Matukio 10 Yaliyotikisa Bunge la Tisa 2006-2010

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Bunge la tisa linamalizika leo likiwa na matukio mengi yaliyoitikisa na kukumbukwa katika historia ya Tanzania. BUNGE hili la tisa lilikuwa na Wabunge 320 kati yao tisina na nane(98) walikuwa ni Wanawake na 44 walikuwa ni wa Kambi ya Upinzani wa Vyama vya CUF,UDP,CHADEMA na TLP,ambacho baadaye kiti chao kimoja kilipotea baada ya Mbunge wake pekee Phares kabuye kufariki dunia mwaka jana na kiti hiki kuchukiliwa na CCM.

Bunge hili liliongozwa na mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta akisaidiwa na Naibu Spika Mama Anna Makinda Mbunge wa Njombe Kusini.

Viongozi hawa walikuwa pia wakisaidiwa na Wenyeyviti Jenista Mhagama Mbunge wa Peramiho,Job Ndugai Mbunge wa Kongwa na Zuberi Maulid Mbungewa Kwamtipura. Wote tunafahamu kuwa Wabunge wengine hawatarudi tena Bungeni wengine wakiwa wameaga kuwa hawatagombea tena. Wengine hawatarudi kwakuwa watapoteza viti vyao.


Matukio hayo yakukumbukwa ni kama ifuatavyo;


1. Kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri Mkuu Edward Lowassa-Feb 2008

Itakumbukwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa Mbunge wa Monduli alituhumiwa kuhusika katika kashfa ya utoaji wa Zabuni ya kuzalisha umeme kwa Kampuni ya Richmond. Lowassa alijiuzulu pamoja na Mawaziri wengine wawili,Ibarhimu Msabaha na Nazir Karamagi waliowahi kuwa Mawaziri wa Nishati na Madini. Kujiuzulu kwa Lowassa kulimfanya Rais Kikwete kuunda Baraza jipya la Mawaziri chini ya Mbunge wa Mpanda Mizengo Peter Kayanza Pinda.


2. Kusimamishwa kwa ZittoKabwe

Tukio la Kusimimsihwa bungeni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe mwaka 2007 ni moja ya matukio yaliyotikisa Bunge na nchi kwa ujumla baada ya Zitto kufungiwa kuhudhuria Vikao vyote vya Bunge kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Agosti-2007. Zitto alisimamishwa baada ya kudaiwa kulidanganya Bunge alipomtuhumu aliyekuwa Waziri wa Nishati na madini Nazir Karamagi kudanganya kuhusu Mkataba wa madini aliotia saini Hotelini London Uingereza. Miezi michache baadye Nazir Karamagi alijiuzulu nafasi hiyo.


3. Wabunge wa CUF Kugomea Vikao

Itakumbukwa pia Aprili 2008 Wabunge wa CUF waligomea bunge na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakipinga kucheleweshwa kwa mazungumzo ya muafaka baina ya Viongozi wa CCM na CUF.


  1. Vifo vya Wabunge
Katika Bunge hili la tisa wabunge tisa walifariki dunia katika mazingira tofauti tofauti. Wabunge hao ni Amina Chifupa, Chacha Wangwe, Benedict Lusorutia, Salome Mbatia, Richard Nyaulawa, Faustine Rwilomba, Sigfrid Ng'itu, Juma Akukweti na Phares Kabuye. Itakumbukwa kuwa vifo vya Amina Chifupa,Chacha Wangwe,Salome Mbatia na Phares Kabuye viliacha gumzo kubwa mpaka hii leo.

5. Waziri Mkuu Pinda kulia Bungeni


Mwanzoni mwa mwaka jana Waziri Mkuu Pinda alijikuta akiangua kilio alipokuwa akitetea hoja ya kuhusu matatatizo yanayowapata Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino). Pinda liangua kilio hicho alipokuwa akijibu hoja ya wapinzani kupinga kauli yake alipoeleza kwamba wauaji wa Albino nao pia wauawe.



6. Wabunge Kuchukua Posho mbili

Itakumbukwa kuwa kulikuwa na mivutano baada ya wabunge na Edward Hosea mkurugenzi wa TAKUKURU aliyetaka wabunge wachunguzwe kwa kupokea posho mara mbili .Hosea alikuwa akiwalenga Wabunge waliokuwa wamejipambanua kama Makamanda wa kupinga ufisadi hasa baada ya sakata la Richomd.


7. Hofu ya Ushirikina

Itakumbukwa pia Bunge lilikumbwa na hofu ya ushirikina baada ya baadhi ya wabunge kudai kwamba kuna unga uliomwagwa katika viti vyao ambao ulidhaniwa kwamba haukuwa salama. Hofu hiyo ilipelekea Spika Sitta kuamua kwamba unga huo upimwe na Mkemia Mkuu wa Serikali. Lakini ilibainika kuwa Unga ule hakuwa na madhara yeyote.


8. Ajali ya Mudhihir

Tukio jingine la kukumbukwa ni lile la ajali ya Mudhihir Mudhihir Mbunge wa Mchinga.Mudhihir alilazimika kukatwa mkono na baadaye kuwekwa mkono wa bandia. Ajali ilikuzua gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari na mawasiliano.


9. Kuzima kwa Vipaza Sauti

Itakumbukwa hivi karibuni jengo jipya la Bunge lilipata hitilafu na kusababisha vipaza sauti kushindwa kufanya kazi.Bunge lililazimika kuhamia kwenye ukumbi wa zamani wa Pius Msekwa ili kuendlea na shughuli za Bunge baada ya kusbiri kwa takribani saa moja wakisubiri vitengamae.Ikumbukwe kuwa jengo hili ni miongoni mwa majengo ya kisasa barani Afrika.


10. John Cheyo kuvuliwa kuwa Msemaji wa kambi ya Upinzani

Mbunge wa Bariadi John Cheyo ameingia katika historia mpya ya kuvuliwa uwaziri kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kuwa kinyume na msimamo wa kambi ya upinzani. Uamuzi huu ulifanyika baada ya Cheyo kubainika kuwa alisaliti uamuzi wa pamoja wa kutounga mkono bajeti ya Serikali iliyokuwaikiptishwa.
 
No 1 itaendelea kuwa Moja kwa muda wa kutosha tu..!
La USHIRIKINA liliniacha hoi..manake ule 'unga' ulifikaje au kuna wale wadudu wanaobungua mbao?
 
duh.....waafrika hasa tunakufa duh! ajali na maradhi kwa kila mtu tu
 
8. Ajali ya Mudhihir

Tukio jingine la kukumbukwa ni lile la ajali ya Mudhihir Mudhihir Mbunge wa Mchinga.Mudhihir alilazimika kukatwa mkono na baadaye kuwekwa mkono wa bandia. Ajali ilikuzua gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari na mawasiliano.


Wengi walisema hii ilikuwa ni laana aliyopata Mudhihir, kwani yeye alikuwa ni mbunge wa kwanza kuomba Mh. Zitto affukuzwe bungeni.
 
8. Ajali ya Mudhihir

Tukio jingine la kukumbukwa ni lile la ajali ya Mudhihir Mudhihir Mbunge wa Mchinga.Mudhihir alilazimika kukatwa mkono na baadaye kuwekwa mkono wa bandia. Ajali ilikuzua gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari na mawasiliano.




Wengi walisema hii ilikuwa ni laana aliyopata Mudhihir, kwani yeye alikuwa ni mbunge wa kwanza kuomba Mh. Zitto affukuzwe bungeni.

Na ndio maana ni tukio la kukumbukwa.
 
Mi kuna jingine ambalo kwangu pia nililichukulia la ajabu; pale mawaziri (na wabunge wa CCM) walipolazimika kuingia mtaani kuitetea bajeti ambapo baadhi walirushiwa mawe...
 
Mh Spika 6 kumwonya Naibu wake asiparamie mambo amsubiri mpaka arudi toka safari! Baadaye alikujaomba radhi!
 
Halikutokea ndani ya Bunge lakini lilibadili misimamo ya Wabunge wengi wa CCM. Nalo ni Spika Sitta kujadiliwa vikali ndani ya vikao vizito vya CCM. Baada ya hapo Richmond ikafa kifo cha mende, wapambanaji wa ufisadi wakawa hivyo walivyo sasa......
 
Back
Top Bottom