Matrafiki Wanaongoza Magari Wakati Taa Zinafanya Kazi

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Matrafiki Wanaongoza Magari Wakati Taa Zinafanya Kazi

Kwa wale wanaojiunga hivi punde na haya yanayojiri, ambao bado wanajiuliza kwani je vipi somo mbona trafiki kuongoza magari wakati taa za kuongozea magari zinafanya kazi? Hii hapa historia fupi.

Miaka ileeee palizuka kelele nyingi kwa nini askari wa barabarani (a.k.a trafiki) wasiziachie tu taa za barabarani zifanye kazi? Watu wale walidai kwamba taa zikifanya kazi magari hutembea, foleni hupungua na mambo huwa murua kabisa. Tena walizidi kudai kwamba trafiki wanapoongoza magari huku taa zikifanya kazi, husababisha foleni, kwani trafiki hao huita magari ya upande mmoja kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo taa hufanya ambazo huita pande zote sawa.

"Hao trafiki si wangekaa pembeni, wasubiri muda ambao taa hazifanyi kazi?" ndio kilikuwa kibwagizo chao.

Kelele zilikuwa nyingi kweli, japo miaka hiyoooo hakukuwa na mitandao ya kijamii, au tuseme haikuwa mashuhuri kama vile sasa.

Kelele zikawafikia wakuu. Ndipo siku moja wakatoa maagizo kwa trafiki kuziachia taa zifanye kazi, na wao wakae pembeni. Kama vile tu watu walivyokuwa wakipiga kelele iwe.

Asubuhi asubuhi, matrafiki wakaenda kwenye vituo vyao. Madhali taa zafanya kazi, wao "wakala sushi", wakiangalia magari yanavyoongozwa na taa.

Unajua jiji la Dar es Salaam, pale panapoitwa "katikati ya jiji" siyo kati. Ni Mashariki ya Jiji. Magari hutoka kila upande kwenda huko asubuhi, na kurejea jioni.

Hivyo asubuhi kwenye mataa magari yakawa yanakaa foleni ndefu upande mmoja wa kuelekea mjini. Kutokea mjini hakuna foleni. Hivyo taa zikiruhusu magari mawili matatu ya upande wenye foleni, ziliwastopisha na kuanza kuruhusu magari ya pande nyingine. Lakini pande hizo nyingine hazikuwa na magari. Hivyo ilionekana muda mwingi ulipotea kusubiri zamu irudi huku kwenye foleni. Na trafiki alikuwapo hapo kuhakikisha taa zinaheshimiwa.

"Huyu trafiki si angeruhusu tu haya magari ya upande huu? Haoni pande zile zengine hazina magari?" walisema. Na trafiki walikuwa wakali kuhakikisha hakuna gari linalo'antilogi'. Magari yalichelewa sana kuingia mjini.

Kufikia jioni magari yanarudipo nyumbani, hali ikawa hivyohivyo. Watu wakawa wanawabembeleza matrafiki waongoze magari, japo taa zilikuwa zinafanya kazi. Na kelele hazikusikika tena kuhoji kwa nini trafiki wanaongoza magari wakati taa zafanyakazi.


Mabibi na Mababu, hiyo ndiyo historia fupi ya kwanini mpaka leo matrafiki huongoza magari wakati taa zinafanya kazi.
 
Nadhani kwa sababu za kiitifaki ni muhimu kuondoa hii chemicola mezani,au ikiwezekana watumie ile pin code.

Solution itakua kwny kipengele cha overhauling au stress-testing ambayo ni direct proportional to intensity yake.
 
Hizo taa wazifunge na kwenye mabaa au club..haiwezekan wahudumu wakiwa wanaingia kazn hawalipii..ila wakitaka kutoka tu utasikia kalipie kwa MENEJA..
 
Back
Top Bottom