Matokeo ya VPL: Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL kuendelea kutimua vumbi leo January 4, 2021kwa mechi mbili kupigwa, ambapo Dodoma Jiji FC wanakabiliana na Mnyama Mkali Simba SC, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku KMC wakicheza na Namungo FC kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Mechi hizi ni za viporo na ni mwanzo wa kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania VPL, baada ya kusimama kupisha michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN ambapo bado inaendelea nchini Cameroon.

Mchezo wa Dodoma Jiji FC na Simba SC unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizongatia ni mara ya kwanza kukutana kwenye VPL.

Kocha wa Simba SC Didier Gomes ambaye atakongoza jahazi kwanza mara ya kwenye VPL, amesema " Utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kupambana ni muhimu sana, tuna michezo mitatu mkononi tunatakiwa kushinda" amesema Gomes.

Kwa upande wa Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makatta amesema " Ni mechi muhimu kushinda kutokana na kuwa sehemu ambayo si rafiki kwenye msimamo wa VPL, lakini wapo tayari kuwakabili Simba SC na hata wachezaji wanalijua hilo.

Yote ni ndani ya dakika 90 za mchezo. Kumbuka mitanange hii ni kuanzia saa 10: 00 jioni Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

Screenshot_20210204-153944.jpg
Screenshot_20210204-154007.jpg


Update;

===========================

Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Simba ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa mshambuaji Maddie Kagere na Bernard Morrison akifunga bao la pili huku Mkandala akifunga bao moja upande wa Dodoma Jiji FC

FT, VPL; Dodoma Jiji FC 1-2 Simba SC
 
09' Dodoma Jiji wanashambulia lango la Simba, anapiga shutiiiiii lakini Manula anadaka bila wasiwasi

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC
 
15' Free Kick kuelekea Dodoma FC, eneo bomba kuweza kupata bao

Inapigwaaaa Wawaa, anakosa
 
21' Miquissone anapigaaaa loooooo, anababatiza ukuta wa Dodoma na kuwa kona
 
Daaaah Morrisoon weeee, namna gani hapa unapoteza nafasi ya kufunga
 
Back
Top Bottom