musicarlito
Senior Member
- Dec 29, 2020
- 176
- 289
Ni kweli ipo siku tutakufa, lakini hali hii haizoeleki.
Mara nyingi yanatokea matukio ambayo karibu yachukue uhai wetu mathalani ajali, magonjwa nk. Huwa tunasema ..."kama Mungu tu" lakini kwa tunaoamini Mungu kweli huwa ni Mungu ameepusha, ashukuriwe.
Yafuatayo ni matukio ambayo siwezi sahau.
Nikiwa mdogo sana kama miaka 8 niliwahi dumbukia kisimani, nikazama mara ya kwanza naibuka bahati nzuri kuna dada alikua anafua nguo jirani akaja kuniokoa.
La pili, ilikua kwenye ajali ya mpira wa miguu...nilipanda mpira ukiwa kwenye 'motion' nilirushwa juu nikaangukia sehemu ya nyuma ya kichwa(kisogo)...nilipoteza fahamu...walioniona wanasema nilitoa povu na damu nashukuru wapo waliojizatiti kunipepea mpaka nikaamka wengine walikimbia siwalaumu mimi pia muoga kuona ajali ila najifunza, nilipoteza fahamu dish lilirudi katika hali yake baada ya muda ila mpaka leo nna matatizo ya kusahau.
Mengine ni ya kukoswa koswa na mgari barabarani
Wewe unakumbuka lipi au yapi?
Tuendelee kumshukuru Mungu...NB kunusurika haimaanishi ambao hawakunusurika wamepewa adhabu