozi watoto wilayani Muleba, Kagera yadhibitiwe!

Halfcaste

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
972
215
Kumekuwepo na matukio mbalimbali ya kupotea kwa watoto na kukutwa wamechunwa ngozi wilayani Muleba, hasa maeneo ya Kamachumu na Muhutwe kiasi cha kufanya wakazi wa maeneo haya kuishi kwa hofu kubwa.

Hivyo, tunaomba vyombo vya usalama kuigilia kati na kukomesha haraka vitendo hivi.
 
Wiki iliyopita nilikuwa Maruku,Bukoba vijijini,nilikuta simulizi za uchunaji ngozi wa watoto. Lakini niligundua ni uvumi ambao utakua unasambazwa kwa malengo fulani na wanaofaidika na uvumi huu ni watawala!
 
Hayo matukio ya kuibiwa watoto maeneo hayo yaliyotajwa yapo. huu ni mwaka wa tatu tangu nisikie na ni mwaka wa pili tangu tum-resque mtoto kutoka kwa mwizi ambae alikua anajaribu kusepa nae. Kama ingekua amri yangu tungeweka adhabu ya kunyonga wezi kama hao. Inasikitisha kuona hata wale walioshikwa na ngozi za Zeruzeru wapo wanadunda mitaani.
 
Wiki iliyopita nilikuwa Maruku,Bukoba vijijini,nilikuta simulizi za uchunaji ngozi wa watoto. Lakini niligundua ni uvumi ambao utakua unasambazwa kwa malengo fulani na wanaofaidika na uvumi huu ni watawala!

sio uvumi mimi mwenyewe mtoto wa mama yangu mdogo amechunwa ngozi,alikutwa kwenye msitu wa kambi ya jeshi kaboya akiwa hana ngozi baada ya kupotea kwa siku nane. Hiki kitu ni kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom