Matokeo ya Utafiti: Kikwete, Freeman Mbowe, Zitto, Killango, Jerry Silaa na Dr Slaa

kuongea kwa sauti kubwa au kwa uchungu sio tija!

hilo nimelipenda; ndio maana watu wengine wanasema Chadema au viongozi wake wamefanya mengi kwa sababu wanaongea kwa sauti kubwa na uchungu! the same can be said with some members ndani ya CCM..
 
..hii nchi imekuwa neglected and abused kwa muda mrefu sana na matokeo yake ndiyo hayo mnayoyaona sasa hivi. kwa mfano: elimu imetelekezwa kwa muda mrefu kiasi kwamba leo hii ukijenga madarasa na usiyapatie waalimu na vifaa wananchi wanaridhika na kuwapeleka watoto wao huko.

..ole wao CCM wananchi wakijua maana halisi ya maendeleo na jinsi ya kudadisi na kupima utendaji wa viongozi na serikali.

Umekosea inatakiwa isomeke hivi 'huko huko' LOL

Pamoja na uelewa wangu katika michakato ya kuandaa tafiti (sampling procedures). Hiyo yenye nyekundu hapo juu inanifanya niupasishe huu utafiti kwa 90% lakini chini ya sifuri.

90% divide 0 = infinity, katika real life we sema zero tu

hilo nimelipenda; ndio maana watu wengine wanasema Chadema au viongozi wake wamefanya mengi kwa sababu wanaongea kwa sauti kubwa na uchungu! the same can be said with some members ndani ya CCM..

That is our country , ukiona umekosea kitu, we nenda bungeni katoe chozi, ! hawana hiyana! EL alisahau hii technique angelia bungeni ,masafi ya mtume, leo hii angekuwa madarakani!

We need tangible and undisputable proofs kwa kila kiongozi anayesema ameleta maendeleo!

Zito anaongoza kigoma, mnawauliza watu DSM kuwa kama ni mbunge mzuri, watu wanajibu bila hiyana! hii aibu, aliyeturoga huyu sijui alienda wapi kuturogea bara la antactica?
 
Tuseme ni kweli!

Wali interview watu wangapi na kutoka maeneo gani? ya nchi

Katika hao wana ccm ni wangapi na wasio wanaccm ni wangapi?

Wanaume wangapi na wanawake wangapi pia vijana wangapi wazee wangapi

walitumia njia zipi kuwapata hao wananchi? je ni wafanyakazi au wakulima?

Blah Blah tu hizo
 
Leo synovate wamekutana na wanahabari na kutangaza matokeo ya utafiti wao kuhusu hali ya taifa. Wametaja kuwa Kikwete anaongoza kwa kuwa na asilimia 70 akifutiwa na Freeman Mbowe mwenye asilimia 10, akiwa ametangulia kidogo Lipumba. Hii ni katika nafasi ya urais.

Katika bunge utafiti wao unaonyesha kwamba Zitto Kabwe ndiye mbunge bora kuliko wote akifuatiwa na Anna Kilango. Katika matokeo hayo Mbunge mwingine bora anayetajwa ni Jerry Silaa ambaye ni diwani wa ukonga. Utafiti huo unasema kwamba wananchi wapatao elfu mbili waliohojiwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamemtaja diwani huyo kuwa anachapa kazi kwa kiwango kikubwa na wakiamini kwamba ni mbunge. Katika utafiti huo Dr Slaa anatajwa kuwa nyuma.

Kwa upande wa vyama matokeo yanaonyesha kwamba CCM iko karibu zaidi na wananchi kwa asilimia 70 ikifuatiwa na CHADEMA yenye asilimia 14.

......ndiyohiyo
Napata kigugumizi kuamini utafiti huu kama si hoax ama la ina maana hayo maeneo mbalimbali ya nchi wanamjua huyo mbunge Jerry Muro/Silaa kwa kiasi gani hivi watu wa Kasulu Kigoma watu wa Mtwara watu wa Loliondo Magu Pemba Itigi Singida Mbeya wameulizwa angalau kumtambua huyo Diwani wa Ukonga achilia mbali kujua kazi gani huwa anafanya labda watuambie hizo sehemu mbalimbali walikuwa na maana ya maeneo yote ya Ukonga ndiyo maana kuna watoahoja humu wamesema utafiti umefanyika leo wakati wa chai ya saa nne pale Lumumba
 
usikute ni deal la huyo diwani kutaka ubunge nji hii utaiweza?
 
Tuna miezi kama tisa tu, tutajua kama hayo yana ukweli au la.

Ila kwa maoni yangu, mwaka jana nilikuwa na imani kwamba CHADEMA wangekiweza hata kupata zaidi ya 40% ya viti vya ubunge. Lakini tokea waamue kuzembea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kutumia mbinu kumzuia Zitto asigombee uwenyekiti wa chama. Ushindi kwa CCM mwezi wa kumi ni wa kishindo.

Hakuna la maana walilofanya CCM au huyo Kikwete wao lakini pia upinzani na hasa CHADEMA wamejiangusha mno kwa kuua changamoto mpya ambayo Dr. Slaa na Zitto waliileta kwenye chama chao.

Naionenea huruma Tanzania yetu maana CCM wakishinda tena kwa asilimia zaidi ya 60, nchi yetu itakuwa imekwisha.

Tusipoteze muda kulalamikia utafiti, tujisogeze vijijini kwenda kuwaandaa wananchi. Hata mwaka 2005 waltu tulilamika hivyo hivyo, matokeo yake JK akapata kura nyingi kuliko hata utafiti walivyosema.
 
Kura zakifisad matoke yakifisadi. Inaönyesha yote ni propaganda. Tumewashi2kia wana ccm.
 
Tatizo letu wana-JF ni wepesi wa kulaumu pasipo kuchukua hatua mbadala.Badala ya kuilaumu Synovate ingekuwa vema kufanyika alternative opinion poll itakayoangalia maeneo kama masuala ya ufisadi,kulindana,kutotimiza ahadi,kukumbatia rushwa,nk.Hawa Synovate wana rekodi nzuri tu ya kujipendekeza kwa Kikwete.Next tutaskia opinion poll kutoka REDET kwa yule mchemkaji anayeshika nafasi ya Prof Mkandara.Then,kama kawaida yetu tutaishia kulaumu tena.Let's not forget,kuna Watanzania wenzetu wanaamini kabisa hizi opinion polls za kibabaishaji.Na come October,CCM watakuwa na data za kusapoti "kukubalika" kwao,na hapo itakuwa too late kuendelea kulalamika.
 
Katika matokeo hayo Mbunge mwingine bora anayetajwa ni Jerry Silaa ambaye ni diwani wa ukonga. Utafiti huo unasema kwamba wananchi wapatao elfu mbili waliohojiwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamemtaja diwani huyo kuwa anachapa kazi kwa kiwango kikubwa na wakiamini kwamba ni mbunge.
Kama wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wameweza kumfahamu diwani wa Ukonga basi watanzania wana uelewa mkubwa na habari zinafika kiurahisi vijiji vyote. Kama kuna wananchi hawajui Pinda ni nani iweje diwani Jerry Silaa afahamike nchi nzima? Haiingii akilini hata kidogo!
 
Leo synovate wamekutana na wanahabari na kutangaza matokeo ya utafiti wao kuhusu hali ya taifa. Wametaja kuwa Kikwete anaongoza kwa kuwa na asilimia 70 akifutiwa na Freeman Mbowe mwenye asilimia 10, akiwa ametangulia kidogo Lipumba. Hii ni katika nafasi ya urais.

Katika bunge utafiti wao unaonyesha kwamba Zitto Kabwe ndiye mbunge bora kuliko wote akifuatiwa na Anna Kilango. Katika matokeo hayo Mbunge mwingine bora anayetajwa ni Jerry Silaa ambaye ni diwani wa ukonga. Utafiti huo unasema kwamba wananchi wapatao elfu mbili waliohojiwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamemtaja diwani huyo kuwa anachapa kazi kwa kiwango kikubwa na wakiamini kwamba ni mbunge. Katika utafiti huo Dr Slaa anatajwa kuwa nyuma.

Kwa upande wa vyama matokeo yanaonyesha kwamba CCM iko karibu zaidi na wananchi kwa asilimia 70 ikifuatiwa na CHADEMA yenye asilimia 14.

......ndiyohiyo

Synovate ndiyo mdudu gani? REDET? Ka watanzania wanajua kudandia, Baada ya utafiti wa kupika wa REDET uliompendelea JK hadi Mkandala kuteuliwa VC wa UDSM, nao Synovate wanafuata nyao wakumbukwe.

Hivi synovate wanafadhiliwa na nani? Akina nani kwa majina wanaunda Synovate. Historia yao ikoje? Ni wanachama wa chama gani? Hapa Tz taasisi za kiraia zinazoheshimika kwa utafiti ni ESRF na REPOA, wengine wanaganga njaa tu.

Hitimisho: Synovate wafanye utafiti wao huo hapa JF.
 
Ni research (utafiti)? au ni opinion poll(s)? Ngoja tusubiri REDET watakuja na madudu yepi.
 
I have no comment as sample yenyewe ni sample selection bias (kwani ukawachukua wanaccm 10, chadema 1, cuf 1 halafu ukadai CCM inapendwa asilimia 83) just kufurahisha waheshimiwa. Nilipoisoma kichwa cha habari nikawa na shauku kujua sample size ni ngapi nilipoona hakuna na habari yenyewe nikapatwa na mshangao mkuuubwaa!!!!
 
(Habari Leo)
RAIS Jakaya Kikwete amepewa nafasi kubwa ya kushinda Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu kwa kuwa wananchi wanampa nafasi kubwa ya kuwashinda wapinzani wake watakaojitokeza kuwania kwenda Ikulu.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya Synovate umebainisha kuwa, utendaji wa Kikwete unawaridhisha wananchi kwa asilimia 75.

Wananchi pia wamesema, chama cha siasa ambacho kipo karibu zaidi na wananchi ni Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Kwa mujibu wa wananchi hao, CCM ipo karibu na wananchi kwa asilimia 70, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa asilimia 17, Chama Cha Wananchi(CUF) kwa asilimia 9, NCCR Mageuzi kwa asilimia 2,Tanzania Labour(TLP) na UDP asilimia 1.

Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti ya kura ya maoni ya robo ya mwisho Oktoba- Desemba mwaka jana iliyofanywa na kampuni hiyo, lengo lilikuwa ni kupata kura ya maoni ya watanzania katika mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika vipindi tofauti ndani ya mwaka.

Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma wa kampuni hiyo, Abdallah Gunda, amewaeleza waandishi wa habari kuwa, kampuni hiyo ambayo zamani ilijulikana kwa jina la Steadman Group ilikusanya maoni kwa kuwahoji watu 2000.

Amesema, watu hao waligawanywa sawasawa na uwiano wa idadi ya wananchi wa Tanzania na ilikusanya mahojiano ya uso kwa uso katika maeneo tofauti yaliyochaguliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,watu hao walipoulizwa ni Rais yupi wangependa awe kwa mwaka 2010, walimchagua Kikwete kwa asilimia 75.

Kikwete alifuatiwa na Freeman Mbowe kwa asilimia 10, Profesa Ibrahim Lipumba alipata kura kwa asilimia 9, John Cheyo, Salim Ahmed Salim na Zitto Kabwe ambao walipata asilimia 1.

Mbunge aliyefanya vema kwa kipindi hicho cha mwisho wa mwaka 2009 ni Zitto Kabwe kwa asilimia 31, Anne Kilango Malecela asilimia 13, Dr. Wilbroad Slaa asilimia 7, Dr. Harrison Mwakyembe asilimia 6, John Magufuli asilimia 3, Lawrence Masha asilimia 2.

Wabunge wengine ni Mizengo Pinda, Mohamed Dewji, Lucas Selelii, Samuel Sitta, John Cheyo, John Nchimbi, Halima Mdee, Jenista Mhagama, Philemon Ndesamburo, Hamad Rashid Mohamed, David Mathayo, Mark Mwandosya na Hamis Kagasheki ambao wote wamepata kura za maoni kwa asilimia 1.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,zaidi ya robo tatu ya watanzania wanaamini kwamba Tanzania ni nchi yenye demokrasia, asilimia 57 kati yao wanaamini kwamba yapo matatizo madogo madogo.

Asilimia 21 ya waliohojiwa wamesema, Tanzania ipo demokrasia kamili, demokrasia yenye matatizo makubwa asilimia 15 wakati asilimia 3 ya wananchi walidai kwamba nchi haina demokrasia.

Wananchi walipoulizwa endapo uchaguzi ungeitishwa kesho ni wangapi wangepiga kura asilimia 94 walidai wangepiga kura, na asilimia 5 walisema wasingepiga kura.

Asilimia 69 walidai wamechoshwa na siasa, asilimia 9 walisema hawajajiandikisha, asilimia 7 ya wananchi walisema wagombea hawawasaidii.

Gunda amesema, katika utafiti huo walipita mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mbeya,Kagera, Dar es Salaam, Kigoma, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Tabora, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Mtwara, Mara, Singida, Rukwa, Manyara, Ruvuma, Pwani, Lindi na Pemba.

Aidha alisema kuwa waliwahoji wanaume kwa asilimia 54 na wanawake asilimia 46,waliwagawa katika matabaka manne kuanzia umri wa mika 18-27 asilimia 39 walihojiwa, 28-37 asilimia 32, 38-47 asilimia 16 na miaka 48 na kuendelea walihojiwa asilimia 14.

Pia alisema kuwa watu 100 walishiriki kufanya mahojiano na kwamba,walikuwa wamepatiwa mafunz
 
Yatakuja mengi ya kumsafisha Kikwete.
Inawezekana mmesahau kuwa Kikwete ni bingwa wa kutengeneza image yake mbele ya umma. 2005 alijjitengenezea image ya nabii sijui leo anakuja na image gani?
 
Je sample size yake ni ngapi total. Tukija katika kuchambua data waliyofanyia utafiti ni wangapi walikuwa ni wanachama wa CCM, CUF Chadema na wengineo??? Unaweza kuchukua watu 10 Arusha, Mwanza, Zanzibar na kwengineko lakini 80 of watu hao ni wanaCCM, 2% CUF, 14%Chadema na iliyobakia wengineo.

Pia authenticity ya maswali yakoje. Mfano kisomi kuna kinaitwa rings questions mfano Je JK ni rais mzuri kuliko wote??? Hili ni swali ambalo mtu utakayemuulize obvious atajua unataka support kwa kikwete. An unbiase question ni mfano tupe mafanikio ya kikwete au je rais kikwete unamrate vipi kiutendaji??? Hapo ndio jibu utalipata la kweli.

Ndio maana nakaa kimya maana nikianza kuichambua hii study mtakuja kuona upuuzi bure wacha nijikalie kimya ila bado nina mshangao mkubwaaa!!!1
 
Huu utafiti upo so bias,ili tuamini kwamba research yao ilikidhi viwango watuletee pia research instuments walizotumia kama ni questinnairs au interview guide,hii itatusaidia kujua mengi,lakini kwangu mimi hii ni muendelezo wa propaganda ambazo zilizinduliwa rasmi na Shehe Yahaya Hussen,..hebu fikiria kuna mahali pengine nimesoma nafikiri kwa michuzi kama sikosei,eti asilimia 1%ya waliohojiwa wanasema Zitto Kabwe,Salim Ahmed Salim na Mtikila wanafaa kuwa Marais kwenye uchaguzi ujao,..sasa hii kama sio research feki ni nini,katiba imeweka wazi kabisa ,kwamba ili uwe rais wa nchi hii sharti uwe na umri usiopungua miaka 40,sasa Zito kafikisha miaka 40 lini ili kumuweka kwenye huo utafiti wa nafasi ya raisi,halafu huyo sijui Jerr Slaa,who knows him,bora hata wangesema Adam Kimbisa tungewaelewa maana watu wengi wanamfahamu.
 
Silaumu waliokusanya statistics,.. nalaumu uelewa wa waTanzania... kweli Anna Kilango ndio mbunge effective kuliko wote CCM... nina hakika hata ukimuuliza Sitta na Wabunge wengine watakwambia hapana... kuongea kwa sauti kubwa au kwa uchungu sio tija!

Kuna jamaa yangu mmoja pale Mwanza, ukiongea saaaana huwa anamalizia......"PATACHIMBIKA HAPA".
 
Yatakuja mengi ya kumsafisha Kikwete.
Inawezekana mmesahau kuwa Kikwete ni bingwa wa kutengeneza image yake mbele ya umma. 2005 alijjitengenezea image ya nabii sijui leo anakuja na image gani?

RA na Salva je mmeanza ya 2005,mbona safari hii mapema mno?
 
Back
Top Bottom