Elections 2010 Matokeo ya Urais kwa jimbo la Karatu yako wapi?

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
965
1,000
nimepita kwenye mtandao watume ya uchaguzi ili kujua matokeo ya urais jimboni humo lakini jimbo hilo na matokeo yake hayapo. nini kilichojiri mpaka matokeo yasiwekwe kwenye website ya NEC?
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Hawakutaka kuonyesha, kwa sababu aligaragazwa kwa aibu kubwa mno. Siyo Karatu tu, hata baadhi ya majimbo ya mkoa wa kilimanjaro hawakuonyesha, Jimbo la Kyela ambalo ameshinda Mwakyembe kura za rais hawakutaka kuonyesha kwa kuwa kiukweli alipigwa bao.
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290

Katika jimbo loa Kyela, Kikwete alipata 23,000+ kwa 21,000+ za Dr. Slaa.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,757
2,000
Katika jimbo loa Kyela, Kikwete alipata 23,000+ kwa 21,000+ za Dr. Slaa.

Haiwezekani Kikwete akapata kura nyingi kuliko Dr.Slaa Kyela kwasababu watu wa kule wanaamini kuwa huyu bwana hampendi mbunge wao na ndio maana hata akamteua Mwakipesile [aliyekuwa ameshindwa na mbunge wao kwenye kura za maoni za kugombea ubunge ] kuwa mkuu wa mkoa huo huo wa Mbeya ili amthibiti!! Kura hizo walichakachua lazima.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,635
2,000
Matokeo yake ni ya kuchakachuliwa na wala hayana maana yoyote kwa sababu NEC walijitungia majibu waliyoyataka..............
 
Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
195
Matokeo yake ni ya kuchakachuliwa na wala hayana maana yoyote kwa sababu NEC walijitungia majibu waliyoyataka..............
Ni lazima kupigania kura zote hizo ziingizwe katika idadi kwani hii inagusa idadi ya wabunge wa viti maalumu si suala la kuacha lipite hivi hivi.Vilevile sitashangaa kuona hiyo asilimia ikiwa ni 30 badala ya hiyo 61 ya kupikwa.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Katika jimbo loa Kyela, Kikwete alipata 23,000+ kwa 21,000+ za Dr. Slaa.

Hapana Butola, kura za Kyela kutoka jimboni zilionyesha kuwa Dr. Slaa alipata 28,567 wakati Kikwete alipata 18,381, lakini zilipofika tume ya uchaguzi wakachakachua kibabe. Kama walivyofanya kule Hai.
 
makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,641
2,000
nimepita kwenye mtandao watume ya uchaguzi ili kujua matokeo ya urais jimboni humo lakini jimbo hilo na matokeo yake hayapo. nini kilichojiri mpaka matokeo yasiwekwe kwenye website ya NEC?

Is not only Karatu, majimbo yote ambayo CCM wamehenyeshwa hawajaweka matokeo kwenye website yao.Kama wameweka ni yale yaliyokuwa yamechakachuliwa. Ni wizi mtupu.Yale ambayo CCM walikuwa wanashinda walikuwa wakiya-post haraka sana kwenye website. Ilikuwa kuwafanya watu wasijue kinachoendelea.
Mimi nimeshasema this can be one of the evidences za kuwabana NEC. Kwanini hawajayaweka kwenye website, hapa walikuwa wanaficha baadhi ya figures kuwa-confuse Watz.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom