Matukio ya kupigana nondo yaibuka upya Mbeya.

ugawafisi

Senior Member
Jul 22, 2011
127
12
Kwa kipindi kirefu jijini Mbeya tulipumzika kukumbwa na matukio ya kikatili kama ilivyozoeleka hapo nyuma, bila shaka tunakumbuka uchunaji wa ngozi na matukio mengine, jambo la kusikitisha ukatili huo umeibuka ghafla ambapo jana usiku watu 9 ktk eneo la Uyole wamepigwa nondo na kukatwa masikio.

Kuna jirani yangu ametoka kuangalia mpira nae ameuliwa na kukatwa masikio, inaonekana kuna imani za kishirikina, jeshi la polisi lifanye kazi yake kwani hali ni mbaya hata watoto wanaogopa kwenda shule mida ya asubuhi sana.

Yaani mby sijui kuna laana gani,...anyway ni kwetu lakn,...anyway poleni wahanga na rip wafu

Mbeya inaweza kuwa ni moja ya eneo linaloongoza kwa watu wake hasa vijana kuendesha shughuli zake kishirikina hasa kibiashara, vijana wadogo wamejiingiza kwenye mambo ya kishirikina.

Nakumbuka nilikuja kipindi fulani(2008) pale SAE nikalala hotel moja nzuri sana inaitwa Golden sity' na nikaonyeshwa kijana mdogo sana anaye imiliki na nikapewa tetesi kwamba kaipata kishirikina kwa shart la kufa yeye mwenyewe mmiliki baada ya miaka kadhaa, na nilipoenda juzi kwenye ile Hotel nikaambiwa mmiliki amesha fariki.

Nilishangaa sana huu ni utajiri gani Watu wa mbeya? ni heri uwe na vipesa vyako vya kawaida na uishi kwa amani.

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana

aiseeeeeeee!...ritz na mitazamo yake_haya mkuu.

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana
Nonsense sidhani kama uina akili timamu unaweza ukaleta mzaa kwenye tukio la kuhuzunisha kama hili, watch your tounge kama mmoja kati ya waliokufa angekua ni mtu wako wa karibu sidhani kama ungetamka maneno kama hayo ya kejeli.

Vijana wa Mbeya wanapiga nondo kwasababu mbunge wao Sugu hajawasaidia lolote kama alivyowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010.

Wakati wa uchaguzi huo SUGU aliahidi kuwa atawasaidia sana vijana kwa kuwaanzishia miradi ya maendeleo lakini tangu ameingia mjengoni amekaa kimya na sasa amejinunulia magari mawili. Vijana waache ushabiki Chadema ni wasaniii tu kama ilivyo CCM

uli mbine ugwe, uka nkafu. Njoo Mby uone sugu anavyo supply makompyuta kwenye shule za kata ambazo nyie CCm mzitelekeza

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana

AGHRRRRR ,ACHA UONGO HAWA VIONGOZ WA CHAMA CHENU NDO WATEJA WAKUU WA VUGAGULA! HAPO BAGAMOYO SANGOMA KANUNULIWA VX, MMMH PALE NANILIU HAO SANGOMA WANA FREE PASS, TENA USISEME MADUDU HAYO,MWEMBECHAI SI NDO ALIKUWA KAMANDA MKUU WA WALINZI LOOOL

mbeya wazee waliomba kibali kwa Serikali iwashugulikie wote,kuanzia wabaki,wauaji wa albino,na wapiga Nondo.

Nakumbuka walisema hao wahalifu wangejileta wenyewe polisi kama serikali itawashirikisha kwa hilo.

Mbeya mi nimekaa miaka minne nilishuhudia majeruhi wa Kupigwa Nondo Mwaka 2006 yani hawachukuliwi chochote,wao shida yao ilikuwa Mabaki ya Damu kwenye Nondo

Mbeya kulizuka Mauaji ya Kukatwa Matiti kwa wanawake,mpaka leo sikupata jibu wanayatumia kutengeneza nini?

Mji wa mbeya ndo unaongoza kwa wingi wa makanisa sasa inakuwaje huko? Hawamuogopi Mungu kabisa?
Mungu amwage moto mbeya pa tulie

Mungu atuepushe na shirki na wanaofanya vitendo hivi Mungu awalaani

Jamani poleni sana na RIP wafu,ila hapa kwe2 Arusha nakwambia vijana wanatumiaga nondo sana lakini kwa kupora na kuvunja milango,Ila juzi kuna bwana mdogo mmoja aliuwawa na kunyofolewa nyeti yote na kuna mwingine alijitetea ktk wiki moja iliyopita naye alinusurika na kisanga hicho. Hakika hali si shwari Arusha mjini hasa pembezoni mwa mji hasa Olmatejo,Engusero, Mianzini,Sakina juu na Ilkiurei hakika hali si nzuri kabisa. Nawapa pole wenzetu Mkoani Mbeya.

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana

Ijapokuwa Mi nilikuwa Gesti humu kitambo mpaka leo nikajiunga rasmi na nimepokelewa na nina furaha jamvi,lakini kuna baadhi ya ID nikisisoma utafikiri mtu alipost hana uweza wa kufikiri hakika wana akili ndg sana kama huyu Best!

Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana

Mmemwagiana wenyewe hiyo Tindikali, si mnajulikana sana nyie Kilimba yuko wapi? Acheni hizo siasa zenu uchwara.

QUOTE=ritz;2500089]Lazima watakuwa CDM tu ndio wana tabia hizo si mmeona Igunga, walivyomfanya yule kijana mpenda amani, wamemwagia Tindikali bana[/QUOTE]

Mmemwagiana wenyewe hiyo Tindikali, si mnajulikana sana nyie Kolimba yuko wapi? Acheni hizo siasa zenu uchwara. Nendeni mahakani basi ushahidi si mnao?

wakuu mpaka sasa maendeleo si mabaya kwani jeshi la polisi limeshamkamata kijana mmoja kwa tuhuma hizo, na pia tumeamua kuliko kujifungia ndani mapema kwa hofu ni bora tujipange raia tupige doria, watu wana hasira mbaya nadhani akikamatwa mtu haeleweki patachimbika.

Unajua mbeya wakinga wapo wengi sana na wanafanya biashara kwa uchawi, kwa hiyo mganga akiibuka tu na dawa mpya nasi masharti yake ndiyo yasnayoua watu (ni fikra tu..)

jamani wanyakyusa kubadili mitazamo yao ya ndani ni ngumu,wanasilka ya kutu,hawabadiki daima.
Wanyakyusa ni walewale jana,leo na kesho na hata milele.

Back
Top Bottom