Matokeo yangu baada ya kuacha kufanya mapenzi na kunywa pombe kwa miezi 3

Nakuelewa sana sana.

Kanisa katoliki hawakuwa wajinga kuzuia mapadri na maaskofu kuoa. Yani it didnt happen out of blues, walikuwa wanajua wanachokifanya na ndii maana ndio wanaoiendesha dunia kwa sasa.

Wengi hawatakuelewa lakini tupo tunaokuelewa mkuu.

Unforgetable
 
Shida yako Nguzo1 unapenda mambo hayo yakutokee kama yalivyokutokea katika miezi mitatu ila sasa wewe unapenda kuchanganya Mungu na mambo machafu vitu hivi havichanganyani kuwa upande mmoja kama wampenda Mungu acha pombe na zinaa au tafuta mwanamke mmoja oa kabisa Mungu anakupenda sana nguzo1 na anamengi ya kukutendea katika maisha fanya vile Mungu atakavyo kukutendea kuna mengi mazuri yanakuja mbeleni baada ya kujikabidhi mikononi mwa Mungu.

Huu ni ushauri wangu ukitaka ufanikiwe zaidi ufuate ukitaka kumkumbatia zaidi shetani endelea kumshikilia maisha haya ni mafupi na duniani tunapita!!!

Asante kwa kunisikiliza Nguzo1 maamuzi ni kwako mwenyewe!!!
 
Usipo kunywa pombe na kufanya mapenzi utaishia kuwa Masikini, kwa sababu utakua self contented.
 
Just be positive na.uwe mtu wa haki kwa upande wangu nikisema nitende jambo baya au niwaze.kwa.namna fulani negatively basi baadae inakuja kuniathiri mimi kitu kikubwa tu uwe na.mawazo.chanya na fanya.vile.vitu ambavyo.na wewe.pia.unapenda.

kufanyiwa hapo utaenda sawa tu na kama upo kwenye dini usisahau ibada japo.hapa kwenye dini napo.unatakiwa.uwe macho.sana.hasa kama.ni mkristo.....kama ni muislam huna shida sana maana dini inaendana na huo.mfumo.wa haki
Okay asante mkuu nitazingatia.
 
Binafsi nimekuelewa sana sema bahati mbaya sana hadhara ya hapa wengi ni ngumu kukuelewa Mkuu. Sorry.
Tuko pamoja mkuu mimi pia nakosa lugha nzuri ya kufafanua zaidi haswa mazingira na vitu nilivyo experience ndani ya huo ulimwengu mwingine ila nitajitahidi kwa kadri nitakavyoweza!!
 
Nakuelewa sana sana.

Kanisa katoliki hawakuwa wajinga kuzuia mapadri na maaskofu kuoa. Yani it didnt happen out of blues, walikuwa wanajua wanachokifanya na ndii maana ndio wanaoiendesha dunia kwa sasa.

Wengi hawatakuelewa lakini tupo tunaokuelewa mkuu.

Unforgetable
Asante mkuu baada ya kugundua hii hali ya utofauti nikaanza kukomand baadhi ya situation nikiwa ofisini au nyumbani na baadhi vikawa vinanitii. Nakumbuka nilikuwa nina tabia ya kupiga miayo kwa muda wa sekunde tano au kumi sasa nikawa niko ofisini nikaona dalili za kupiga miayo ile nimeanza kufungua kinywa kwenye ubongo wangu/kimoyomoyo nika toa amri "acha kupiga miayo" Na ile hali ikapotea ghafla ikawa ndiyo tabia yangu kila nikiona dalili za kupiga miayo au kupiga chafya naistopisha kama vile unavyozima Tv kwa remont. Wakati nafanzia majaribio hii comand power kwenye vitu vingine ndiyo nikaja kutumbukia kwenye Pombe Natamani sana ule uwezo ujirudie.
 
Shida yako Nguzo1 unapenda mambo hayo yakutokee kama yalivyokutokea katika miezi mitatu ila sasa wewe unapenda kuchanganya Mungu na mambo machafu vitu hivi havichanganyani kuwa upande mmoja kama wampenda Mungu acha pombe na zinaa au tafuta mwanamke mmoja oa kabisa Mungu anakupenda sana nguzo1 na anamengi ya kukutendea katika maisha fanya vile Mungu atakavyo kukutendea kuna mengi mazuri yanakuja mbeleni baada ya kujikabidhi mikononi mwa Mungu.

Huu ni ushauri wangu ukitaka ufanikiwe zaidi ufuate ukitaka kumkumbatia zaidi shetani endelea kumshikilia maisha haya ni mafupi na duniani tunapita!!!

Asante kwa kunisikiliza Nguzo1 maamuzi ni kwako mwenyewe!!!
Hakika mkuu sikujua kwamba ule uwezo niliupata kwa kujitenga na maovu ndani ya hiyo miezi mitatu ningelijua hilo wala nisingefanya mapenzi na kutumia kilevi ila sasa ndiyo nimedhamiria kuacha hizo dhambi na nikifikia uwezo nikiokuwa nao basi mimi na pombe basi na hata mapenzi nitajitenga nayo kabisa na nikizidiwa nitachukua uamuzi wa kuoa.

Nitajitahidi sana kutoshiriki ngono. Wakati nikiwa katika hiyo hali ya ufunuo kuna kipindi nilikuwa nimepumzika sehemu ya uwazi mida ya mchana nilikaa hapo kwa utulivu mkubwa mno baada ya lisaa limoja nikawaona mtu na mpenzi wake wanatembea huku wameshikana viuno kwa mahaba (tuwaite Jack na James) wakakaa meza iliyopo mebele yangu nikaanza kuwawazia (ikaja picha/screen kwenye paji la uso wangu nikaanza kuona jinsi watakavyoagiza chakula na vinywaji nikaona jinsi james atakavyoinuka na kwenda kuongea na mhudumu wa pale wakinongonezana akarudi kukaa na mwenza wake.

Ile screen ikaendelea kunionyesha picha jioni watakavyo kwenda room na kuanza kufanya mapenzi na wakati wanafanya mapenzi kuna watu wengi watakuwa wanawaangalia pembezoni mwa kitanda wakiwa kimya sura zao sikuziona na ni kama mashabiki wa mpira walikuwa wanaangalia penalt inavyopigwa uwanjani huku wakijiandaa kushangilia goli kama penalt ingepenya golini.

jack na james walipofika kileleni nikasikia sauti nyingi za watoto wachanga wakilia kana kwamba wamezaliwa na nikawaona wakianza kuzagaa mle chumbani wakitokea kitandani alikolala jack&james wale watu waliokuwa wanawaangalia pembezoni mwa kitanda waliposikia sauti za watoto wakashangilia na kuanza kuwakamata na kuwatafua kama kumbikumbi na watoto wengine wakawekwa kwenye cage/kitu kama box lilitengenzwa kwa nyavu kisha wakatoweka. Wale viumbe walivyotoweka basi jack alianza kuinuka kitandani kwa taabu sana huku akiwa amebadilika na kukonda sana kama mtu ambae hajapata chakula kwa muda mrefu james yeye aliendelea kulala. Gafla nikaona kama ninapaa hadi juu ya paa la ile hoteli nikapaa juu zaidi nikaanza kuona nyumba za jirani nikapaa juu zaidi kiasi cha kuliona jiji lote la dar es salaam nikiwa angani nikaanza kusikia zile sauti za watoto wachanga zikilia kila kona ya jiji na ile mijitu ikishangilia kwa nguvu zidi nikaanza kutua na kurudi nilipokaa nannikawaona jack na james bado wapo pale mezani nitakata kujua kujua kile nilichokiona ni ndoto au kweli basi nikajisemea kama ni ndoto ngoja nishtuke kutoka usingizini nikafanya kama kukohoa/kusafisha koo kidogo kama vile najiandaa kuongea na sikuona utofauti wa mazingira zaidi ya ile screen kupotea baada ya kukohoa hiyo sikuwa usingizini.

Wakati natafakari mara akaja mhudumu akawaletea chakula jack na james kumbe kweli waliagiza chakula sasa cha kushangaza ni jinsi mhudumu alivyokuwa anawanawisha mikono ni vilevile nivyoona kwenye ile screen muda mchache uliopita yule mhudumu alimwagia maji bahati mbaya james kwenye kiatu na kule kwenye screen niliona hivyo hivyo asee nilistuka sana nikagundua kumbe nilichokiona kwenye screen ndicho kinachokwenda kutokea nikazidi kuogopa haswa nilivyokumbuka kwenye scree niliona wale viumbe wa ajabu wakila wale watoto wachanga moyoni nikajisema ngoja niondoke nisije pata balaa.


Nikamwita mhudumu amwite mhudumu aliyenihudumia ila alichelewa kuja baada ya kama dakika 20 nikalipa bill yangu ila nikasubiria chenchi...chenchi nayo ilichelewa kuja na wakati ananiletea chenchi jack & james walikuwa wamemaliza kula tayari. Ile nataka kuondoka simu yangu ikaita kunagalia simu nikajua aliyenipigia lazima atakuwa na maongezi marefu na mimi hivyo nikakaa mezani ili nikimaliza kuongea na simu ndiyo niondoke. Niliongea na simu kwa muda kama dakika 45 na nilipokata nikaona James amenuka na kwenda Conter kuongea na mhudumu asee huwezi amini jamaa alivyonyanyuka kuelekea counter ni vile vile nilivyoona kwenye screen alivyotembea hatua mbili alirudi mezani na kuchukua simu yake na akaelekea hadi counter.

Hapa nikapata ujasiri wa ajabu nikasema siondoki ngoja nishuhudi. Alivyokuwa conter sikumuona vizuri aliporudi mezani alipomwacha jack kuna kitu alimwambia jack halafu wote wakacheka na jack akampiga kofi la mahaba begani huku wakiendelea kucheka Asee hapa nusu nipagawe tena maana ni kama nilikuwa naangalia movie ya marudio yani alivyompiga kofi begani na walivyocheka ni vilevile nilivyoona kwenye screen nikajisemea hapana hapa siko ndotoni hii ni kweli na nikambuka kwenye screen kuna muda nilipaa juu na kuliona jiji lote la dar nikaingia woga nikasema siko tayari kuendelea kukaa ile sehemu nikaondoka huku nikiwa na maswali mengi sana kichwani.

Wakuu yani hili tukio dogo tu ambalo lilitokea kati ya masaa mawili au matatu kwa kifupi nina mengi ya kuandika na kiukweli naitamani sana hii hali initokee tena.
 
Tuko pamoja mkuu mimi pia nakosa lugha nzuri ya kufafanua zaidi haswa mazingira na vitu nilivyo experience ndani ya huo ulimwengu mwingine ila nitajitahidi kwa kadri nitakavyoweza!!
Ni wachache sana watakaokuelewa hapa.
 
Usipo kunywa pombe na kufanya mapenzi utaishia kuwa Masikini, kwa sababu utakua self contented.
Hapana mkuu halafu kunan kitu nimekuja kugundua ukiwa a nyege/stimulated ni raha sana ukiweza kuzicontroll (yani kucontroll maana yake ni uwe sexually stimulated kwa muda mrefu by using your brain ONLY (hours or days) bila kupizz/ejaculate utapata raha ya ajabu).

Unapofanya mapenzi na mwanamke utamu mkubwa upo pale unapokojoa na ukiweza kukojoa kwa masaa matatu mfululizo unaweza ukafa kwa utamu utakaoupata na sasa ukiweza kujicontroll utaweza kupata same feelings zinazokaribiana na kukojoa na uka experience raha zaidi kwa muda mrefu kuliko ambavyo ungefanya mapenzi na mwanamke ungefika kileleni na baada ya hapo unarudia hali ya kawaida.

Kujicontroll maana yake unaimagine sex event bila kumshika mwanamke au kujishika wewe sehemu yoyote ile au bila kuangalia filamu/picha yoyote ile just stand still/ stay awake and let your brain do the rest and make sure at the end you don't hit/reach orgasim. Yapo mengi ya kuelezea ila ngoja niishie hapa kwa leo.
 
Wahi matibabu mkuu au nenda kawaone watalam wa saikolojia watakusaidia
Pole sana
 
Wakuu heshima kwenu,

Kwa mara ya kwanza nimeweza kujicontroll na kuacha kufanya mapenzi na kunywa pombe kwa muda wa miezi mitatu (kuanzia January hadi Aprill mwanzoni)

Nikiri kwamba nimepata nguvu za ajabu mno na uwezo wa ubongo kuchanganua mambo umeongezeka mara dufu. Nilipokuwa meza moja na jamaa zangu nilikuwa nawapa ushauri na wanaosolve mambo yao 95%

Kubwa katika yote ni kwamba hivi karibuni (Mwezi May 2021) kila nikilala usiku ninakuwa usingizini lakini bado akili yangu inakuwa macho na ninaweza kupanga mipango yangu ya kesho au kuvuta kumbukumbu ya nini nimekifanya kwa siku ya leo Na ninakuwa na feelings za mazingira ya hapa duniani na dunia ingine mpya( Yani tuseme Sebuleni = hapa duniani na Chumbani= Dunia ingine mpya) Sasa ndani ya ubongo wangu ndiyo na switch either Chumbani Au sebuleni na mazingira yanabadilika muda huohuo.

Usiku mida ya kulala Nikifunga macho na kutuliza sehemu zote za mwili na bila kukaza msuli wa aina yoyote ninakuwa sioni tena giza badala yake naona screen mbele ya paji la uso wangu na kuna maandishi yanapita na ninakuwa na uwezo wa kuyasoma na yanakuwa ni kama maelekezo fulani juu ya vitu ambavyo sijawahi kabisa kuona au kusikia popote hata google.

Inafikia mahali najisahau nachezesha kope za macho na hiyo hali inaondoka narudi kwenye ulimwengu huu wa nyama na damu lakini nikitulia baada ya nusu saa naingia tena kwenye ile hali na muda huo ninakuwa najua kabisa kwamba hapa nikichezesha kope za macho au nikijitingisha popote mwilini au kukaza msuli wowote iyo hali itapotea na nikifanya hivyo inakuwa kweli.

Nina mengi ya kusimulia ila nahisi sitaeleweka.

Hapa kati kati nilikuja kujihusisha na mapenzi na pombe kidogo na ile hali ikapotea kabisa. Mwili ukawa mzito, nikiamka asubuhi najiona nimechoka sana, akili inakuwa nzito nashindwa kufikiri kwa haraka na confidence ya kuongea na watu ikapungua.

Sina hakika kama mapenzi na pombe ndiyo chanzo cha kupoteza uwezo wangu ila nimeamua tena kuviacha kwa muda wa miezi mitatu nione kama hii hali itajirudia tena.

Mara ya kwanza niliweza kufikisha miezi 3 kutokana na kwamba niligombana na mpenzi wangu na nikapata safari ya huko maporini kwa muda wotehuo ndiyo maana sikupata chance ya kufanya mapenzi kwa muda huo.

Chakula nilichokuwa natumia ni Mihogo, karanga, Ugali mboga za majani, matunda , maziwa tangawizi ya kutafuna kila siku asubuhi na jioni, hakika mwili ulibadilika na nikawa mwepesi sana na nilijiamini kupita kiasi. Pia nilikuwa na uwezo wa kufikiria mambo magumu na kuyatolea ufafanuzi japo sikuwaji kujifunza kabla. Nilikuwa na uwezo wa kusikiliza watu wawili wakiongea kwa wakati mmoja mfululizo hata kwa dakika kumi na nikawaelewa wote kwa mkupuo.

Yani sijui nisemeje wakuu ila yote haya yameondoka baada ya kulala na mwanamke mwezi huu wa sita huku nikiwa na k-vant kichwani

Itaendelea.....
Ila nyeto unapiga mara ngapi kwa week?
 
Ila nyeto unapiga mara ngapi kwa week?
Hapana ndugu, Mimi na nyeto ni kama Moto na maji yani hatuendani kabisa trust me.

Kufanya mazoezi ya mwili, kuwa bize na kazi, kuepuka mazingira ya ushawishi especially kuwa pekeyako muda mwingi au kujichanganya na makundi yenye ushawishi wa hizo mambo ni baadhi ya njia zitakazokufanya ukae mbali na zinaa.
 
Back
Top Bottom