MATOKEO Ya Vyuo yametoka

Status
Not open for further replies.

Mwandishi

Member
Jul 19, 2008
5
0
Habari za Mchana.

Habari nilizozipata Asubuhi hii ni kwamba Matokeo ya Wanafunzi waliochaguliwa Vyuo Mbali mbali yametolewa.UDSM,MZUMBE,Zanzibar State University,SUA,TUDARCO,AU,UDOM,ST. Augustine,MUCCOBS,MWUCE,DUCE,IUCO,SUZA,RUCO,MUHAS(Muhimbili),MMU,TEKU,ZU,WBUCHS,SMMUCO,St Johns,Open University,SEKUKO,RUSSIA,MUCO
na vyuo na taasisi zote za vyuo vikuu kama Chuo cha Ustawi

Kujua Umechaguliwa Chuo gani tuma sms

Apply[space]index number kwenda 15522.

index number zinatomika ni yoyote ya O level au High Level

mfano Apply 1234 na utume kwenda namba 15522.
Ni hayo tu asubuhi hii..
 
Asante Mkuu wetu yalitoka tangu juzi.mimi nimesikia tangu juzi.ilay ahivyo vyuo vingine kuna doubts ya UDSM tangu juzi.
 
Asante Mkuu wetu yalitoka tangu juzi.mimi nimesikia tangu juzi.

Ila TUME ya vyuo imeweka Huduma hii ili watu wayapate kwa urahisi,sababu wanafunzi walioomba ni wengi na wanatoka sehemu mbali mbali za Tanzania ambk hata Magazeti hayafiki,na njia ya SMS ni rahisi kuwafikia watu wengi..
 
Mkuu usitake kuongopea watu hapa JF. Hiyo habari kwamba tume ya vyuo imeweka huduma hii wakati tunajua ni biashara ya mtoto wa mama six na mtoto wa Dialo si sahihi kabisa. Wewe endelea kutangaza biashara. SMS moja ni bei gani vile?
 
hiyo siyo Biashara ya mtoto wa mama Sita wala Diallo,Application imetengenezwa na vijana wadogo tu ambao wamemaliza chuo pale UDSM mwaka huu..Bei ni TSH 250

Nyambala,
vijana hawa wameamua kujikomboa na wamejitolea kusaidia watanzania kuwapa huduma zilizo bora na za bei nafuu
 
hiyo siyo Biashara ya mtoto wa mama Sita wala Diallo,..Bei ni TSH 250

Mkuu inaonyesha umeshaanza kufikiria negative tayari na hivyo unanitisha. Hiyo biashara tunaifahamu vizuri sana na ilianzishwa wakati mama six akiwa waziri wa elimu. Lengo ikiwa ni Dogo yule Benja kumuinfluence mama yake matokeo ya shule yakitoka wanapata wao kwanza yakiwa hot na yanminywa say for a day or two bila kutolewa in public then biashara inafanyika.

Kiujumla ni wazo zuri na ujasiriamali regardless ni ya wakina nani wanaifanya. Il mradi tu kusiwe na elements za nia ovu ndani yake.

Nachopingana na wewe ni hili lakusema eti tume ya vyuo imeamua kurahisisha kufikisha information. Hii ni uongo na kama kuna mtu amekutuma basi inatakiwa akulipe maana hii ni biashara si free service period.
 
Kiujumla ni wazo zuri na ujasiriamali regardless ni ya wakina nani wanaifanya. Il mradi tu kusiwe na elements za nia ovu ndani yake.
hii imetulia..ila siyo kwamba kila jambo wanajua wao,mie hata huyo mtoto wa sitta simfahamu.Nilitegema ungeniomba tutorials nikupe ili nawewe ujifunze kucheza na python.
 
Mkuu usitake kuongopea watu hapa JF. Hiyo habari kwamba tume ya vyuo imeweka huduma hii wakati tunajua ni biashara ya mtoto wa mama six na mtoto wa Dialo si sahihi kabisa. Wewe endelea kutangaza biashara. SMS moja ni bei gani vile?
Sasa Mkuu mbona unakuwa kama enzi zile za zama za mawe za kale......hata kama ni biashara ya mtoto wa nani vile....lakini ni huduma safi...
 
Wana jambo forum naomba mnisaidie kuna matokeo ya somo la STATISTICS kwa vijana wa UD wanaotarajia kujiunga mwaka wa pili hayakuonekana na wao walifanya hilo somo.Naomba huyo mhadhiri ashughulikie hili suala mapema maana adhabu yake ni kwa hawa vijana kutoendelea na masomo.
 
wanafunzi wa mwaka wa pili wa kozi gani?niandikie kwenye PM nitalishughulikia,ila siyo possible kupotea labda kama kuna ishu nyingine
 
Habari za Mchana.

Habari nilizozipata Asubuhi hii ni kwamba Matokeo ya Wanafunzi waliochaguliwa Vyuo Mbali mbali yametolewa.UDSM,MZUMBE,Zanzibar State University,SUA,TUDARCO,AU,UDOM,ST. Augustine,MUCCOBS,MWUCE,DUCE,IUCO,SUZA,RUCO,MUHAS(Muhimbili),MMU,TEKU,ZU,WBUCHS,SMMUCO,St Johns,Open University,SEKUKO,RUSSIA,MUCO
na vyuo na taasisi zote za vyuo vikuu kama Chuo cha Ustawi

Kujua Umechaguliwa Chuo gani tuma sms

Apply[space]index number kwenda 15522.

index number zinatomika ni yoyote ya O level au High Level

mfano Apply 1234 na utume kwenda namba 15522.
Ni hayo tu asubuhi hii..

Mkuu Mwandishi,

IFM iko chini ya TCU?
 
Mkuu usitake kuongopea watu hapa JF. Hiyo habari kwamba tume ya vyuo imeweka huduma hii wakati tunajua ni biashara ya mtoto wa mama six na mtoto wa Dialo si sahihi kabisa. Wewe endelea kutangaza biashara. SMS moja ni bei gani vile?

Kama ni biashara, wapo smart kuanzisha na kufanikisha. Uhuru wa competition kuianzisha ni kwa yeyote.
 
Tunashukuru sana kwa habari nyeti kama hii. Hata hivyo inaonekana kwenye sites za vyuo husika matokeo hayo hayapatikani. Angalia AU hakuna kitu na habari zinazozungumzwa AU hazikidhi haja, maana hakuna updates. Naomba msaada.
 
UDSM yapo kwenye website yao au fungua attachment hapa chini
 
Attachments

  • UDSM admission.pdf
    355.1 KB · Views: 635
mbona hayo matokeo hatuyaoni nielekeze na hiyo sehemu ya index no na jina mbona haipo?
 
Duh kwa nini wasiweke kwenye mitandao utume sms utozwe 250 upate matokeo yako duh hii kali. Huu mradi wa watu wachache kama kawaida yao fikiria 250x600000=150,000,000/= wajanja wanaramba mkwanja huo.
 
mbona hayo matokeo hatuyaoni nielekeze na hiyo sehemu ya index no na jina mbona haipo?

Pole Suzan hii ni thread ya mwaka jana kwa hiyo hii taarifa si sahihi kwa tarehe ya leo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom