Matukio ya kustaajabisha Tanzania

Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,292
3,391
Habari wana jamvi,hebu leo tukumbushane matukio ambayo yalishawahi kutokea ama kutendwa/kutangazwa na serikali yetu ambayo katu hayaingii akilini hata kwa mtoto wa darasa la tano,mi naanza na yafuatayo
1.bangi kuibiwa kituo cha polisi
2.serikali kuamua kutorusha live bunge,
3.bunge maalum la katiba kuamua kupiga kura ya wazi badala ya siri wakati wa kujadili rasimu ya katiba
4.serikali kuanzisha studio ya bunge na chaneli nyingne kuchukua matangazo huko,hvyo studio ikikorofisha watz wote hakuna kuona bunge,

Tuendelee matukio mengineyo
 
Jecha kushindwa ubunge kwenye kura za maoni na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa zec
 
wageni kuchimba makaa ya mawe kyela zaidi ya miaka mitatu bila kuwana kibali chochote toka serikalini.
 
Mfanyakazi anayeitwa Hewa kulipwa mshahara na kupanda madaraja bila kuandamana huku mfanyakazi aliyeko kazini muda wote wa kazi akishindwa kulipwa stahiki zake na kutukanwa juu kudhalilishwa na mavitisho lukuki haya yote hewa hayampati katulia tuliiiiii salary slip inasoma
 
Back
Top Bottom