Meale
Member
- Nov 24, 2009
- 91
- 0
Habari zisizo rasmi kutoka katika vyanzo tofauti tofauti zinadai kwamba, mgombea ubunge kwa jimbo la Hanan'g Chadema ambaye pia alikuwa mke wa Dr. Slaa, Rose Kamili amembwaga mpinzani wake waziri Mary Nagu aliyekabidhiwa mikoba ya kuliongoza jimbo hilo na waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye.
Mwenye habari za uhakika zaidi atujulishe tafadhali.
Update: Tumewasiliana na mgombea ubunge wa Hanan'g Rose Kamili anasema kwamba Dr. Slaa anaongoza maeneo mengi jimboni mwake huku Chadema wakiongoza udiwani katika kata 12 kati ya kata 25. Kura za ubunge bado wanachuana vikali, kasema ni vigumu kusema nani kashinda mpaka sasa.