Matokeo ya utumbuaji majipu: Serikali kulemewa na uchunguzi usioisha

Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,836
1,382
Habari zenu wana JF,

Baada ya salaam, ningependa kutoa yangu ya moyoni hususani kuhusu kile kinachoitwa " utumbuaji majipu" unaoendelea kufanyika chini ya serikali ya awamu ya tano. Kinachonishangaza katika utumbuaji huu, hatuoni hatma ya wale waliotumbuliwa awali. Kwa mafano ;

1. TRA-Mkurugenzi mkuu alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi-Hatujapata hatma yake, uchunguzi unaendelea.

2. Bandari-Bodi ilivunjwa na menejimenti inaendelea kuchunguzwa.

3. Muhimbili, kuhusu mashine za MRI na TSCAN ambako Mkurugenzi mkuu aliondolewa na kupelekwa wizarani kupangiwa kazi nyingine-Je tatizo limeisha?

4. DART-Mkurugenzi alisimamishwa na uchunguzi unaendelea, sakata la UDA bado kizungumkuti.

5. Uhamiaji nako hawakubaki nyuma, Kamishna Mkuu na mkuu wa fedha na utawala wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

6. Baadhi ya mawaziri pia wametanganza uchunguzi; Mwiguru ametangaza kufanya uchunguzi maeneo yafuatayo;

kampuni ya NARCO inayosimamia Ranchi za taifa-Meneja Mkuu alisimamishwa kupisha uchunguzi na bodi kuvunjwa. Pia Mwiguru alitoa amri ya saa 48 kuhakikisha wanunuzi waliokopa mazao kwa wakulima wanalipa mara moja-bado hatujapata mrejesho kama malipo yamefanyika au uchunguzi unaendelea.


7. Afya hawakubaki nyuma, Dr. Kigwangwala akafanya ziara ya kushtuka kwa anayejiita Dr. Mwaka- matokeo ya ziara hiyo bado kwani nadhani huyo jamaa bado anajiita doctor na anachapa mzigo kama kawa.

8. Wizara ya Ardhi pamoja na ile inayosimamia Mazingira- bomoa bomoa inayoendelea nini hatma yake?

Swali: Ni taasisi gani inayoratibu chunguzi hizi zote kwa pamoja ili kujiridhisha kuwa haki imetendeka kwa watuhumiwa? na Je? endapo ikionekana sehemu kubwa ya watumishi hawa wa umma waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi wakaonekana hawana hatia na pengine kurejeshwa kazini na fidia juu, hatua gani zitachukuliwa kwa waliowasingizia na kuisababishia serikali hasara? Na kwa nini serikali isiweke utaratibu wa kupata mrejesho wa majipu ya awali kabla ya kuendelea kutumbua mengine?


Naomba tutafakari hayo kwa leo na tuishauri vema serikali yetu.
 
Kila taasisi ina vyombo vyake, inaweza kuitwa kamati au idara.
Madai ya walimu yatachunguzwa na watu wa elimu, kilimo na watu wao na pale kwenye jinai ndio kuna polisi, kwenye rushwa takukuru.
 
Kila taasisi ina vyombo vyake, inaweza kuitwa kamati au idara.
Madai ya walimu yatachunguzwa na watu wa elimu, kilimo na watu wao na pale kwenye jinai ndio kuna polisi, kwenye rushwa takukuru.

Issue inakuwa ngumu zaidi pale kila uchunguzi unahusisha jinai. Hivyo polisi na hao TAKUKURU sijui watajigawa vipi
 
Kila taasisi ina vyombo vyake, inaweza kuitwa kamati au idara.
Madai ya walimu yatachunguzwa na watu wa elimu, kilimo na watu wao na pale kwenye jinai ndio kuna polisi, kwenye rushwa takukuru.

Issue inakuwa ngumu zaidi pale kila uchunguzi unahusisha jinai. Hivyo polisi na hao TAKUKURU sijui watajigawa vipi
 
Yaani ninachokiona mpaka sasa ni kujengana hofu tu. Wananchi wamebaki wanashangilia majibu kutumbuliwa, lakini sisi tunaoangalia mambo kwa kina hatuoni jambo muhimu kwa uchumi. Tulitarajia kuona shida ya umeme inapatiwa ufumbuzi, wangalau basi hata majibu ya uhakika wa huu mgao wa ajabuajabu. Mafuta yameshuka bei kwa kiwango cha juu kwenye soko la dunia, lakini hapa punguzo hata ni vichekesho.

Utetezi eti ana siku chache madarakani. Sasa kama ana siku chache sifa zote za nini? Ukiachia hofu anayowapa watumishi wa umma, dalili zinaonyesha atafanya madudu sana kwenye uchumi.
 
Back
Top Bottom