Matokeo Ya Uchaguzi; Tafsiri Yangu ( Makala Raia Mwema)

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
( Makala hii imechapwa kwenye Raia Mwema, Novemba 3, 2010)Na Maggid Mjengwa,

MTOTO anayetegemea maziwa toka titi la mama anafanyaje anapolikosa? Jibu lake; mtoto huyo atahangaika sana, na kama ataliona titi lingine, atalishika alinyonye, hata kama si la mama yake. Na mtu mzima anafanyaje? Nawe una majibu yako.

Hatimaye Watanzania tumeshiriki tena kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wetu. Katika nchi , matokeo ya uchaguzi yana maana pia ya ujumbe au salamu zinazotolewa na walioshiriki uchaguzi huo; yaani wananchi kwenda kwa viongozi.
Nionavyo, matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu yamebeba ujumbe mmoja mkubwa, lakini mfupi sana; MABADILIKO.

Kwamba umma umeanza kwa dhati kabisa kuonyesha unataka mabadiliko. Hamasa ya kisiasa imeongezeka. Kazi ya wanasiasa na hususan vyama vya siasa ni kusaidia kuyaongoza mabadiliko hayo katika njia salama.
Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa mara nyingine tena, kama kutakuwapo na dhamira ya kisiasa, yanakipa Chama Cha Mapinduzi, jukumu hilo kubwa la kuyaongoza mabadiliko hayo.

Kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika sio tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.

Kuna watakaopuuza, lakini kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimeipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi.
Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.

Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala.

Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge.
Isifike mahali Chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo.

Ndio, CCM inahitaji mabadiliko makubwa; maana CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao. Wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi.

Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!

Hapa kuna tatizo kubwa, kuwa kuna wanaotafuta uongozi, wakiupata, si tu wanatumia muda mwingi kujipanga na kujiandalia yenye manufaa wao wenyewe. Wanawasahau wananchi na chama chenyewe. Wanajitafutia umaarufu wao, na wanasahau kufanya kazi ya kukipa chama umaarufu.

Huu ni wakati pia kwa Chama Cha Mapinduzi kuanzisha rasmi mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya. Inawezekana, kama tutaanza sasa mchakato huo, kwa Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu ujao tukiwa na Katiba mpya. Katiba itakayotokana na matashi ya Watanzania kwa uwingi wao na wala si kikundi kidogo cha watu. Maana, kwa hakika, Katiba yetu ya sasa isiyoendana na mahitaji ya wakati uliopo na ujao ni kiini pia cha matatizo yetu mengi.

Kwa mwanadamu, siku zote, ni vema na ni busara kuheshimu anachotaka mtu mzima mwenzako. Uheshimu mawazo hayo hata kama ni wewe ndiye mwenye maamuzi. Maana, ukifanya maamuzi yenye kwenda kinyume na anachotaka mtu mzima mwenzako, basi, ukimpa nafasi na yeye afanye maamuzi, atafanya maamuzi yaliyo kinyume na unachotaka wewe. Busara ni kutambua, kuwa unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini, kamwe huwezi kumlazimisha punda huyo kuyanywa maji.

Hata kama kazi ya uandishi si ya utabiri, lakini mengine tunayoyaona sasa tumeshayaandika huko nyuma. Zikiwa zimebaki siku 45 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, kwa hali niliyoiona wakati huo, nilibainisha kuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete angeibuka mshindi . Dr Wilbroad Slaa ( CHADEMA) angechukua nafasi ya pili na huku Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF) akishika nafasi ya tatu kwa nafasi ya Urais. Kwamba CUF wangeibuka kuwa chama cha pili baada ya CCM kwa idadi ya wabunge, hivyo basi, CUF kuwa chama kikubwa cha upinzani bungeni. ( CUF ina wabunge wengi kutoka visiwani).

Nikaandika kuwa Jakaya Kikwete angeunda serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na Upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge. Ni kutokana na ujio wa Dk. Slaa kama mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

Tumeona kuwa ujio wa Dk. Slaa umesaidia kuongeza hamasa ya kisiasa na hata kuchangia chama chake ( CHADEMA) kuvuna viti vingi zaidi. Na hata Profesa Ibrahim Lipumba naye amefanya kazi kubwa kuongeza hamasa ya kisiasa na hata chama hicho kujinyakulia jimbo moja bara na huku Profesa mwenyewe akishika nafasi ya pili kwa kura za urais kwenye mikoa ya kusini.

Hakika, Dk. Slaa na mwenzake Profesa Ibrahim Lipumba wametoa mchango mkubwa na wa kupongezwa katika kusaidia kuingiza wabunge wengi wa upinzani bungeni, na hivyo kusaidia katika kuijenga demokrasia yetu changa.
Huko nyuma niliandika pia; ‘Ni dhahiri Chama Cha Mapinduzi, baada ya Oktoba 31, kinatakiwa kijipange upya kuikabili hali mpya katika uwanja wa kisiasa. Viashiria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana.

Katika hili, CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo." Niliandika hayi huko nyuma. Na hakika, mabadiliko yameanza mijini, yatasambaa mpaka kwenye miji-vijiji, maana mabadiliko haya yana mwangwi wake.

Huko nyuma nilisisitiza pia; " CCM ianze sasa kufikiria namna itakavyounda Serikali miaka ijayo kwa kushirikiana na vyama vingine. Uwezekano wa kuwapo Serikali ya Mseto hata hapa Bara. Ndio, kutoa fursa kwa chama au vyama pinzani vitakavyokuwa na idadi kubwa ya wabunge kushiriki kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. Katika miaka kumi na tano ijayo tutakuwa na Tanzania iliyo tofauti kabisa na ya sasa . Kwamba mtaziona ishara." Niliandika.

Na ishara za jamii inayotaka mabadiliko tumeshaziona. Na tubuni wenyewe Katiba Mpya itakayotuongoza kuelekea kwenye mabadiliko hayo. Katiba ina maana pia ya uwepo wa taratibu za haki na usawa kwa wote.

Ni vema na busara kabisa tukawa na taratibu na nidhamu ya kuzifuata taratibu. Na nidhamu ya kufuata taratibu inatokana na sheria na adhabu zinazoendana na kukiukwa kwa taratibu hizo. Katiba itakayoridhiwa na wengi itatusaidia katika hilo. Inawezekana.mjengwa

hs3.gif
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,057
2,000
Mjengwa:

You can't teach an old dog new tricks. The Tanzanian system of government has run its course. Mataifa mengine ya kiAfrika yalihamua kufuata mfumo wa chama kimoja hili kuepukana na matatizo ya kikabila au kuwapa watawala nguvu zisizo na upinzania.

Kwa Tanzania utawala wa chama kimoja ulikuwa ni kuendeleza siasa za ujamaa. Tanzania imeachana ujamaa lakini bado mfumo wa kiutawala na kisiasa bado ni ule wa ujerumani mashariki, Cuba au North Korea.

Kama unataka demokrasi ya kweli, Tanzania uchukue mfano wa nchi za Hungary, Poland, CzechSlovakia na nchi zingine za ulaya mashariki zilizofanikiwa.

Kwanza ichaguliwe serikali ya muda. Itakayoongozwa na technocrats. Pili liundwe baraza la watu wenye hekima kutoka pande zote za nchi watunge katiba mpya. Kama hilo litashindika, tumieni katiba aliyoacha mwingireza au copy and paste katiba ya USA.

Tatu vyama vya kisiasa vijisajiri upya kwa kutumia katiba mpya. Nne uchaguzi ufanyike ukisimamiwa technocrats ambao hawana uhusiano na chama chochote.
 
Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
1,195
Wakati wa Kampeni hukuyasema haya, kazi ilikuwa ni kuonyesha mapungufu ya CHADEMA na Dr. Slaa. Je, hukumsikia Kikwete akimnadi Mramba [ambaye ana kesi ya ufisadi]? Je, hukumwona/sikia JK akiwanadi Chenge, Lowassa na Rostam ambao wote wanatuhumiwa na ufisadi?

Magazeti yaliandika sana kuhusu mgombea wa CCM wa Jimbo la Muhambwe kwamba ni jambazi na Kamati ya Usalama ya Mkoa iliitwa kutoa taarifa lakini chama chako pendwa kiliziba masikio. Hicho ndio chama chako pendwa, wakati wa kampeni mnakaa kimya hamsemi kasoro za chama chenu, uchaguzi ukipita ndio mnaanza kutuzuga.
 
Double X

Senior Member
Nov 4, 2010
184
0
Sina hata appetite ya kukusoma bw majjid, wewe ni wale wale......!!! huna jipya as long as u a ccm puppet(KIBARAKA!!) endelea nao kuchumia tumbo tu!!
 
Fishyfish

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
231
0
"CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine."

Very true.
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,038
2,000
( Makala hii imechapwa kwenye Raia Mwema, Novemba 3, 2010)Na Maggid Mjengwa,

MTOTO anayetegemea maziwa toka titi la mama anafanyaje anapolikosa? Jibu lake; mtoto huyo atahangaika sana, na kama ataliona titi lingine, atalishika alinyonye, hata kama si la mama yake. Na mtu mzima anafanyaje? Nawe una majibu yako.

Hatimaye Watanzania tumeshiriki tena kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wetu. Katika nchi , matokeo ya uchaguzi yana maana pia ya ujumbe au salamu zinazotolewa na walioshiriki uchaguzi huo; yaani wananchi kwenda kwa viongozi.
Nionavyo, matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu yamebeba ujumbe mmoja mkubwa, lakini mfupi sana; MABADILIKO.

Kwamba umma umeanza kwa dhati kabisa kuonyesha unataka mabadiliko. Hamasa ya kisiasa imeongezeka. Kazi ya wanasiasa na hususan vyama vya siasa ni kusaidia kuyaongoza mabadiliko hayo katika njia salama.
Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa mara nyingine tena, kama kutakuwapo na dhamira ya kisiasa, yanakipa Chama Cha Mapinduzi, jukumu hilo kubwa la kuyaongoza mabadiliko hayo.

Kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika sio tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.

Kuna watakaopuuza, lakini kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimeipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi.
Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.

Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala.

Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge.
Isifike mahali Chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo.

Ndio, CCM inahitaji mabadiliko makubwa; maana CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao. Wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi.

Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!

Hapa kuna tatizo kubwa, kuwa kuna wanaotafuta uongozi, wakiupata, si tu wanatumia muda mwingi kujipanga na kujiandalia yenye manufaa wao wenyewe. Wanawasahau wananchi na chama chenyewe. Wanajitafutia umaarufu wao, na wanasahau kufanya kazi ya kukipa chama umaarufu.Huu ni wakati pia kwa Chama Cha Mapinduzi kuanzisha rasmi mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya. Inawezekana, kama tutaanza sasa mchakato huo, kwa Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu ujao tukiwa na Katiba mpya. Katiba itakayotokana na matashi ya Watanzania kwa uwingi wao na wala si kikundi kidogo cha watu. Maana, kwa hakika, Katiba yetu ya sasa isiyoendana na mahitaji ya wakati uliopo na ujao ni kiini pia cha matatizo yetu mengi.

Kwa mwanadamu, siku zote, ni vema na ni busara kuheshimu anachotaka mtu mzima mwenzako. Uheshimu mawazo hayo hata kama ni wewe ndiye mwenye maamuzi. Maana, ukifanya maamuzi yenye kwenda kinyume na anachotaka mtu mzima mwenzako, basi, ukimpa nafasi na yeye afanye maamuzi, atafanya maamuzi yaliyo kinyume na unachotaka wewe. Busara ni kutambua, kuwa unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini, kamwe huwezi kumlazimisha punda huyo kuyanywa maji.

Hata kama kazi ya uandishi si ya utabiri, lakini mengine tunayoyaona sasa tumeshayaandika huko nyuma. Zikiwa zimebaki siku 45 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, kwa hali niliyoiona wakati huo, nilibainisha kuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete angeibuka mshindi . Dr Wilbroad Slaa ( CHADEMA) angechukua nafasi ya pili na huku Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF) akishika nafasi ya tatu kwa nafasi ya Urais. Kwamba CUF wangeibuka kuwa chama cha pili baada ya CCM kwa idadi ya wabunge, hivyo basi, CUF kuwa chama kikubwa cha upinzani bungeni. ( CUF ina wabunge wengi kutoka visiwani).

Nikaandika kuwa Jakaya Kikwete angeunda serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na Upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge. Ni kutokana na ujio wa Dk. Slaa kama mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

Tumeona kuwa ujio wa Dk. Slaa umesaidia kuongeza hamasa ya kisiasa na hata kuchangia chama chake ( CHADEMA) kuvuna viti vingi zaidi. Na hata Profesa Ibrahim Lipumba naye amefanya kazi kubwa kuongeza hamasa ya kisiasa na hata chama hicho kujinyakulia jimbo moja bara na huku Profesa mwenyewe akishika nafasi ya pili kwa kura za urais kwenye mikoa ya kusini.

Hakika, Dk. Slaa na mwenzake Profesa Ibrahim Lipumba wametoa mchango mkubwa na wa kupongezwa katika kusaidia kuingiza wabunge wengi wa upinzani bungeni, na hivyo kusaidia katika kuijenga demokrasia yetu changa.
Huko nyuma niliandika pia; ‘Ni dhahiri Chama Cha Mapinduzi, baada ya Oktoba 31, kinatakiwa kijipange upya kuikabili hali mpya katika uwanja wa kisiasa. Viashiria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana.

Katika hili, CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo.” Niliandika hayi huko nyuma. Na hakika, mabadiliko yameanza mijini, yatasambaa mpaka kwenye miji-vijiji, maana mabadiliko haya yana mwangwi wake.

Huko nyuma nilisisitiza pia; “ CCM ianze sasa kufikiria namna itakavyounda Serikali miaka ijayo kwa kushirikiana na vyama vingine. Uwezekano wa kuwapo Serikali ya Mseto hata hapa Bara. Ndio, kutoa fursa kwa chama au vyama pinzani vitakavyokuwa na idadi kubwa ya wabunge kushiriki kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. Katika miaka kumi na tano ijayo tutakuwa na Tanzania iliyo tofauti kabisa na ya sasa . Kwamba mtaziona ishara.” Niliandika.

Na ishara za jamii inayotaka mabadiliko tumeshaziona. Na tubuni wenyewe Katiba Mpya itakayotuongoza kuelekea kwenye mabadiliko hayo. Katiba ina maana pia ya uwepo wa taratibu za haki na usawa kwa wote.

Ni vema na busara kabisa tukawa na taratibu na nidhamu ya kuzifuata taratibu. Na nidhamu ya kufuata taratibu inatokana na sheria na adhabu zinazoendana na kukiukwa kwa taratibu hizo. Katiba itakayoridhiwa na wengi itatusaidia katika hilo. Inawezekana.mjengwa

hs3.gif

Mjengwa wewe ni mtanzania kweli? unaangalia maendeleo ya mambo ya siasa Tanzania?
Haya yote unayosema yalishasemwa siku nyingi, tena yalielezwa vizuri kuliko unavyoeleza wewe. Jaribu kupitia ripoti ya tume ya Jaji Nyalali, jaribu kusoma ripoti ya tume ya Jaji Warioba, Jaribu kusoma ripoti ya ripoti ya jaji bomani(sina hakika), utaona kuwa yote haya yamekataliwa, na yaliyokubaliwa yamekubaliwa kwa kinyongo na kwa mbinde.

Tatizo lililopo hapa Tanzania ni kuwa CCM ni bora na ina maana zaidi kuliko Tanzania. Serikalini na CCM kuna watu wako tayari kuua na kufa kwa ajili ya CCM, lakini hakuna anayejali Tanzania. Hakuna asiyejua kuwa prural economy inahitaji prural politics, hakuna asiyejua kuwa Tanzania ni defacto one party state, na de jure multiparty, hilo sio tatizo. Tatizo ni kuwa tumeisahau Tanzania. Nyerere na Karume wamekufa na Tanzania yao.

Sasa hivi wenzetu visiwani wameanza kuwa na akili kidogo, wanaona Zanzibar ina maana zaidi kuliko CCM na CUF, sisi huku bado sana. Tuko radhi kuona kiongozi wa serikali anatembelea gari la fahari lakini tunachekelea kumuona mwanamke anayezaa mtanzania anajifungua kwa foleni tena sakafuni. Hakuna anayejali mali za taifa, hakauna anayewajali watanzania kwa moyo wote.

Sisi si watoto tunajua tatizo liko wapi, ndio maana watu wanajaribu kuleta mabadiliko ili mentality hiyo iondoke.
 
Akiri

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,446
1,250
ndugu maggid wasalaam.

Binafsi kwa ukweli kabisa katika idadi ya wasomaji wako ulinipoteza kabisa na sikuwa nakuelewa. makala hii niliiona kwenye gazeti lakini sikuisoma kwa kujua maggid yule yule ataandika yale yale ya ccm. leo nimesoma makala yako na nimejitahidi kuielewa na nimeielewa na kuipenda.

maggid nilikuwa nachukizwa na wewe kuto kuona mapungufu hayo uliyoyaandika na kuamua kuwa shabiki wa chama kinachotutesa kwa sela zake mbaya, kumbe mimi ndiyo nilikuwa sikuelewi na kwa hilo uniwie radhi.

nafurahi kujua kwamba tuko pamoja katika kuitakia mema nchi yetu kipenzi Tanzania leo nimekufahamu maggid kwa upya.
mambo uliyouyasema ni mwehu peke yake atakaye yapuuza

wasalaam
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom