Matukio matano ambayo yalitawala Bunge la 11 la Tanzania 2015-2020

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Bunge la 11 la Tanzania (2015-2020) linatamatishwa leo Jumanne Juni 19, huku likiwa limegawanya mitazamo ya wachambuzi wa masuala ya siasa.

Bunge hilo likiwa chini ya Spika Job Ndugai linatajwa kutofikia viwango vya ubora wa Bunge la 9 na lile 10 chini ya Maspika Anne Makinda (2010-2015) au Samuel Sitta (2005-2010).

Job Ndugai alichaguliwa Spika wa Bunge la Tanzania mnamo Novemba 17 mwaka 2015 baada ya kumshinda mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA. Katika uchaguzi huo Ndugai alipata kura 254 dhidi ya 109 za Ole Medeye kati ya kura 363.

Yafuatayo ni mambo matamo yaliyotikisa Bunge hilo.

Kufutwa 'Bunge Live'


Januari 27, 2016, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye alitangaza umma kusitishwa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya bunge.

Licha ya vyombo vya habari binafsi kuwa tayari kutumia gharama zao kurusha matangazo ya Bunge mbashara lakini Bunge la Ndugai lilitupilia.

Kushambuliwa na kufukuzwa ubunge Tundu Lissu

Hadi Bunge linafikia tamati sakata la kushambuliwa Tundu Lissu halijapatiwa majibu hadi leo, hakuna aliyekamatwa wala kupandishwa mahakamani juu ya tukio hilo

Shambulizi la Septemba 7 mwaka 2017 dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ni moja ya matukio makubwa kuwahi kutokea katika historia ya siasa za vyama vingi nchini Tanzania.

Namna ambavyo tukio hilo limeshughulikiwa na bunge pia ni moja ya mambo ambayo yanapigiwa mfano wakati wa kukosoa miaka mitano ya bunge la 11.

Mvutano wa 'Bunge dhaifu' kati ya Spika na CAG

Mvutano kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kuhusu udhaifu wa Bunge ulichanja mbuga na kuibua mjadala mkali dhidi ya uongozi wa Bunge ambao mnamo Januari 7 mwaka 2019 ulitangaza kumwita CAG bungeni kwenda kujieleza.

Hama hama na kufukuzwa wabunge

Bunge la 11 limeshuhudia wabunge zaidi ya 8 wakihama upinzani kwenda kujiunga CCM pamoja na mbunge wa CCM Lazaro Nyalandu kujiunga na upinzani.

Wabunge wa upinzania waliojiunga CCM na kurejea bungeni baada ya kushinda chaguzi ndogo ni Maulid Mtulia (Kinondoni), Dk. Godwin Mollel (Siha), Julius Kalanga (Monduli), Mwita Waitara (Ukonga), Marwa Ryoba(Serenteti), Pauline Gekul (Babati Mjini), Lazaro Nyalandu (Singida kusini). Joshua Nassari (Arumeru mashariki) alipoteza ubunge wake baada ya kutohudhuria vikao vitatu mfululizo.

Virusi vya Corona

Virusi vya corona havikulitikisa bunge la Tanzania peke yake bali ofisi na sehemu mbalimbali ndani na nje yanchi hiyo.

Kwa Bunge la Tanzania, kama ilivyotokea kwa mabunge mengine ulimwenguni taratibu za kiuendeshaji zilibadilika kabisa.

Hata hivyo, bunge hilo ambalo lilikuwa katika mkutano wake wa mwisho wa bajeti, halikusitisha kabisa vikao vyake kama baadhi ya nchi zilivyofanya.

Hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya vyama vya upinzani pamoja na wanaharakati.

Bunge la Ndugai liliingia kwenye migogoro ya mara kwa mara na wabunge wa upinzani, na sakata la corona pia lilizua mgogoro mwengine baina ya Spika na wabunge wa Chadema.

Spika Ndugai aliwazuia wabunge wa Chadema kutoingia bunge hadi wahakikishe wamelipa posho walizolipwa kwa madai hawakufanyia kazi. Pia aliwapa sharti kuwa wataruhusiwa kuingia bungeni ikiwa watawasilisha vyeti vya kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona.

Mambo matano yaliyotikisa 'Bunge la Ndugai'
 
Back
Top Bottom