Matukio haya ni ya Makusudi ama ndiyo utendaji wenyewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matukio haya ni ya Makusudi ama ndiyo utendaji wenyewe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Nov 7, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Baada ya kutafakari kwa undani leo nimeona wacha niulize hapa hapa nisikie wewe wasemaje.

  Waandishi wanachanganyikiwa na kushindwa kufuatilia matukio haya hadi mwisho ama ni kitu gani hutokea baada ya tukio kugusa hisia na maisha ya Watanzania baadaye kuishia hewani tu ?

  Hivi kesi hizi ziko wapi ?

  1.Wizi wa pesa za na risasi kuwaka hadharani pale Ubungo ?
  2.Mahalu sasa nguvu ya kutueleza maendeleo ya kesi yake inapungua ?
  3.kubenea kufungiwa kwa uchochezi ni njis ys kumzima kwa kuwa ndiye pekee mzamiaji wa habari hizi bila uoga ?
  4.Kesi ya Muhimbili na upasuaji iko wapi ?
  5.Kesi ya majengo 2 ya Keko na Upanga ziko wapi sasa ?
  6.EPA nayo itazimwa na tukio lipi lijalo ?

  waandishi ni kwamba wame elemewa na habari hizi hadi wana acha kutupa ukweli wake ama ndivyo ilivyo Sirikali ya CCM kufunika matukio na Watanzania tunaenda kwa ushabiki ?
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Lunyungu, ni jambo la kushukuru kwamba wewe upo hapa jamvini.
  Umeamua kuziba hili pengo la mrengo mwingine usio wa "Breaking News". Tafadhali endelea kuvaa hivyo 'viatu'.

  Wengine ambao nao wamekuwa wakiziba hili pengo kila wanapopata nafasi ni pamoja na Mwanakijiji.
  Asante ndugu, Mungu awabariki!  .
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Tuko katika ngumu .Wakati wako dhoofu kabisa lakini wanaamua kuuza utu wao kwa kofia ama chai na nauli ya leo .Wachache watasimamia haki na kupiga makelele kila wawezpo.Watanzania wote tunapaswa kuweka kumbukumbu zetu na kuwahoji hawa viongozi kila mara wajapo na porojo zao kuomba lolote kwetu .Naomba mzidi kunikumbusha ni nini matokeo ya matukio haya ama ndiyo mbinu za utawala bora kila issue ikisha kuwa kubwa na wanashindwa kujinasua basi wanakuja na mitego yao ?
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nikawa nimeasahau na tukio la mkuu Nyari na wizi wa silaha kule AR
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama sikosei, kesi ya Nyari ilishaisha na hukumu kutolewa siku nyingi.
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tatizo wengine wa waandishi ni njaa kali. Sasa imekuwakama BONGO FLEVA inavuma baada ya muda inakwisha utamu. Hii ndo fashion ya uandishi wa kisasa. Unapeleka sokoni kinachouzika.
  Tuliwahi kushuhudia watu wakimkejeli Kubenea eti hana jipya zaidi ya Lowasa tu?
  Hivi ndivyo watu wanavyotaka. Raha ya andazi ulile la moto likipoa sio zuri.
   
Loading...