Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

So far so good Jamani. Mikimiki ni pale matokeo yatakapoanza kurushwa kutoka vituoni. Hapo tutapata picha vizuri.
 
Pocha kama ujafanya tafiti usiongeze!! Yaani unasifia TV ambazo zinaonesha recorded, tune Azam Tv upate habari za instantly na zisizo na upendeleo! Tv zako hizo ni za mlengo wa mgombea fulani

Mkuu mi ugomvi wangu ni television ya Taifa, bahati mbaya sina Azam TV hapa nilipo. Nakushukuru kwa kuongeza Azam TV kwenye list hii. Mi kwangu kwa mantiki ya coverage ITV na EATV wamefanya vizuri kuliko hizo zingine
 
Wewe nawe mshamba tu kama hutapiga kura!
Unajua nia yao lakini kuna wasamaria walishajitolea kuwasafirisha wanachuo popote walipo wakapige kura,
Kwa hiyo kama ulikuwa umejificha utakuwa umechangia kujinyima HAKI yako mwenyewe.
 
Mbona watu wamesafirishwa? Mimi nilijiandikishia Arusha na nimepata usafiri wa bure...
 
Hivi ni kwann tume imeamua kutunyima haki yetu ya kupga kura cc wanachuon tuliojiandikisha vyuoni but now tupo likizo ma-kwetu.Nimefanikiwa kufka vituo viwili hapa Dodoma lkn hkuna form no 16 Kwa ajili ya wanachuo.Nahisi co haki kikatba!!!Tupeane mtazamo.

Inauma lakini haitawasaidia
 
Mwanachuo wa wapi wewe! hakuna mwanachuo sharp ambaye amekosa kupiga kura! facilitation zilikuwa za kutosha sana tu!
 
Habari Jf!
Siku ya leo tarehe 25.10.2015 ni siku ambayo watanzania tunafanya maamuzi mazito kwa maslai ya nchi yetu.
Kwa hali ilivyo leo ni tofauti kabisa na matarajio ya wananchi wengi. hali ya usalama ipo vizuri sana, nchi imetulia kimya. mitaani unasikia kelele za ndege tuu na wala si mabomu kama wengi walivhotarajia.
Nadhani hata yale magari waliyonunua 777 hayana kazi katika uchaguzi huu. Ila sijasema ni matumizi mabaya ya hela za walipa kodi.
Kwa suala ya usalama hongera sana mheshimiwa Rais.
Ila upande wa pili wa hili zoezi kuna dosari za kura feki kukamatwa kila pande ya nchi pamoja na majina mengi ya wapiga kura kutokuwepo kwenye daftari.
Hili la kukamatwa kwa kura feki vipi mbona mheshimiwa upo kimya na tume nayo ipo kimya?
Naomba hili la majina kutokuwepo kwenye daftari wakati watu wanavitambulisho halali lifanyiwe kazi haraka lisitutie dosari.
Ukitatua haya mawili mkuu nadhani utaipa nchi yetu heshima kubwa sana kimataifa. Hata kina Paul Kagame wataamini democracy tunayoihubiri Tz ni ya kweli kabisa.
 
Hivi ni kwanini tume imeamua kutunyima haki yetu ya kupga kura sisi wanachuo tuliojiandikisha vyuoni but now tupo likizo ma-kwetu.

Nimefanikiwa kufka vituo viwili hapa Dodoma lakini hkuna form no 16 kwa ajili ya wanachuo.Nahisi sio haki kikatba!

Tupeane mtazamo.
CCM walisha wadharau wasomi wa kitanzania.wakati mko yvuoni zoezi la kuandikisha wapiga kura lilifanyika na tume haikusema vyuo vifungwe ili watu wakajiandikishe makwao ama kutafuta utaratibu unaofaa kuhakikisha wanavyuo wanapiga kura lakini leo hii wakati wa kupiga kura wameamuru vyuo visifunguliwe ili wanavyuo wapige kura makwao huku tume ikijua hamkujiandikishia huko mliko.connect dots.
 
Wanajituma na kuwajibika kwa bidii sana. Wanamenipa maelekezo kwa ufasaha sana na walicho ni furahisha zaidi wanasaidia mpaka kukunja karatasi ya kura.
 
Hujui wewe. Wananchi wananchi munaachwa mupige kura kwa wingi ili usiku waibe uzuri, jana tu kura 8 milion zimesambaa nchi, mumekamata gari mbili tu. Usiondoke linda kura
 
Tbc wengi pale ni mambumbumbuuu wanaonyesha vikatuni muda huu utafikil hamna jambo muhm la kitaifa.
 
Back
Top Bottom