Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani ni ushindi kwa CCM au CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya Uchaguzi wa Madiwani ni ushindi kwa CCM au CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyota Njema, Oct 31, 2012.

 1. N

  Nyota Njema Senior Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matokeo ya uchaguzi wa madiwani katika kata 29 zilizofanya chaguzi ndogo hivi karibuni yanaonekana kukosa mjadala mpana kutoka kwa wadau wa siasa hapa nchini, lakini mimi naona kama yana haja ya kujadiliwa ili kuona mstakabali wa siasa hapa nchini unaendaje na hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao wanahitaji mabadiliko makubwa ya kisiasa ili kuikwamua nchi na uchumi tegemezi wa nchi hii yenye rasilimali nyingi, huku nyingine zikiwa adimu duniani.

  Nilimuona Katibu mwenezi wa CCM ndugu Nape Nauye akizisifia tambo za chama hicho kuwa kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo; jambo ambalo limenifanya niwe na tafakari kubwa ni kuwa, je, ni kweli huu ni ushindi wa kishindo kwa CCM au kwa sababu Katibu huyo ni chombo cha propaganda na hivyo alikuwa anatimiza wajibu wake kwa kutueleza hivyo?

  Kwanza, naomba nikubaliane na Nape kuwa CCM ilipata viti vingi vya udiwani katika uchaguzi huo kuliko vyama vingine; lakini pili naomba ufafanuzi wa "great thinkers" wengine kuwa, je ushindi huu ni kweli unazidi kuifanya CCM kuwa imara kiasi kwamba Katibu wake mwenezi anaweza kusimama kwenye vyombo vya habari kuusifia bila kutaja mapungufu chama hicho kiliyoyapata huku akimkejeri Katibu Mkuu wa CHADEMA? Hoja au swali langu litajikita katika mambo au maswali makubwa mawili;

  1. Katika uchaguzi huo wa kata 29, kabla ya kata hizo kubaki wazi kata 26 zilikuwa ni za madiwani wa CCM, 2 za CHADEAMA na 1 ya TLP. Katika uchaguzi huu CCM wamekomboa kata 22 tu na kupoteza nyingine 4, wakati CHADEMA wamekomboa kata zote 2 na kupata kata mpya 3 kutoka mikononi mwa CCM, TLP imekomboa kata yake moja, huku CUF nayo ikibeba kata moja iliyokuwa ya CCM. Hapa ushindi unakuwa ni wa nani hasa, kama sio wa CHADEMA na CUF ambao wamepata kata mpya? Katika uchaguzi huo, CCM pekee ndiyo iliyopoteza kata zake wakati TLP wametetea kata yao!


  2. Pamoja na mchanganuo uliotajwa hapo juu, ni kwanini, pamoja na kuwa CCM ndiyo iliyopoteza kata 4, lakini imekuwa ni ya kwanza kujitokeza kwenye vyombo vya habari kutangaza kuwa imepata ushindi wa kishindo? Je ilikuwa na wasiwasi kuwa ingelipoteza kata nyingi zaidi kuliko hizo ilizopoteza? Na kama ni hivyo, ni kwa nini hasa kama sio imani kuwa chama hicho kimepoteza mvuto wao kwa wapiga kura na hivyo mategemeo ya Nape na wenzake yalikuwa ni kupoteza kata nyingi zaidi kwa wapinzani na hasa CHADEMA? Je tukifanya utafiti zaidi hatutagundua kuwa hata kura CCM ilizozipata katika kata iliyoshinda zitakuwa zimepungua sana ikilinganishwa na zile ilizozipata wakati wa uchaguzi mkuu uliopita? Je huo ni ushindi wa kishindo au ni kushuka kwa kukubalika kwake kwa wananchi, na kama ni hivyo, je maneno ya Nape yana ukweli wowote kuwa M4C haijaisaidia lolote CHADEMA? Je kwa Nape ni bora CCM kufa polepole kuliko kufa haraka haraka maana yeye atakuwa ameshapata mtaji wake?


  Hebu tulijadili hili maana mimi naona kuwa, kama ambavyo CCM ilivyoanza kupoteza kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu uliopita, ndivyo inavyoendelea kupoteza katika chaguzi zinazoendelea. Nikiangalia mfumo wa Tume ya Uchaguzi kwa sasa, ikiwa ni pamoja na mapungufu katika uboreshaji wa daftari la wapiga kura; nakiona dhahiri kifo cha CCM ifikapo 2015 endapo mabadiliko makubwa yatakuwa yamefanyika ndani ya Katiba mpya ili kuruhusu sheria na taratibu za usawa katika upigaji wa kura. Swali linabaki kuwa, je Nape kama kiongozi mkubwa ndani ya CCM hawezi kuwa na upeo wa kuyaona haya? Na kama anayaona kweli, kwa nini anafikiri watanzania ni wajinga kiasi cha kueneza propaganda ya uongo ambayo mwisho wa siku itakigeukia chama chake? Hii ndio busara ya uongozi wote wa CCM au ni ya Nape peke yake? Na kama ni ya kwake peke yake, kwa nini wanakaa kimya wakati anaendelea kuwaonyesha watanzania kuwa CCM ni chama kinachojijenga kwa kuwaambia uongo na majigambo yasiyo na mashiko?
   
Loading...