Matokeo ya VPL: Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

Sijawahi kuna pamoja na ukubwa wa team kama Barca, Real, Man, Liver sijui city na wengine wengi wakaenda ugenini kucheza halafu watu waka support team ya wageni. Wenzetu mapenzi wanayo na team kubwa lakini full support team zao za nyumbani. Kwa hili tutabaki kuwa watumwa wa team hizi mbili. Kidogo miaka ile ya Pamba, CDA, Reli sijui Tukuyu hata RTC Kigoma team zilikuwa zinapendwa kwao. Penda Simba na Yanga sababu ya ukongwe ila wakija nyumbani kwenu shangilia team ya nyumbani nchi zote ndio utamaduni. Najuwa nitatukanwa humu ila ndio ukweli
Watanzania hawapendi mchezo wa mpira bali wanapenda timu. Ndio maana hata uwanja ulikuwa haujai kwenye Simba Cup.
 
90+3'

Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa VPL, uwanja wa Jamhuri Dodoma

Hoza anapiga mbele, mabeki wa Simba wanazuia mpira unatoka nje, wanarusha kuleee, ni faulo kuelekea Simba

Dodoma wanapata Free Kick, inapigwaaaa, Manula anachumpa na anadaka bila wasiwasi, ilikuwa hatari lango la Simba, dah almanusura wasawazishe...

Naaaam mpira umekwishaaaa ambapo Simba wameibuka na ushindi mabao mawili kwa moja, mabao ya Kagere, Morrisoon na huku Mkandala akifunga upande wa Dodoma Jiji FC

VPL' FT: Dodoma Jiji FC 1-2 Simba SC

Ghazwat
 
Back
Top Bottom