Matokeo ya Utafiti: Kikwete, Freeman Mbowe, Zitto, Killango, Jerry Silaa na Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya Utafiti: Kikwete, Freeman Mbowe, Zitto, Killango, Jerry Silaa na Dr Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachero, Feb 22, 2010.

 1. K

  Kachero JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Tiganya Vincent-MAELEZO
  Asilimia 75 ya watanzania waliohojiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na utafiti wa masuala ya siasa, uchumi na kijamii wameonyesha kuwa wangependa Rais Jakaya Mrisho Kikwete andelelee kuongoza Tanzania mara baada ya uchaguzi Mkuu mwisho mwa mwaka huu.
  Hatua hiyo inafuatia watanzania 2000 waliohojiwa kutoka sehemu mbalimbali kumkubali kuwa Rais Kikwete anastahili kuchaguliwa tena kuwa Kiongozi Mkuu wa Tanzania.
  Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda alipokuwa anatoa matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia hapa nchini.
  Alisema kuwa asilimia hizo ni zaidi ya theluthi mbili ya Watanzania ambao walihojiwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
  Katika utafiti huo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata asilimia 10 wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi alipata asilimia 9.
  Gunda aliongeza kuwa Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) , Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Dkt Salim Ahmed Salim walipa asilimia moja kwa kila mmoja wao ya Watanzania wenye uwezo kupiga kura wakipenda kuwa wanafaa kuwa Rais.
  Meneja huyo alisema kuwa katika utafiti wao asilimia mbili ya wahoojiwa wote walisema kuwa wasingependa kueleza nani wangependa awe Rais wakati asilimia mbili nyingine hawajui wa kumchagua.
  Aidha katika utafiti huo Chama cha Mapinduzi kilioneka kuwa watu wengi walio karibu nacho kwa kuapa asilimia 70, CHADEMA asilimia 17, CUF asilimia 9, NCCR-Mageuzi kuwa na asilimia 2 huku TLP na UDP zikiwa na asilimia moja kila kimoja.

  Source Michuzi Blog
   
 2. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Can you trust this guy,Abdallal Gunda?

  Tanzania hatuna kitu kama Gallup poll,hata magazeti yetu hayaaminiki kufanya scientific polling
   
 3. K

  Kachero JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri propaganda ndio zimeanza na kampeni za chini chini kuonyesha kuwa JK hapingiki ndio zimeanza.

  Hili linafanyika ikiwa ni jitihada za kuzima maandalizi ya watu wenye uwezo kujitokeza kugombea kiti cha Urais na huu ni uzandiki.
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,464
  Likes Received: 26,354
  Trophy Points: 280
  Hii 70% ndiyo ile fata upepo aliyosema mkulu mwenyewe?
   
 5. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo synovate wamekutana na wanahabari na kutangaza matokeo ya utafiti wao kuhusu hali ya taifa. Wametaja kuwa Kikwete anaongoza kwa kuwa na asilimia 70 akifutiwa na Freeman Mbowe mwenye asilimia 10, akiwa ametangulia kidogo Lipumba. Hii ni katika nafasi ya urais.

  Katika bunge utafiti wao unaonyesha kwamba Zitto Kabwe ndiye mbunge bora kuliko wote akifuatiwa na Anna Kilango. Katika matokeo hayo Mbunge mwingine bora anayetajwa ni Jerry Silaa ambaye ni diwani wa ukonga. Utafiti huo unasema kwamba wananchi wapatao elfu mbili waliohojiwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamemtaja diwani huyo kuwa anachapa kazi kwa kiwango kikubwa na wakiamini kwamba ni mbunge. Katika utafiti huo Dr Slaa anatajwa kuwa nyuma.

  Kwa upande wa vyama matokeo yanaonyesha kwamba CCM iko karibu zaidi na wananchi kwa asilimia 70 ikifuatiwa na CHADEMA yenye asilimia 14.

  ......ndiyohiyo
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  waliulizwa ni chama kinahusishwa na ufisadi na uporaji wa maliasili za taifa?
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Jerry Silaa ni Mbunge wa wapi na amefanya nini mpaka naye awemo kwenye list?
   
 8. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 1,052
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  Huu utafiti umefanyiwa CCM Lumumba wakati wa chai ya saa nne leo 22/2/2010.
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,158
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ...sasa kama wananchi waliulizwa 90% walikuwa wanachama wa CCM, unategemea nini?
   
 10. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo utafiti waonyeshe dodoso lao isije ikawa wamewachanganya wananchi kuhusu jina la Dr Slaa na Silaa, ili kugawanya maoni kuhusu Dr Slaa. Diwani Silaa ni nani katika nchi hii mpaka aingizwe katika hojaji? Mwakyembe ameshika nafasi ya ngapi pamoja na Samuel Sitta?

  serayamajimbo
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hii nimeipenda.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  ndiyo hivyo mojwapo ya maswali ambayo wangetupa tuelewe ni kuwa ni wangapi wana jiconsider kuwa ni mashabiki au wanachama wa CCM..
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  UPUUZI MTUPU! :confused:
  Kipi alichokifanya Kikwete tangu aingine madarakani kinachostahili apate 70%!? :confused: Juhudi zake za kutetea mafisadi wa EPA, Richmond, Kiwira etc!?
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Acheni ujinga wenu wa kuspin mambo ; huyo mnaempigia debe watu hawamtaki na ndio maana siku hizi mmeimalisha ulinzi wake!! Msiwatukane watanzania kwa kubandika matokeo ya propaganda kwa kufanya hivyo mnaahilisha matatizo na kuzidi kupandisha hasira ya wadanganyika!!Haiwezekani kuwa Jakaya akapata marks nyingi hivyo wakati chama anachoongoza KINABAKA haki za msingi za wananchi za kuwa na mgombea wakujitegemea!! Ubakaji huu wa katiba ya nchi ni sawa na kubadilisha katiba ili iwanufaishe wale waliomadarakani na matokeo yake ni mabaya kama yaliyowapata wenzetu huko Niger! Ccm lazima ijue kuwa serikali yao inategemea sana majeshi lakini wanajeshi hawaigopi serikali bali wanawaogopa wananchi kwani jeshi haliwezi kushindana na nguvu ya wananchi; inapoonekana kuwa wananchi hawaiungi mkono serikali yao hapo ndipo wanajeshi huwa wana jaza ombwe na matokeo yake si mazuri. CCM msijidanganye, nguvu ya wananchi[umma] ni kubwa kuliko majeshi. Take notice!!
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,137
  Likes Received: 27,113
  Trophy Points: 280
  huyo jer ni nani ?
  kafanya nn kwa watanzania?
   
 16. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 6,942
  Likes Received: 23,655
  Trophy Points: 280
  Huu ni utafiti au utafuti, nadhani kuna cha kuhoji hapa. Moja kuwauliza wa Tz nzima kuhusu diwani wa ukonga ni kuikosea heshima tasnia ya utafiti, huyu diwani tangu nianze kuwa karibu na vyombo vya habari amefanya Habari kubwa mbili, moja ni kuwasindikiza warembo wa ilala katika ofisi ya mkuu wa mkoa na pia gazeti la Nipashe liliwahi kutoa nini anatarajia kufanya. Kikundi hiki cha watafiti nadhani kuna baadhi ya sifa hawajataka kutupatia kuhusu respondent wao, kwa mfano, ndiyo ni watanzania lakini, wanaamini katika chama gani, je Kikwete aliwekwa kama rais ama m/kit wa ccm. Kina Mbowe na Lipumba waliwekwa kundi gani.

  Mbunge bora! katika nini, kuvaa, kusema sana bungeni, kuchangia sana miswada ama kuongea kwa jazba. tunawajua wabunge makini wanaofanya kzi yao kikamilifu ya kuwawakilisha wananchi na si kujiwakilisha wao kwa kusema maslahi yao kwa sauti kubwa.

  Tubadilike na kwa kweli naunga mkono kwa kukubalina na huyu bwana anayesema utafiti huu ulifanyika pale Lumumba wakati wa chai ya asubuhi, pumbaf kabisa.
  UKWELI HAUFI HATA KAMA UONGO UTATAMALAKI
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,572
  Likes Received: 6,705
  Trophy Points: 280
  ..hii nchi imekuwa neglected and abused kwa muda mrefu sana na matokeo yake ndiyo hayo mnayoyaona sasa hivi. kwa mfano: elimu imetelekezwa kwa muda mrefu kiasi kwamba leo hii ukijenga madarasa na usiyapatie waalimu na vifaa wananchi wanaridhika na kuwapeleka watoto wao huko.

  ..ole wao CCM wananchi wakijua maana halisi ya maendeleo na jinsi ya kudadisi na kupima utendaji wa viongozi na serikali.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,524
  Likes Received: 576
  Trophy Points: 280
  MwanaKJJ, nimeipenda hiyo hapo juu.

  Hivi hii kitu nani aliagiza ifanyike na nani kailipia?

  Isije kuwa imefanywa kwa maagizo ya Mfalme wetu Wanyamwezi kutoka Igunga.
   
 19. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,316
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Pamoja na uelewa wangu katika michakato ya kuandaa tafiti (sampling procedures). Hiyo yenye nyekundu hapo juu inanifanya niupasishe huu utafiti kwa 90% lakini chini ya sifuri.

  Hiyo ya kijani inatushawishi tuamini kuwa waliohojiwa ni wakazi wa kati sijui ya ukonga au ndio kinyerezi!

  Umesema aliyefanya huo utafiti ni mtafiti! Hebu tupe Jina lake ili tuweze kuangalia rekodi yake katika makala alizochapisha kwenye majarida yanayokubalika isije ikawa anafanya tafiti zinazoishia manzese kama Ngawaiya. Siku hizi watafiti ni wengi wakiwemo wa kutafiti matumbo yao yanahitaji kiasi gani.
   
 20. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Silaumu waliokusanya statistics,.. nalaumu uelewa wa waTanzania... kweli Anna Kilango ndio mbunge effective kuliko wote CCM... nina hakika hata ukimuuliza Sitta na Wabunge wengine watakwambia hapana... kuongea kwa sauti kubwa au kwa uchungu sio tija!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...