Matukio Pacha ya Ujambazi, Muda wa Matukio, Aina ya Walengwa, Vifaa Vilivyoibwa ni Sawasawa

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Attn: Mods nawasihi hii nyuzi iacheni kama ilivyo ingawa inafanana na ile mliyoitolea ufafanuzi.

Kuna matukio ya ujambazi ambayo yametokea usiku wa saa 8 kuamkia leo 22/ Oktoba/ 2012. Katika matukio haya ambayo yametokea katika jiji la DSM yanahusu uharibifu na wizi wa computer na laptop. Mambo ni hivi:

Wakati kituo na ofisi za ATN (Agape TV) kikivamiwa na majambazi usiku wa saa 8 maeneo ya Mbezi Beach-Jogoo nako huko Mbezi Luis, Kwa Mzungu kituo cha Kulelea watoto wa mitaani " Child in the Sun" ambacho kikochini ya Kanisa katoliki kimevamiwa na majambazi usiku wa saa 8 kuamkia leo.

Mali zilizoporwa katika matukio yote mawili ni computer kadhaa na Laptop kadhaa. Katika matukio hayo yote wahusika hawakumdhuru mtu ye yote kimwili.

Uvamizi wa kituo cha "Child in The Sun" limeripotiwa na padri mlezi wa kituo hicho katika kituo cha Polisi cha Mbezi.

My take: Penye wengi hapa haribiki neno, humu jamvini kuna vichwa hebu tuyaangalie matukio haya mawili tofauti lakini yako kama pacha vile.
 
inawezekana sana lengo lao ni kuharibu mali za kanisa kwani madai yao wanapendelewa na serikali
na pia nia ni kudhoofisha ukristo.
lakini hao majambazi soon watajisalimisha wenyewe kwa Yesu hakuna kinachojificha kila kitu kitaanikwa wazi
wasiechezee nguvu ya maombi, wale waliovunja makanisa mbagala mtawasikia karibuni watakuwa machizi,wataumwa magonjwa ya ajabu,watakufa vifo vya ajabu na wengine watajisalimisha wenyewe,ni laana kwao na hata vizazi vyao.
 
Dini za kigaidi kamwe haziwezi kujificha. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyoendelea kuwa hadharani. Tuendelee kuona sinema hii.
 
Ndio Maana Leo Kevin Motto na James Thobias sijawasikia leo katika uchambuzi wa Magazeti,Dr Fernandez Nunua hata miguu ya kuku uwape walinzi wako.....
 
Dini za kigaidi kamwe haziwezi kujificha. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyoendelea kuwa hadharani. Tuendelee kuona sinema hii.
Hayo maneno unayoongea sio ya mtu mwenye hekima na anayejua Dini anayoiamini, Hivi ujambazi kufanyika makanisani na vituo ambavyo vinalelewa na kanisa imekuwa ni waislam waliofanya hivyo? Tuwe na upeo wa kuelewa kidogo kwani hii ni mara ya kwanza kwa makanisa kuibiwa? na wakati huo yalipoibiwa walioiba walikuwa ni waislam? Tumeshuhudia migongano katika makanisa na wizi wa fedha za misaada na michango mbali mbali makanisani wanaoiba ni waislam? Hapa tunachotakiwa ni kulilaumu jeshi la polisi kwa kutochukua hatua pale ujambazi unapotokea kwani kazi yao ni kulinda raia na mali zao.
 
Dini za kigaidi kamwe haziwezi kujificha. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyoendelea kuwa hadharani. Tuendelee kuona sinema hii.

Ubaya wa sinema hii, hata kwa upendaye kuwa mtazamaji tuu, kwa jinsi inavyogusa suala nyeti-imani-madhara yanakuja kuwaathiri waigizaji, waandika mchezo, wachezeshaji hadi watazamaji! Hayachagui mpaka- sote inatugusa!
 
naona usalama wa tanzania na mali zetu unaanza kuchukua sura mpya sana.........
any way tutafika tu.............
 
Proof ya haya matukio kutokea tunaipata wapi? isijekuwa unafabricate story kuendeleza mambo ya udini ambao tumeazimia kuupiga vita kwa kuwapa mateso ya pekee ring leader huko jela waliko na mkakati wa kuwavutisha hewa ya sumu
 
Lolote laweza kuwa, ingawa watz kwa unafiki wao hugoma kuongelea matatizo ya msingi yahusuyo udini ili kupata suluhu ya kweli. Husubiri hadi Mbagala ijitokeze ndipo waanze kulaani serikali wakati watu waliotoa thread za maonyo walishambuliwa vikali. Eti wengine wanadai wamechoka na habari za udini wakiomba mods wafunge thread hizo utadhani jf ndio chanzo cha udini. Wanasahau kuwa mambo haya yanajadiliwa kwenye majumba ya ibada na watu wasio hata na wazo kuna kitu kinaitwa jf. Nadhani unafiki wa kukwepa kujadili matatizo yanapojitokeza unaila jf. Endeleeni kudai wahuni, majambazi... Alamsiki.
 
Saa hizi ni saa kumi alfajiri. Matukio saa nane alfajiri. Wewe umejulia wapi, ni polisi ama jambazi?
Hai ni wwzi wala sio majambazi, majambazi hayaibi laptop. Ugumu wa maisha tu. Usilete uchochezi wa.kidini.
 
Kwa btaarifa nilizopata kutoka kwa mtu anayeishi na kufanya kazi "child under the sun" ni kuwa padri amejeruhiwa kwa mapanga na wamepora pesa pia, si laptop na computer tu kama ulivyoelezea. Sitaki kuamini kuwa zina uhusiano na vurugu za kidini bali uhalifu kama uhalifu mwingine.
 
naona usalama wa tanzania na mali zetu unaanza kuchukua sura mpya sana.........
any way tutafika tu.............

narudia tena: polisi ni majambazi yanayotumia kodi zetu kutuibia! Raia linda mali zako!
 
Moderators,

Tafadhalini these fabricated stories kuweni nazo makini. Enough with these hate, fabricated stories. Inamaana kila wizi sasa unastory behind it? Angalieni msije kuwa mnachochea fitna za udini kwani wahuni na majambazi hawana dini na mwisho wa siku litakalo tokea la kutokea msije kulaumu mtu.
 
Mijitu kwa uchochezi wa kidini haijambo.Kwani majambazi hawaibi laptop.Ukitumia vibaya akili ni janga kwako na Taifa kwa ujumla
 
Nimegundua watu wana anzisha threads ili wwawatukate waislamu na Uislam, but waislam huwa hawajibu hayo matusi ni busara ilioje, maana watu watakua wanaiba kwa kisingizio cha dini na kwa sababu vichwani mwao wamejaa chuki wanaishia kutukana na kuhukumu, maana imeandikwa kwenye vitabu vya dini usihukumu, sasa wewe unayetukana unatofauti gani na aliyekojolea msahafu au aliyechoma Kanisa? Tujitafakali wadau vinginevyo tutakuwa tunaiba pesa mfuko wa kulia tunaweka mfuko wa kushoto!
 
Wameshajua nchi yetu ni dhaifu, umakini ni tuuzidishe kwenye kufunga na kuomba ili mapepo yapite mbali na sisi
 
Back
Top Bottom