Matukio ni mwalimu mwema. Nimejifunza kitu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
"Asiyefunzwa na ***** hufunzwa na Ulimwengu"

Huu msemo mwanzo sikuwaza hata Kama unamaana Sana hapo awali niliukariri Kama wimbo tu

Lakini matukio yamenifunza

Kama Hujawahi kulala njaa, Mwaga chakula lakini siku ukifulia Ndipo utaelewa njaa Ni nini
  • Huwezi kuona umhimu wa konda Kama Hujawahi kula nauli, Siku ukila nauli ndipo utaelewa kumbe konda naye mtu, Utaelewa umhimu wa kupita chochoro ukoje
Maisha ya kushukuru

Nimejifunza kumbe kushukuru kwa kutendewa mema na wengine, kunalipa zaidi kuliko kujifanya jeuri na mjuaji, nimejifunza pia kumbe kushukuru Ni sawa na kuomba tena, nimejifunza kumbe anayekupa siyo kwamba hakitaki Bali kaona ikufae wewe zaidi kuliko wengine, pia nimejifunza kumbe anayetoa hufurahishwa zaidi akiona umetumia alichokupa ipasavyo! Nimejifunza kushukuru kunalipa zaidi

Maisha ya kusamehe
Maisha ya uswahilini yanaboa, maisha ya kupanga nyumba yanaboa sana, lakini kumbe hutakiwi kuboreka moja kwa moja Aisee Kuna Neema iliyofichwa nyuma ya dhiki,

Nimejifunza wenye dhiki hukaa sehemu moja,. huchukiana wao kwa wao lakini ukifanikiwa kutoka kimaisha maadui wanakuja wengine kabisa kwa level yako!
Nitatoa mfano juu ya hili!
1. Ukiwaa na dhiki, mtagombana sana na wapangaji wenzako kufagia,kununua hata LUKU uswahilini n.k, tena mtachukiana Sana na kusemeana mbovu, hata kuombeana mabaya kwa Mambo madogo tu n.k lakini Ukweli Ni kwamba Ni vile mnamaisha ya dhiki tu!

2. Ukipanda daladala bahati mbaya uguse wigi la mtu atakavyokuangalia utazani umegusa roho atakuwakia, au ukimkanyaga mtu bahati mbaya anawaka hatari yaani hujakaa sawa Utasikia konda naye anapita na minguo yake michafu nakukuamlisha sogea nyuma Mara sogea mbele, yaani mtu hadi unatamani siku ukiwa na Gari lako umuoneshe huyo anaekusumbua;

Kumbe hayo yote Ni mawazo ya dhiki, UKIPATA GARI/ UKIJENGA NYUMBA YAKO wala hutakaa ukutane nao tena hao watu, Vituo vya daladala utavisahau, kuchangia LUKU itabaki story!
Ukiwa na nyumba yako mwenyewe, au Gari lako mwenyewe adui zako watakuwa wengine kabisaa tofauti na matarajio yako, Ukiwa na Gari Adui zako watakuwa wenye magari wenzako watakuchomekea kwenye foleni unune hatari, Adui zako watakuwa Ni Traffic watakuandikia makosa Hadi uone Dunia chungu.

Yaani pesa inatabia ya kuja na maadui wapya kabisa tofauti na matarajio yako!
Nimejifunza kumbe dhiki huleta malengo na adabu, Kinachotakiwa ni kuvumiliana tu!

Nimejifunza Adui Ni kama Siraha unamchonga mwenyewe ili aje akuue

Unaweza ukawa unafanya/Unasaidia kwa wema, lakini fanya hivyo usitarajie fadhila za wema, Utakuja kulipwa machungu kuliko matarajio yako!

Kama umewahi sikia kinyago ulichokichonga kinaweza kukutisha ndivyo hivi!

Nitawapa mfano hai!

Kuna wanasiasa wanaitwa SILINDE na NASSARI!
Hawa watu walikuwa makapuku; MBOWE Akawasimamia vyema;
Chadema walikesha kulinda kula za NASSARI akiwa bado kinda kabisa Hana hata Mia mbovu!

Vivyo hivyo kwa SILINDE Akiwa chuo kikuu UDSM akisoma BCOM! hakuwa na mbele wa nyuma, migomo ilipotokea chuo akafukuzwa, MBOWE na chama chake wakamnunulia SUTI na kumsimamia Agombee, akagombea akiwa bado mwaka wa pili chuo akashinda Ubunge! baadae Ndipo Chadema kikawasimamia kesi akarudi kumalizia chuo akiwa MBUNGE, (HATA KAMA MBOWE KAKOSEA) Hakustahili kumtusi na kejeli alipaswa kuondoka kimya kimya tu!
Vivyo hivyo kwa NASSARI na LIJUALIKALI wote Hawa Ni Watoto Walipaswa kuelewa Nani kawatoa JALALANI kabla ya kumtusi mtu mzima (Hata Kama ana mapungufu)

Hii ndiyo dhana ya kutengeneza Siraha halafu inakuumiza mwenyewe!

Mifano ipo mingi! Wangapi mmepokelewa maofisini huko mkiwa hamjui kitu, lakini Leo mnawatesa wazee wa watu huko kisa mshajua kazi?

Wangapi mmesomeshwa na ndugu lakini hata salamu tu za kutambua mchango wao hamuwapigii? hata likizo kwenda kusalimia tu hamtaki tena na kibaya zaidi hao watu mnawatuhumu walikuwa wachawi/roho mbaya

KUSEMA UKWELI MAISHA YAMENIFUNDISHA
"Moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema Yote"
 
Umenena mengi, nmepata fkra mpya.
Asante

Back
Top Bottom