Matokeo ya Utafiti wa matumizi ya Juisi Ya Miwa Waibua Hofu Kubwa Jijini Mwanza

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Wadau wa JF

Taarifa Kutokea Jijini Mwanza Tanzania kuhusu matumizi ya Juisi Ya miwa

Vimelea vinavyopatikana kwenye kinyesi vyakutikana

Utafiti wa awali uliofanywa na Wataalamu Watafiti kuhusu matumizi ya Juisi ya Miwa umeibua hofu na sintofahamu kubwa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake na mikoa ya jirani.

Matokeo ya awali ya utafiti huo yanatoa athari hasi kwa Watumiaji wake kutokana na sababu mbalimbali zilizoainishwa

Taarifa zaidi ya utafiti huo wa kina zinapatikana katika Gazeti la Mwananchi

MCL
 
Dah nilistuka sana kuona matokeo ya ule utafiti. Inabidi watengeneze juice za miwa wabadilike aisee.
 
Wewe endelea kugonga juice hizo kwani watu kunywa juice ya miwa wameanza leo? Achana na watafiti wangese
Naweka akiba ya maneno...

Tunakoelekea mpaka mpunga utakuwa ni sumu! Og..yoyote..

Tuanze kuzoea vya kutoka nje ndio

Vizima
 
mimi sio mtaalamu sana kufafanua hiyo tafiti ya huko mwanza, ila walichukua sampuli ya juisi ya miwa kutokea sehemu mbalimbali wanapouza na wakakuta asilimia kubwa ya sampuli za juice ina vimelea (sijui kitaalamu huitwa ni vimelea au vijidudu) ambavyo hupatikana kwenye kinyesi, na hivyo kutoa picha jinsi ya hali ya usafi katika sehemu za kutengenezea juisi hiyo.

Nafikiri huu utafiti ukiletwa Dar ingependeza zaidi maana huku hunywewa sana.
 
Kwa hiyo hao wa mikoani wanatoka kukata gogo bila kunawa wanakuja kukamua miwa?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom