Mattaka na mjomba wake washikilia magari ya ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mattaka na mjomba wake washikilia magari ya ATCL

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 22, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Habari zilizotufikia hivi punde na zenye uhakika zinasema lile sakata la magari
  lililokuwa likipigiwa debe hapa jamiiforums kutokana na ubadharifu kampuni ya ATCL sasa limefikia mahali pake,wakati tukienda mitamboni TAKUKURU nao wamekuwa wakilifuatilia swala hili na kuna baadhi ya docs ziko mkononi
  zinaionyesha mh MATAKA alishiriki kumpa mjomba wake tender ya kununua magari ya atcl 26...katika hilo kuna docs zinaonyesha magari hayo kama mtumba mashangingi yamenunuliwa kwa million 65 wakati bei halisi kule dubai ni sh million 18 mpaka 20,,
  Baada ya kupewa tenda ya kuleta magari haya toka dubai mjomba huyu alifanya pati kubwa iliobaki kuwa taarifa pale masai inn kinondoni na kuwashirikisha watu wote wanaouuza magari kujipongeza kupata mlo wa atcl....na kuna baadhi ya picha zikionesha mjomba akipeana cheers na waalikwa akiwemo mh mattaka,..
  Kashfa hii imefikia pabaya nakumbuka nikiwa Bongo ilivuma sana na taarifa zilizotufikia hivi punde baada ya kuletwa magari hayo..mjomba mattaka aliyapeleka yote kwenye yadi .yake akishirikiana na mattaka..yakisubiri kulipiwa kodi..na huku mh mashaka(MJOMBA) akipokea pesa za ATCL USD 3750 kila mwezi!!!
  mpaka leo hii kuna ushahidi wa makaratasi yametolewa magari 8 tu kati ya 26magari haya yameletwa toka mwaka jana na MH MATTAKA amekuwa akilikwepa sana swala hili maana akijua linamgusa moja kwa moja...kuna baadhi ya docs tumewasilisha TAKUKURU natumaini wanazifanyia kazi naaomba muwe wapole tusubiri watafanya nini...swala hili si swala la kumfukuza mtu ni swala la kufikishwa mahakamani kwa kuhujumu mali ya umma.....

  TUKIO LA AJABU
  kumekuwa na mawasiliano mengi na uongozi wa atcl kuhusu magari yaliyopo pale nyumba ya makao makuu yao atcl. mwandishi wetu amekuwa akiulizia kila siku haya ni magari ya nani na mbona yamechakaa sana alipoweza kumfwata mh mattaka ambae akuweza kutaja uhalali wa magari yale ....
  kilichomchanganya ni kitendo alichoelezwa kwamba magari yale yametolewa BOND laikini hayajalipiwa kodi!!!
  Bado swali langu najiuliza najihisi ningekuwa tanzanania ningemuuliza maswali mengi sana mh mattaka

  1))Wapi ameona GARI lisilolipiwa KODI likatolewa BOND na kuwekwa sehemu ya mtu binafsi ama uraiani.

  2)) TRA mnajua hili kuna magari ya ATCL yametolewa BOND na ayajalipiwa...
  je kuna sheria kama hii ambayo nahisi makuwa mmeianzisha si chini ya masaa 6
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  hii story niliisikia siku nyingi kidogo kwamba jamaa aliiba kweli kwenye dili la magari na kibaya kampa tender ya kuleta magari huyo ndugu yake...
  but what i know huyu mjomba wake kipindi mattaka alikuwa choka mbaya
  kiasi chakwamba akinunuliwa bia anaibadilisha na hela kwa kumuachia anaeuza sh 150,,,huyu mjomba wake ndie aliejitolea kumsaidia na kumtoa mpaka hapo mnapomwona.....ndugu zake engi walimtosa maana alivyokuwa PPF alikuwa anawasaidia VIDOSHO tu majimama huku ndugu zake wakiteketea na hali ngumu.....naona ameamua kulipa fadhila.....
  hii ndio serikali yenu mtafanyaje
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili si la kufumbiwa macho kama mnasema ni la siku nyingi haimaanishigharama Umma ulizoingia ni bure!!.Iweje mtu huyu aendelee kupeta tuu,akiuguza majeraha ya wakati huo kwa gharama za walipa kodi wa nchi hii.Huu uswahiba kwenye dhamana za umma tunautazamaje Watanzania??Hivi kweli hatuna njia mbadala ya kuepukana na maudhi haya?Kura tu , kura tuu!!Kwani hata 2010 ni mbali katika mtizamo kama huu !Je JK anapowateua watu wenye kashfa kwa kulinda umtandao hatima ya nchi itakuwaje?Na mbona mambo haya yanajirudia kila kunapoitwa siku nyingine?Kodi zetu zinachezewa na watu wachache,Maisha ya Mtanzania yanazidi kuwa duni,Lakini kibaya ni kwamba hata upeo wetu wa kuona na kufikiri unazidi ku-diminish.Hapa tulipo tunapaswa kufanya mageuzi ya kifikra ndipo tusonge mbele.Kwa kujua tunataka nini na kwa wakati gani.Kama tunadhani tunaelewa shida yetu ni nini basi hatuna budi kuelekeza nguvu yetu kule kulikokuwa na tatizo.

  Na kama hatujaelewa shida yetu tunadhani tutaelewa lini?
   
 4. M

  Mr II Senior Member

  #4
  Feb 23, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nashukuru waheshimiwa kwa kutuhabarisha na kutukumbusha kashfa za mheshimiwa huyu aliyepewa kuongoza shirika letu la ndege kwa uswahiba. Sina hakika kama chama tawala na walio madarakani wanauzalendo wa kweli na nchi hii. Huyu mheshimiwa alikuwa na kasfa inayofanana na hiyo PPF, JK kwa kupenda uswahiba wa kichama na kwa kujidai hajui hilo akampa kuongoza tena ATCL. Hivi ni kweli raisi hana washauri?, nchi ilikosa watu wa kuongoza shirika kama hilo?. Kwa sasa tutajiuliza maswali mengi na hatuta pata majibu. Nchi zingine kabla mtu hajapewa uwaziri au baadhi ya vyeo vikubwa hufanyiwa 'vetting', kwa lengo la kumfahamu mtu kwa undani kabla hujamkabidhi madaraka. Nasi tungeanzisha mpango huo pia. Dunia hii waweza pata chochote upendacho, swali litakuwa kwa gharama zipi, sisi ndio tulioiweka serikali hii madarakani,tunatakiwa tuwe na uwezo wa kuwawajibisha. Mwakani uchaguzi, watakuja kutudanganya tena. Mimi kwa muono wangu, nchi ilikotoka, ilipo, na inakokwenda ahadi za maisha bora kwa watanzania wote ni ndoto. Sasa tujadili hawa tulio wapa madaraka wapo hivyo na sidhani kama watabadilika je tufanye nini?
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii Tunaita ukosefu wa uongozi bora. Wenzetu kuna kitu wanaita "third part" disclosure baada ya kugundua kuwa CEO's na managers wanatumia njia ya kuanzisha miradi na kuwapatia tender watu wao ambao most of the time the real cost of these projects are lower than the amount allocated.

  Sasa kinachofanyika ni kwamba unatakiwa kueleza uhusiano wako na unayempa tender na ikigundulika umedanganya (Lazima watagundua tu) ni kosa la jinai. Sasa sisi Tanzania huu umekuwa ni mchezo wa watendaji wetu kwa miaka nenda miaka rudi na kila mtu anaufahamu na wanaoucheza wanasifiwa kuwa "wajanja" watu wa mjini.

  Mifano ya haya mambo ni mradi wa Vitambulisho vya raia nao ni mkondo mmoja na dili hizi. Sasa umefika wakati sheria zichukue mkondo wake kama tunaitakia mema nchi yetu. Vinginevyo miaka 10 ijayo tutakuwa "Law of the jungle" struggle for existence survival for the fittest. Kama haupo kwenye system wewe ni wa kuliwa tu mpaka kizazi chako na vitukuu, hali itakayofanya watu waingie mitaani na marungu sasa kuchukua nao kwa nguvu (Mfano ni KIBOKO MSHELI)
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mattaka,
  Kama kuna watu wanafikiri UKUTA WA BERLIN milele hauanguki basi ni kama huyu Mattaka. Badala ya kukimbia siku nyingi, kang'ang'ania hapo hadi waje wamuumbue.

  Nafikiri kuna haja asikilize wimbo huu wa Kenny Rogers ajue nini alitakiwa afanye zamani.

  [ame=http://www.youtube.com/watch?v=kn481KcjvMo]YouTube - Kenny Rogers - The Gambler[/ame]
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  MATATIZO MENGINE YAPO TRA
  nilisoma kwenye hiyo issue ya magari ya nyuma ya office za ATCL na cha kuwaambia kinasikitisha sana ,yale magari si ya ATCL yaliletwa kwa MGONGO WA MAGARI YA ATCL....KUNA DOUBLE COASTER 2 NA HIACE MOJA...NILIPOPANDA JUU NILIKUMBANA NA MMOJA WA WAH HAPO JUU ALINIMWAGIA YOTE

  DOUBLE COASTER NO ....1 ILE YA KWANZA KUSHOTO NI GARI YA ELIASAPH MATHEW HUYU ALIKUWA CFO WA ATCL...LAKINI MAJUZI UJUE UPUUZI WA HII NCHI WAMEMTOA WANAMPA CHIEF AUDITOR,,HAYA

  ILE NYINGINE DOUBLE COASTER NI YA MH ALIEONDOLEWA MAJUZI KWENYE POST YA
  DIR WA OPERATION...NILIPEWA JINA LAKE NDEFU KIDOGO NIMELISAHAU

  ILE HIACE MOJA ILIOPAKI PALE NI YA MH SANA """"DM""" NANI FUMBUA MWENYEWE

  HIVI NDIVYO NCHI INAVYOLIWA....
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Haa!Watu wanahoji kama Rais hana washauri,
  Hivi hamjui Kikwete alivyo mbishi.jamaa hapendi kushauriwa,si mnajua jamaa mjeda.?
  Napenda kueleweka kuwa KIKWETE mara nyingi anafyatuka ndo maana hata kule MBEYA 'walimpiga' baada ya kushauriwa na makachero kuwa haipendezi kakaa sehemu mmoja kwa muda mrefu na kuongelea kitu kilekile.jamaa alikataa na matokeo yake akapigwa
   
Loading...