Matokeo ya Ubunge Kigoma Mjini yamechakachuliwa mchana kweupe!

Supervisor

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
559
207
Kigoma mambo bado kabisa hata kama jana matokeo ya Ubunge yalitangazwa kihuni na msimamizi wa uchaguzi muda wa saa 2 usiku baada ya askari kuwatawanya wafuasi wa Chadema kwa mabomu. Baada ya kukusanywa matokeo katika kata zote CCM walishindwa kwa zaidi ya kura 300 baada ya mvutano mrefu ccm wakalazimishwa kura zihesabiwe upya hapo ndo walipochakachua. Chadema wameyakataa matokeo na wanasema wanachukua hatua mpaka kieleweke. Pia chadema inaongoza kwa kuwa na madiwani wengi
 
Kama Chadema watalikosa jimbo la Kigoma mjini basi Zitto atakuwa ndio aliyeliuza; kwanini alikubali kuwa kura zihesabiwe mara ya pili wakati zilikwishahesabiwa mbele ya mawakala wote na mshindi wa Chadema kupatikana? CCm wanamchezo wa kutaka kura zihesabiwe upya pale tu wanaposhindwa na masanduku yakilala usiku wao huzichakachua kura halafu baada ya uhalifu wao siku ya pili wanaomba kura zihesabiwe upya!!Chadema msikubali kura kuhesabiwa mara mbili mbili hapo ndipo mtawathibiti hawa wezi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom