Matokeo ya utafiti CHADEMA ina nafasi kubwa kushinda kata ya Vijibweni Kigamboni, Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya utafiti CHADEMA ina nafasi kubwa kushinda kata ya Vijibweni Kigamboni, Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Mar 2, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi mdogo wa kata ya vijibweni unaanza rasmi wiki ijayo ( Baada ya Diwani wa CUF kufariki). Kwa mujibu wa taratibu zetu tulipaswa kufanya utafiti ili kujua mtaji wetu na maeneo yanayohitaji maboresho na kuwekewa nguvu.
  Kamati ya utafiti na baadaye Timu ya kampeni ilihusisha viongozi wote wa majimbo ya mkoa wa Dsm na madiwani. Utafiti huu ushirikisha zaidi ya viongozi 20 wakiwepo viongozi wa kata husika. Kamati hii iliongozwa na Mwenyekiti Filipa Mturano –Mbunge na Mikael P Aweda – Katibu.
  Taratibu zote za utafiti zilitumika ikiwepo kutoonesha identity ya mtaifiti. Tulipeana shule ya kutosha kabla ya kufanya utafiti huo kuhusu mbinu za kufanya utafiti.
  Hadidu za rejea ( TOR) zililenga ktk maeneo makuu yafuatayo;
  v Kukubalika kwa Chadema ktk kata husika.
  v Kukubalika kwa Mgombea ndani ya kata ya vijibweni,
  v Kero za msingi zinazowasumbua wakazi ambazo wangetaka zifanyiwe kazi na Diwani.
  v Nguvu na weekness ya CCM.
  v Athari za proganda za udini zinazoenezwa kuhusu Chadema.
  Tumewahoji vijiana, wazee na wamama 260 kutoka mitaa yote 4 kwa siku tatu

  Hadidu ya nne - Propaganda ya udini dhidi ya Chadema.

  Kata ya vijibweni ina wakazi waislamu na wakristo nusu kwa nusu kwa kukadiria. Kwa hiyo, wale wanachadema ambao ni waislamu tuliwauliza swali la pili . Je, una maoni gani kuwa Chama chako kinahusishwa na dini ya kikirisho na wewe ni Mwislamu? 97 % walijibu haina udini. Walipobanwa kwa nini unadhahani hakuna udini wakati udini unasemwa na viongozi na vyombo vya habari? Walitoa sababu 2 kujitetea.
  • walijibu huo ni uwongo wa wanaccm, walisema hivyo hivyo kwa CUF.
  • wanasema hakina udini kwa sababu viongozi wa kitaifa ni wa dini zote
  • wachache wanasema hawana majibu lakini hakuna udini.
  3% wanasema inawezekana kuna udini bado hawajathibitisha.
  Matokeo ya hadidu nyingine za rejea naomba nisitoe kwa leo ili nisiwafaidi wapinzani wetu .

  Chadema imemteua msomi mwenye Shahada toka Chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Mwl Nyerere Isaya Charles kupeperusha bendera yetu.


  Kwa ujumla matokeo ya utafiti yameonesha kuwa Chadema ina nafasi kubwa ya kushinda kata ya vijibweni kwa zaidi ya 70%
  kama uchaguzi utakuwa huru na haki ( Can not explain the details how?)


  Wanachadema na washabiki wake ambao wangependa kushirikiana nasi kwa namna moja au nyingine kampeni zitakapoanza wawasiliane na viongozi wa kata au jimbo la kigomboni. Kama huna contact zao wasiliana na mimi au Mkiti wa kamati ya kamati ya kampeni Filipa Mturano

  My take;
  Japokuwa utafiti una gharama kubwa sana lakini tija yake ni kubwa sana ktk siasa za kisasa.
  Propaganda za udini zilizofanikiwa kuiua CUF naona sasa imechuja, imekwama jumla. 3% is negligible, tena hawakuwa na hoja za kujustisty hofu yao ya udini. Ikumbukwe karibu wote ni watu wazima.

  NAWASHAURI WANAOHOJI GHARAMA ANAYOTUMIA JOHN MREMA ARUMERU KWENYE KEYBOARD YA LAPTOP WAJE HUKU MTAANI VIJIBWENI WAONE GHARAMA YA WATU 24 KWA SIKU 3 NI KIASI GANI. KUANZIA CHAKULA, MALAZI, MAFUTA YA MAGARI, NAULI, STATIONARY NK. WAKITOKA HUKU WATAELEWA.
  Nawasilisha.
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu, hii ndiyo Chadema tunayotaka!! We are in 21st century, lazima mambo yaende kisayansi na kiuhalisia. Hakuna haja ya kuendelea kukumbatia mifumo ya kikoloni, by the way, tunajidanganya wenyewe tukiendelea kudanganyana sisi kwa sisi. Bravo mkuu! All the best makamanda, tupo pamoja!
   
 3. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Welldone kamanda ,kata tumeshachukua hizo!
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aisee nimeipenda sana hii. Kufanya mambo kisayansi ndo siasa ya kweli

  Bravo CHADEMA! Hongereni sana
   
 5. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hongera kwa kazi nzuri hiyo ndo inatakiwa................hapo tutaenda tukijua tuwekeze nguvu kiasi gani........safi sana.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni nzuri hii!
  Kwa namna hii mnaweza hata kujua kama mu'invest kiasi gani katika kuwania nafasi iliyopo, kuliko kujiingiza ki'Layman.

  Mtikila SIJUI KAMA ANAPITIA HUMU, maana anaonekana huku Arusha akikamilisha mipango ya kugombea Arumeru, wakati angeenda kwa utafiti angebaki kwa mkewe, au kuendelea na kesi mahakamani alizoziweka pending.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mungu awape maisha marefu na wote tuseme AMEN.
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwani huyo mzee wetu ana kesi gani tena?
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu kichwa cha habari ni kuhusu ushindi lakini ndani unaonekana kuonyesha zaidi kuwa watu hawakubali kuwa CDM ina udini na mwisho una conclude kwamba itashinda kwa 70%. Mbona sioni ukisema kuwa tuliwahoji watu kadhaa kama wataipigia kura CDM na 70% wakasema wataipigia.

  Hii nadhani ilikuwa feasibility Study kama ile ya Mrema kule Arumeru, mlitumia kiasi gani?

  Nimeuliza tu sitaki matusi nataka majibu.
   
 10. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ungeonyesha jinsi gani uliwapata study participants, ningeweza kukuelewa! Most of the time ikiwa unachagua participants randomly inasaidia kuondoa kuegemea katika upande fulani (biasness).
  Nani alihusika kufanya utafiti huo! unafikili mwana CDM anafanya utafiti atakuja na majibu gani?

  "Walipobanwa kwa nini unadhahani hakuna udini wakati udini unasemwa na viongozi na vyombo vya habari?" Kitafiti hili ni open question? mara nyingi linahitaji utaalamu wa kutosha,majibu yake huathiriwa sana na nature ya muulizaji, usipokuwa makini katika hili utapata response zenye kukufurahisha tu.

  kwa kukumbusha tu: Gazeti la mwananchi lilikusanya kura za maoni kipindi cha uchaguzi kuuliza nani anafaa kuwa rais, slaa aliongoza kwa zaidi ya 67%, ukibase argument yako kwa tafiti kama ile unakuwa uko far from reality kwa kuwa gazeti hili linafahamika habari zake sio independent kwa hiyo lazima na wapenzi wake sio neutral. In return hali ikawa tofauti.

  Ni hayo tu!
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sijui kutukana mkuu usijali,
  Hebu soma tena, kati ya hadidu rejea tano nimeelezea mmoja, 4 nimeweka kwapani ili nisiwafaidishe ccm. Hiyo ni siri yetu mkuu.
  Tuliangali kukubalika chama, Kukubalika kwa mgombea na kero kuu za kata ile. Sasa nikayaweka hapa yote ccm waka print si itakuwa kazi ya bure? Wewe jua yafuatayo; 1.chadema inakubalika 2. tunajua kero zote za kata by even by priority ya wananchi, 3.tunajua nguvu na weekness ya wagombea wote wa ccm na chadema. can not put every thing here.
  Gharama tutampelekea mtendaji mkuu wa Chama Dr Slaa, hiyo wewe usipate shida. Nikiangalia gharama ya kata mmoja nikilinganisha hizo kata 17 za John Mrema huko Arumeru, najua wanaolalamika hawajui mtaani kukoje, wanajua kutumia key board tu.
   
 12. S

  SIPIYU30 JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 686
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Aweda,
  Nakubaliana na hoja yako: Natatizika na jambo moja tuu, kwamba wewe ni mpiganaji wa Chadema, na wewe ndiye uliyefanya huo utafiti, kwa vyovyote vile, by hoocks and crooks, lazima mnapenda Chadema ishinde. Je hauoni kuwa hiyo research inaweza kuwa biased? CCM (Magamba) wanaweza kuja hapa na kudai kuwa hizo ni propaganda tuu?

  Hata hivyo mimi binafsi nakubaliana na wewe na ninawaombea ushindi daima. nakuaminia kaka yangu wa pale sarwatt
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mikael P Awenda.
  Hii ni mara ya tatu kukusoma ukitoa tathimini na tafiti zako za uchaguzi.

  Ulitoa tathimini uchaguzi wa Igunga kuwa Chadema watashinda matokeo yake tukayaona.

  Mara ya pili ulitoa tathamini yako kwenye uchaguzi wa Uzini tena kupitia ITV ulisema Chadema Zanzibar wameipokea kwa nguvu na watashinda Uzini.

  Mkuu siku zote tathimini zako zinakuwa na utata.
   
 14. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama ametoa kazi kwa mtu mwingine itakuwa ni utafiti mzuri sana na unaowatia moyo
   
 15. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aweda wewe ni Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Ukonga ungekuwa umefanya hivi katika eneo lako tungefaidika sana, ninasema hivyo kwa sababu kazi nzuri kama hii umefanya sehemu nyingine na sehemu yako inadorora.
  Kwanza kabisa ninasema hivyo kwa sababu mie ni mmoja wa wananchi ninaekaa Kitunda ambapo sijawahi kusikia hata siku moja umefanya japo mkutano wa hadhara wa kujitambulisha kwa wananchi kama ndiyo Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Ukonga.
  Pili sijakuona hata siku moja katika Jimbo la Ukonga japo ukifungua tawi kwa minadili ya kukiimarisha chama kama wanavyofanya wenzako katika majimbo yao.
  Tatu napenda kukufahamisha kuwa CHADEMA inapendwa sana eneo lako lakini hawajui pa kukimbilia maana hata ofisi za kata hawajui zinapopatikana na kuamua kupandisha bendera tu, lakini uongozi wa jimbo haujawahi hata kwenda kuwatembelea tu.
  My Take: Naomba ujaribu kufanya research kama hii jiimboni kwako na itasaidia kukinufaisha chama Ukonga.
   
 16. d

  davidie JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  utafiti wa kura za urais kuhusu dr slaa ulikua wa kweli kabisa ukiondoa tabia ya wizi na kuchakachua matokeo slaa alishinda
   
 17. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  niwazi kabisa mgombea akiwekwa wa cdm atasaidia ccm kushinda kutokana natafiti uchwara za namna tunajua kabisa natural ya watu wa vijibweni ndomana ikawa rahisi sana mgombea wa cuf kushinda. Kwakuwa tafiti ipo pande mbili yani imeangalia ccm na cdm huku ikiacha cuf ambayöo ndiyo miliki wa kata hiyo tamaa za cdm zitaipa ushindi ccm ni wazi
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,678
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Huoni kama kuna sampling problem hapo kwenye nyekundu? Kwanini uwaulize wanachadema waislamu?
  Results are always better when your sample is randomly selected, and grouped based on predominance.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu utafiti ulifanywa kwa jinsi ambavyo aweda amefanya huko vijibweni? Basi kama ni hivyo haukuwa na mashiko. Siamini kama ulikuwa wa aina hii!
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa hakukuwa na utafiti uwao wote kwa std hata za chini kabisa za utafiti. Reliability yake ni almost zero. Angesema kwamba ni maoni yake mimi ningekubali ila hili la kuchukua maneno yake na kuwawekea watu kinywani siyakubali.
  Pamoja na hayo wakuu hii pia inaonyesha aina ya tafiti tunazozifanya hasa vyuoni hapa nchini. Mtu anakaa chini anajitungia napeleka kwa msimamizi naye anabariki. Matokeo yake ndiyo haya sasa! Simlaumu Aweda nalaumu system yetu kuanzia tafiti za wanafunzi huko vyuoni ambazo asilimia 99 ni za kupika.
   
Loading...