Elections 2010 Matokeo ya uraisi....

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,636
Jamani eeeh matokeo ya uraisi vipi? Mbona hakuna anayeyazungumzia? Maana kila mtu kajikita kwenye ubunge...kwa nini ya uraisi hayazungumziwi wala kutolewa?
 
hatuhangaiki na Urais kwa kuwa taswira iko clear kuwa JK atachukua. ni vema tu-concetrate kwenye ubunge na udiwani. ya Urais yataumiza vichwa vyetu pasipo sababu.
 
Jamani mbona matokeo yanayokuja ni ya upinzani tu?? Naogopa isijetokea kama kule Zamibia 2006, matokeo yalipotoka upinzani walikuwa wanaongoza. Kumbe wenzao waliwatangulizia hayo matokeo ili wakati wanasherekea wao wanachakachua kwenye ngome zao then mwishoni kabisa matokeo yanabadilika.

JK alifanya kampeni yeye na familia yake. Kwa hiyo sidhani kama atakuwa interested kusaidia mtu badala ya kujisaidia mwenyewe. Hivyo sasa wakati watu wanashangilia matokeo ya ubunge jamaa wanachakachua ya urais.
 
Nimewasikitikia Singida mjini...wamempa jk 19,000 dhidi ya 5,000 za daktari wa ukweli..
 
JHivyo sasa wakati watu wanashangilia matokeo ya ubunge jamaa wanachakachua ya urais.

Hiyo ndiyo hofu yangu mimi maana nadhari yote tumeielekeza kwenye ubunge na uraisi tumesahau kabisa. Au Dkt. wa kweli hana nafasi hata kidogo ya kushinda?
 
Jamani eeeh matokeo ya uraisi vipi? Mbona hakuna anayeyazungumzia? Maana kila mtu kajikita kwenye ubunge...kwa nini ya uraisi hayazungumziwi wala kutolewa?

Nyani,

Ni kwasababu urais dalili zote toka mikoani zinaonyesha JK anashinda. Kwenye majimbo ya vijijini tofauti ya kura ni kubwa sana.
 
Jamani eeeh matokeo ya uraisi vipi? Mbona hakuna anayeyazungumzia? Maana kila mtu kajikita kwenye ubunge...kwa nini ya uraisi hayazungumziwi wala kutolewa?

Hao jamaa wamejikita kule kwa Kibunango ndo wapo busy kutangaza mpaka sasa Seif anaongoza
 
hatuhangaiki na Urais kwa kuwa taswira iko clear kuwa JK atachukua. ni vema tu-concetrate kwenye ubunge na udiwani. ya Urais yataumiza vichwa vyetu pasipo sababu.


mambo yanaweza kuwa ndivyo sivyo jackoB tuna uhakika na Slaa kufanya vyema vyanzo JF tunaomba update za DR Slaa VS DR Kikwete mpaka sasa
 
jamani, najua kwa upande wa Urais CCM wanataka kuchakachua.
Wadau, watu wawe makini, kila wakala/diwani akusanye data zote za kura za uraisi kwenye kata yake na azipeleke kwa Mbunge wake wa chama. Kwa maana hiyo kila Mbunge wa CHADEMA kwenye kila wilaya atakua na list ya kura zake kwenye kila kata.
then sisi tupate taarifa hiyo kutoka kwa wabunge wa kila wilaya then tunaweza kufanya analysis na kuona kwa nafasi ya Urais tuko wapi.
Wakuu tulifanyie kazi hili kuepusha uchakachuaji wa CCM Pls....
 
Nimewasikitikia Singida mjini...wamempa jk 19,000 dhidi ya 5,000 za daktari wa ukweli..

wana mihela ya kulipa ada hawa,life lao ni zuri sana umeme kwao haukatiki hata sku moja barabara ya lami kila sehemu na nyumba zao zote ni nzuri kwa kweli hawa jamaa kama vile hawaishi tanzania
 
jamani eeeh matokeo ya uraisi vipi? Mbona hakuna anayeyazungumzia? Maana kila mtu kajikita kwenye ubunge...kwa nini ya uraisi hayazungumziwi wala kutolewa?

jk amepiga stop wasiyatangaze anaogopa yatasababisha tention nchini kwa kuwa matokeo ya awali yanaonyesha slaa anaongoza...wakuu lengo la kugoma kutangaza pia ni kusababisha watu waanze kuyadai....ili watume vikosi vya jeshi kuzima vurugu feki na ikiwemo kusababisha mabox yavurugike alafu uchaguzi uwe umeharibika...
 
Wasije wakawa katika mchakato wa uchakachuaji maana kwenye ubunge ngoma imekuwa ngumu kuchakachua
 
Hofu yangu ni kwamba JF naona interest ya waliowengi ni kwenye majimbo ya uchaguzi ambayo yanaonesha Chadema inaongoza na hawataki kabsaaaa kusema pale Chadema inapoangukia pua ndio maana nakua na wasiwasi juu ya taarifa nyingi. sitaki tuumizane kwa kupeana matumaini makubwa. Dr. JK bado atashinda ila kwa asilimia ngapi, bado nim kitendawili. Thithiem bado wako fiti maeneo mengi kinoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom