Matokeo ya wananchi kujichukulia sheria mikononi inapokuja swala la vibaka..


paesulta

paesulta

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2009
Messages
227
Likes
7
Points
35
paesulta

paesulta

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2009
227 7 35
Vibaka Dar wafunga mitaa, wapora mali, jambazi lalipukiwa na bomu likipambana na polisi


Waandishi Wetu
WATU zaidi ya 50 waliodhaniwa kuwa vibaka juzi walifunga mitaa ya maeneo ya Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, kuvamia na kupora mali za wananchi,

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zinaeleza kuwa tukio la wahalifu hao kufunga mtaa na kufanya uporaji lilifanywa na vibaka hao baada ya mtu mmoja anayeaminika kuwa ni mhalifu mwenzao kuuawa na wananchi hao kwa tuhuma za uporaji.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema vibaka hao walifanya uovu huo eneo la Yombo Dovya CCM majira ya saa 12:00 jioni baada ya kumzika mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa na baadaye kuchomwa moto.

Fujo za vibaka hao na uporaji waliokuwa wakiufanya katika kila nyumba, ziliwalazimu wafanyabiashara wa maeneo hayo kufunga maduka yao kwa hofu ya kuporwa.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao walilazimika kujifungia ndani ya nyumba zao kujinusuru na vibaka hao, walisema watu hao walikuwa wakivamia kila mtu aliyekuwa mbele yao wakiwa na silaha mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mapanga na marungu.

Kwa mujibu wa mashuhuda......

"Hawa vibaka walienda kumzika mwenzao jana (juzi) na wakiwa wanarudi kila mmoja alishika silaha; panga, rungu, bisibisi na nyingine zenye ncha kali na kuanza kuwashambulia wananchi waliokutana nao njiani na kuwapora mali zao na wengine kuwavua hadi nguo," alisema shuhuda huyo.
Kutoka gazeti la mwananchi....


......sasa mwisho wake ni kama hivi,vibaka kuungana kulipa kisasi cha mwenzao alieuliwa kwa tuhuma za wizi.kitachofuata we unadhani ni nini kama sio kwa wananchi nao ku-react na si ndio machafuko yanavyoanzan hivi?
mi kila siku kwa kweli naangalia na naona tuendako siko,kwani wengi tunashabikia tu,oooh we hujaibiwa ndo maana unawaonea huruma hawa vibaka,swala si hilo wakuu,ila ni kuwa kunatuweka katika kujengeana chuki na tunajenga ukatili mioyoni mwetu,tumekuwa na mkono mwepesi mno kutoa uhai wa binadamu na hili si swala la kujivunia......

Ni mtazamo wangu tu.....
 

Forum statistics

Threads 1,250,868
Members 481,514
Posts 29,748,830