matractor kutoka ulaya

Kingdom_man

JF-Expert Member
May 19, 2010
405
456

Attachments

  • tractor3.doc
    154 KB · Views: 188
  • tractor2.doc
    157 KB · Views: 165
  • tractor 1.doc
    168.5 KB · Views: 195
kuna kigogo mmoja alipewa bure kama msaada alipokwenda vietnam, yalipoletwa umeibuka mradi wa kuuza matrekta wa SUMA JKT. I hope haya hayakuja kwa style hiyo
 
kuna kigogo mmoja alipewa bure kama msaada alipokwenda vietnam, yalipoletwa umeibuka mradi wa kuuza matrekta wa SUMA JKT. I hope haya hayakuja kwa style hiyo

Utakuta hilo likiongozi bado linakumbatiwa katika uongozi na wanalifumbia macho kama vile hawaoni
 
Yanapatikana kwa mkopo, maana naona hii bei kwa mkulima wa Tanzania.....!! Sijui?

Hii ndio bei poa kweli? au macho yangu mabovu?

Ndio attachments za OP zinavyosema hivyo. OP anasahau kwamba kutokana na vipato, upatikanaji wa vipuri na ufundi, watanzania tunatumia matrekta yenye umri wa zaidi ya miaka 20.

Ukipata Massey, Ford, Case, John Deere, Valmet etc ya kuanzia mwaka 1980 ambayo imepiga chini ya masaa 10,000 ya mzigo, inatosha kabisa kufanya kazi na matrekta haya mimi nimeshanunua na hayafiki £7000 kwa moja.
 
Hii bei ni kwa matajiri tu kama akina Lowasa, Sumaye lakini mkulima wa jembe la mkono wa Mgeta, Matombo ni :nono:

Kwa wazee mujini kama nyie mnaweza mkasamehe kununua Vogue mkavuta chombo hicho. Haya matrekta ya A/C bwana
 
Bei zipo katika attachments ni kwenye range ya £25,000 kwenda juu

yaani hiyo £25,000 bado ni chini ndiyo inaanza kupaa hapo? ikiwa hujui hesabu hiyo ni tsh zaidi ya 55 milioni.
Hii post haiko kwenye thread za jokes?
 
Bei zipo katika attachments ni kwenye range ya £25,000 kwenda juu

What? Paundi 25,000? Tatizo la wafanyabiashara ndo hili, serikali inaondoa kodi kwenye matrekta ili watu waweze kumudu kununua ninyi mnataka super profit. Sasa hebu niambie katika hali ya kawaida unafuu uko wapi wa kuuziwa trekta kwa zaidi ya miloni 57 za TZ? wizi mtupu.
 
Jamani tena kwa mkulima wa Tanzania.....sina hakika.labda kama ni wazo la kijiji kununua tena kwa mkopo wa muda mrefu
 
Duh kwa hiyo bei nadhani jembe la mkono litaendelea kushika kasi

Nilifika kijiji fulani huko kusini nyanda za juu,nikasikia hadithi eti kuna mzee mmoja kijijini pale analimisha watu usiku ktk mashamba yake, hii teknolojia itabidi itumike sasa, unafika pale buguruni stand ya daladala au mwenge unafanyizia mateja ili usiku yaje kulima Bagamoyo au mkuranga.Itakuwa poa kweli tehEEeee.
 
Ndugu zangu kuna matractor yanauzwa kwa ajili ya kilimo kutoka uingereza yapo katika hali nzuri kabisa na bei poa, kama tunavyojua hakuna ushuru bandari kutoa vifaa vya kilimo kama tractors kwa ajili ya KILIMO KWANZA!. kama kuna mtu anahitaji basi tuwasiliane kupitia no.+447818716685

See pics of the tractors attached!
View attachment 17277cView attachment 17276hView attachment 17275eView attachment 17277dView attachment 17276!View attachment 17275

Asanteni!
Asante mkuu kwa taarifa. Nimechungulia sehemu ya bei na condition ya kulipata sijaona. Tafadhali kama inaruhusu bandika na bei kabisa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom