Elections 2010 Matokeo ya Uchaguzi Hanang

Meale

Member
Nov 24, 2009
91
0
Habari zisizo rasmi kutoka katika vyanzo tofauti tofauti zinadai kwamba, mgombea ubunge kwa jimbo la Hanan'g Chadema ambaye pia alikuwa mke wa Dr. Slaa, Rose Kamili amembwaga mpinzani wake waziri Mary Nagu aliyekabidhiwa mikoba ya kuliongoza jimbo hilo na waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye.

Mwenye habari za uhakika zaidi atujulishe tafadhali.

Update: Tumewasiliana na mgombea ubunge wa Hanan'g Rose Kamili anasema kwamba Dr. Slaa anaongoza maeneo mengi jimboni mwake huku Chadema wakiongoza udiwani katika kata 12 kati ya kata 25. Kura za ubunge bado wanachuana vikali, kasema ni vigumu kusema nani kashinda mpaka sasa.
 
Mmmh, ya kweli haya? Tupe data basi!! Mbona hii ngoma ina mdundo wenye mvuto kiasi cha kushindwa kuelewa step za kuicheza?
 
Meale, kama huna data kaa kimya... unakera

sasa hivi ni bora mtu kulala tu, maana kila ukifikiria kuleta post ya kishabiki basi unabandika... nadhani kuna haja ya ban kwa wale wanaoleta habari bila ushahidi... we dont need mediocrity in serious business
 
napendekeza ni vema kusema mgombea fulani kapata kura hizi na yule hizi.. hizo ndo data.. ila pia ni vema kuwa makini... isije ikawa habari ni ya kituo kimoja au viwili then tunasema kashinda...
 
Meale, kama huna data kaa kimya... unakera

sasa hivi ni bora mtu kulala tu, maana kila ukifikiria kuleta post ya kishabiki basi unabandika... nadhani kuna haja ya ban kwa wale wanaoleta habari bila ushahidi... we dont need mediocrity in serious business

nimewapigia simu watu wanne tofauti kutoka Hanan'g wamenipa taarifa hizo zinazofanana.
 
Meale utanisamehe aisee.... facts sasa hivi ndo muhimu, tuweke ushabiki pembeni kidogo

unakumbuka ya buchosha na mbeya vijijini?
 
Meale utanisamehe aisee.... facts sasa hivi ndo muhimu, tuweke ushabiki pembeni kidogo

unakumbuka ya buchosha na mbeya vijijini?

Yeah, sijafanya ushabiki najua hatupo kwenye kampeni sasa, nikipata habari tofauti na hizo ambazo ni za uhakika zaidi nitawajulisha pia.
 
Back
Top Bottom