Matokeo yangu baada ya kuacha kufanya mapenzi na kunywa pombe kwa miezi 3

nguzo1

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
347
530
Wakuu heshima kwenu,

Kwa mara ya kwanza nimeweza kujicontroll na kuacha kufanya mapenzi na kunywa pombe kwa muda wa miezi mitatu (kuanzia January hadi Aprill mwanzoni)

Nikiri kwamba nimepata nguvu za ajabu mno na uwezo wa ubongo kuchanganua mambo umeongezeka mara dufu. Nilipokuwa meza moja na jamaa zangu nilikuwa nawapa ushauri na wanaosolve mambo yao 95%

Kubwa katika yote ni kwamba hivi karibuni (Mwezi May 2021) kila nikilala usiku ninakuwa usingizini lakini bado akili yangu inakuwa macho na ninaweza kupanga mipango yangu ya kesho au kuvuta kumbukumbu ya nini nimekifanya kwa siku ya leo Na ninakuwa na feelings za mazingira ya hapa duniani na dunia ingine mpya( Yani tuseme Sebuleni = hapa duniani na Chumbani= Dunia ingine mpya) Sasa ndani ya ubongo wangu ndiyo na switch either Chumbani Au sebuleni na mazingira yanabadilika muda huohuo.

Usiku mida ya kulala Nikifunga macho na kutuliza sehemu zote za mwili na bila kukaza msuli wa aina yoyote ninakuwa sioni tena giza badala yake naona screen mbele ya paji la uso wangu na kuna maandishi yanapita na ninakuwa na uwezo wa kuyasoma na yanakuwa ni kama maelekezo fulani juu ya vitu ambavyo sijawahi kabisa kuona au kusikia popote hata google.

Inafikia mahali najisahau nachezesha kope za macho na hiyo hali inaondoka narudi kwenye ulimwengu huu wa nyama na damu lakini nikitulia baada ya nusu saa naingia tena kwenye ile hali na muda huo ninakuwa najua kabisa kwamba hapa nikichezesha kope za macho au nikijitingisha popote mwilini au kukaza msuli wowote iyo hali itapotea na nikifanya hivyo inakuwa kweli.

Nina mengi ya kusimulia ila nahisi sitaeleweka.

Hapa kati kati nilikuja kujihusisha na mapenzi na pombe kidogo na ile hali ikapotea kabisa. Mwili ukawa mzito, nikiamka asubuhi najiona nimechoka sana, akili inakuwa nzito nashindwa kufikiri kwa haraka na confidence ya kuongea na watu ikapungua.

Sina hakika kama mapenzi na pombe ndiyo chanzo cha kupoteza uwezo wangu ila nimeamua tena kuviacha kwa muda wa miezi mitatu nione kama hii hali itajirudia tena.

Mara ya kwanza niliweza kufikisha miezi 3 kutokana na kwamba niligombana na mpenzi wangu na nikapata safari ya huko maporini kwa muda wotehuo ndiyo maana sikupata chance ya kufanya mapenzi kwa muda huo.

Chakula nilichokuwa natumia ni Mihogo, karanga, Ugali mboga za majani, matunda , maziwa tangawizi ya kutafuna kila siku asubuhi na jioni, hakika mwili ulibadilika na nikawa mwepesi sana na nilijiamini kupita kiasi. Pia nilikuwa na uwezo wa kufikiria mambo magumu na kuyatolea ufafanuzi japo sikuwaji kujifunza kabla. Nilikuwa na uwezo wa kusikiliza watu wawili wakiongea kwa wakati mmoja mfululizo hata kwa dakika kumi na nikawaelewa wote kwa mkupuo.

Yani sijui nisemeje wakuu ila yote haya yameondoka baada ya kulala na mwanamke mwezi huu wa sita huku nikiwa na k-vant kichwani

Itaendelea.....
 
Mnapovuta bangi muwe mnakula chakula cha kutosha kwanza
Mkuu kwa kifupi tu ni kwamba katika maisha yangu hicho kipindi cha miezi mitatu ndiyo muda pekee ambao nimefanikiwa kukaa mbali na na kutojihusisha na mambo ya kidunia kwa 90% na wala sikupanga nifanye hivyo ila kuna vitu vilinifanya automatically ni jitune kwenye hayo mazingira

Mojawapo ni baada ya kugombana na aliyekuwa mpenzi wangu nilikasirika sana nika block mawasiliano yote na nikasema sitaki mazoea na mwanamke yeyote yule isipokuwa mama yangu tu na nilifanikiwa coz nilikuwa na hasira sana juu ya huyu mwanamke.

Pili mazingira ya kazi yalinifanya niwe mtu wa kuingia jobu na nikitoka ni strainght nyumbani nakula nalala hakuna kweda kijiweni au kupiga misele ya aina yoyote ile.

Tatu kwa kipindi hicho imani yangu juu ya mwenyezi mungu iliongezeka na nilimuuliza maswali mengi sana mungu wangu juu ya maisha yangu and from no where nikawa nalazimisha anipe majibu ya mojakwamoja juu ya mwelekeo wa maisha yangu na lengo la mimi kuwa hapa duniani.
 
You have been awakened, watu wengi kwa sasa hasa wenye asili ya Africa mambo yanabadilika.tena yanakuja automatically bila hata ya wewe ku control, hio ilinitokea pia kwa upande wangu mwanzoni nilikua kama. kichaa ila muda unavyoenda ndo naanza kuuelewa huu ulimwengu mpya wa upande wa pili
 
Wacha porojo. COVID 19 kakuzuwia ujinga ukipenda usipende.
Hapana mkuu nina uhakika kabisa sababu siyo covid bali ni niliamua kujitenga na hayo mambo baada ya kupata hasira kutoka kwa mama watoto mtarajiwa na siku hiyo nilivyogombana nae nikaamua kunywa pombe nyingi nikalewa na kusababisha madhara makubwa sana kwangu na kwa watu wangu wa karibu kwa siku ile na hapo ndipo niliamua kujitenga na wanawake na pombe kwani nilipata hasara kubwa sana.

Hii hali ilivyokuja kunitokea nilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukumbuka mambo mengi niliyoyafanya kwa siku yani hadi nukta niliikumbuka.

Kuna muda nikiwa nimekaa kwenye kiti napata wazo la kumpigia mtu simu ile nashika simu tu inaanza kuita na anaenipigia ni yule niliyekuwa nataka kumpigia mwanzoni niliogopa ila baada ya siku tatu nikaizoea hiyo hali.

Nina mengi sana ya kusimulia
 
You have been awakened...........watu wengi kwa sasa hasa wenye asili ya Africa mambo yanabadilika.tena yanakuja automatically bila hata ya wewe ku control.......hio ilinitokea pia kwa upande wangu mwanzoni nilikua kama.kichaa ila muda unavyoenda ndo naanza kuuelewa huu ulimwengu mpya wa upande wa pili
Mkuu naomba elimu zaidi nna ya ku controll hii hali.

Mimi ilianza kunitokea mwezi wa nne na mwanzoni ilinichangnya nikaanza kuandika kwenye notebook yanayonitokea mfano leo nikiwa katika hali fulani naandika niliyoyaona then kesho yake nakuja kusoma nilichokiandika jana cha ajabu baada ya kusoma nilikielewa sana tena nikakitolea ufafanuzi wa kina yani kuna mawazo yalikuwa yanatiririka kwenye ubongo wangu bila kikomo ule woga ukapotea kabisa na nikaanza kuwa na confidence ya hali ya juu sana.

Natumaini hii hali itanirudia kwani mwezi huu wa sita mwanzoni ndiyo nilishindwa kujizuia nikalala na mwanamke na kupiga ulabu kidogo na ule uwezo wangu ukapotea kabisa. Nimetenga muda wa miezi mitatu tena kwanzia Mwezi huu na sintojihusisha na hivyo vitu viwili hadi niupate ule uwezo wangu.

Mkuu kama kuna namna ya ku controll na ku maintain hii hali tafadhali naomba maelelekezo zaidi.
 
Mkuu naomba elimu zaidi nna ya ku controll hii hali.

Mimi ilianza kunitokea mwezi wa nne na mwanzoni ilinichangnya nikaanza kuandika kwenye notebook yanayonitokea mfano leo nikiwa katika hali fulani naandika niliyoyaona then kesho yake nakuja kusoma nilichokiandika jana cha ajabu baada ya kusoma nilikielewa sana tena nikakitolea ufafanuzi wa kina yani kuna mawazo yalikuwa yanatiririka kwenye ubongo wangu bila kikomo ule woga ukapotea kabisa na nikaanza kuwa na confidence ya hali ya juu sana..
Just be positive na.uwe mtu wa haki kwa upande wangu nikisema nitende jambo baya au niwaze.kwa.namna fulani negatively basi baadae inakuja kuniathiri mimi kitu kikubwa tu uwe na.mawazo.chanya na fanya.vile.vitu ambavyo.na wewe.pia.unapenda.

kufanyiwa hapo utaenda sawa tu na kama upo kwenye dini usisahau ibada japo.hapa kwenye dini napo.unatakiwa.uwe macho.sana.hasa kama.ni mkristo.....kama ni muislam huna shida sana maana dini inaendana na huo.mfumo.wa haki
 
Back
Top Bottom