Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya wanafunzi wa darasa la vii waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mw

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by The Quonquerer, Dec 21, 2010.

 1. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Katika Mkoa wa Kagera wenye Halmashauri za Wilaya (8) jumla ya wanafunzi 49,804 waliandikishwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (Darasa la VII) mwaka 2010, kati ya hao walioandikishwa wanafunzi waliotahiniwa na kufanya mtihani wa darasa la saba ni 48,893 ambazo ni asilimia (98.2%) ya wanafunzi wote walioandikishwa kufanya mtihani mwaka 2010, wanafunzi 911 ambao ni asilimia (1.8%) hawakufanya mtihani wa darasa la saba
  Wanafunzi waliofaulu ni 29,385 asilimia (60.1%) kati ya wanafunzi 48,893 waliofanya mtihani. Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2011 ni 27,258 asilimia (92.8%) kati ya wanafunzi 29,385 waliofaulu, na wanafunzi 2,127 asilimia (7.2%) wamebaki kutoka idadi ya wanafunzi 29,385 waliofaulu mwaka huu 2010.
  Aidha kiwango cha ufaulu Mkoa wa Kagera kimepanda kwa asilimia (4.51%) ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana (2009) ambapo kiwango cha ufaulu kilikuwa ni asilimia (55.59%) lakini kwa mwaka huu (2010) kiwango cha ufaulu ni asilimia (60.10%).
  Halmashauri ya Wilaya ya Ngara imeendelea kuongoza Mkoa wa Kagera kwa asilimia (76.3%) na kushika nafasi ya Kwanza, Wilaya ya Biharamuro imeshika nafasi ya pili kwa asilimia (72.5%) kutoka nafasi ya nne iliyoshika mwaka jana 2009. Manispaa ya Bukoba imeshika nafasi ya tatu kwa asilimia (71.9%) na mwaka jana ilishika nafasi ya tatu. Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi imeporoka nafasi mbili kutoka nafasi ya pili iliyoshika mwaka jana (2009) na kushika nafasi ya nne kwa asilimia (65.0%).
  Halmashauri za Wilaya nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyopanda nafasi moja tokay a mwaka jana (2009) na kushika nafasi ya tano kwa asilimia (61.5%). Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeshuka nafasi moja kutoka nafasi ya tano (2009) na kushika nafasi ya sita kwa asilimia (56.4%). Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imeendelea kushika nafasi ya pili kutoka mwisho kama mwaka 2009, lakini mwaka huu 2010 kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia (4.35%), kutoka aslilimia (50.55%) za mwaka 2009 mpaka asilimia (54.9%). Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imeendelea kushika nafasi ya Mwisho Kimkoa japo kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka aslimia (33.99%) za mwaka 2009 mpaka aslimia (50.4%).
  H/WILAYA

  MWAKA 2010
  NAFASIMWAKA2009

  NAFASI

  NGARA
  76.3%

  1
  73.04%
  1​

  BIHARAMULO
  72.5%

  2
  63.45%
  4​

  BUKOBA MANISPAA
  71.9%

  3
  66.27%
  3​

  MISSENYI
  65.0%

  4
  67.90%
  2​

  CHATO
  61.5%

  5
  55.65%
  6​

  MULEBA
  56.4%

  6
  58.24%
  5​

  KARAGWE
  54.9%

  7
  50.55%
  7​

  BUKOBA VIJIJINI
  50.4%

  8
  33.99%
  8​
  JEDWALI HAPA JUU NI VIWANGO VYA KUFAULU KIWILAYA[​IMG]Picha ya Afisa Elimu Mkoa Kagera Bw. Florian Kimolo
  Aidha kiwango wanafunzi waliofaulu walichaguliwa kwa kiwango cha alama ya juu ambayo ni 230 kw awavulana na wasichana alama 228, lakini kiwango cha alama ya mwisho kuchagua ni alama 100 kwa wasichana na wavulana kwa mwaka 2010.
  Shule ilyoishika nafasi ya kwanza Kimkoa ni Shule ya Msingi Kaizilege kutoka Manispaa ya Bukoba . Mwanafunzi aliyeongoza Kimkoa, Kiwilaya na Kishule ni Ligobert Linus Kutoka Shule ya St. Peter Claver iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe . Aidha, Machumi John Nyarukubara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ameshika nafasi ya mwisho kwa kupata alama 6 tu kati ya shule 967 zilizofanya mtihani.
  Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera akielezea sababu za Halmashauri ya Wilaya za Bukoba na Karagwe kendelea kushika nafasi mbili za mwisho alisema pamoja na sababu nyingine maandalizi hafifu kwa baadhi ya shule, hali mbovu ya miundombinu, upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia na baadhi ya walimu kutomudu kufundisha masomo ya Hisabati na Kiingereza na hivyo kusababisha wanafunzi wengi kushindwa masomo hayo.
   
 2. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je naweza kupata matokeo hayo kwa ukamilifu, majina ya shule na wanafunzi nchi nzima ? Kuna mtu amewahi kuyasoma mahala ?
   
 3. j

  jafora New Member

  #3
  Dec 31, 2013
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli ni jambo la kushangaza sana kutangaza idadi ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ilhali majina yenyewe na shule wandazo kutofahamika,wuika wangejipanga wakamilishe yote
   
 4. K

  KENET JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2015
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 259
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  .Serikali inachofanya siku hizi inaangalia shule zile za Private ambazo wanafunzi wamefaulu vizuri na wana GRADE A wanawapangia kwenye shule mojawapo ya kata darasa Zima kwa makusudi kabisa wakijua wazi kabisa kwamba hawa hawatakwenda au wazazi wao hawatakubali mtoto mwenye A masomo yote akasome pale kwa hiyo nafasi zinabaki nyingi wanapeleka hao ambao wametangaza kuwa wamefaulu bila ya kuwapangia shule. Je hii ni halali?
   
Loading...