DOKEZO Matukio ya kutekwa kwa watoto maeneo ya Kigamboni na maeneo jirani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,056
2,195
Kumekuwa na hali ya sintofahamu inayoendelea Kwa wakazi wa Kigamboni na Maeneo jirani ya kijichi, mbagala kuu na Mikwambe baada ya matukio ya kutekwa kwa watoto wadogo wa shule za msingi na secondary hali inayopelekea wazazi wengi wakazi wa maeneo hayo kuhofia usalama wa watoto wao pindi wanapoenda na kurudi shule.

Aidha duru zinadai watekaji hutumia Bajaj au pikipiki Kwa kukifanya kuwa wanaotaka kumpa lift mwanafunzi husika.

Hali ya ukimya Kwa vyombo vya usalama na serikali ya wilaya maeneo hayo bado haiwafurahishi wananchi wa maeneo husika kwani kila kukicha wanapata taarifa mpya aidha miwili wa mwanafunzi wa shule ya msingi au secondary kupatika kwenye makazi yasiyokuwa na pilika pilika au majumba ambayo ujenzi haujakamilika.

Niwaombe wazazi wa maeneo ya Kibugumo, Kisota, Ungindoni, Kibada, Mawwni, Mikwambe Kisarawe 2, Kijichi na Mbagala kuu kuwasindikiza watoto shuleni na kwenda kuwachikua ili kuepuka kutoweka Kwa mtoto katika mazingira ya utatanishi.

Asanteni.
Mdau mmoja.
 
taarifa ya tahaluki kama hii inatakiwa kupata ithibati. angalau nukuu viongozi wa mtaa watupie neno kama kuna ugumu kuwatafuta wakuu wa vyombo vya usalama, wakuu wa shule, maafisa elimu, ustawi wa jamii n.k.

hatahivyo sipingani na uwezekano wa kuweko matukio kama hayo.
 
taarifa ya tahaluki kama hii inatakiwa kupata ithibati. angalau nukuu viongozi wa mtaa watupie neno kama kuna ugumu kuwatafuta wakuu wa vyombo vya usalama, wakuu wa shule, maafisa elimu, ustawi wa jamii n.k.

hatahivyo sipingani na uwezekano wa kuweko matukio kama hayo.

Wanasema chizi anachekesha kama hatoki kwenye familia yako.

Kama mtoto wako au wa ndugu yako hajatekwa/kupotea au kushuhudia mtoto wa jirani yako amepotea/kutekwa hauwezi kuelewa.

Jana karibu mitandao yote imetuma meseji ya kuchukua tahadhali ya kutekwa na kutolewa figo unafikiri hawajui kama kuna hiyo issue?
 
Back
Top Bottom