Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002!

viongozi karibu wote wa serikali wamehudhuria matokeo ya sensa ya watu na makazi. Lakini makamu wa kwanza hayupo, hii imekaaje?. Hausiki au yuko safari.

kabla ya kuuliza fanya kauchunguzi kadogo ujue yupo nchini au la!
 
Hongera JK kwa kuwezesha zoezi la sensa huku serikali ikigharimia 90% wakati wafadhaili 10%
 
Anaongea nini?

Ametoa shukrani kwa watu weengi,hakuna jipya.Waziri mkuu ameshaongea,nilichopata toka kwake ni kuwa watu wanne walikufa ktk utekelezaji wa majukumu yao.Sasa Mh Rais ndio yupo nyuma ya kipaza sauti,tutajulishana.
 
Tukio la UZINDUZI halina umuhimu wowote lakini Sensa yenyewe ina umuhimu katika kupanga mipango ya kimaendeleo.

kwahiyo anazindua sensa? au anazindua matokeo ya sensa? au anatangaza matokeo ya sensa?. nadhani moja ya majibu ya sensa ni kuwa mabubu wameongezeka.
 
Ivi kuna haja ya kuweka sherehe kutoa matokeo ya sensa? Mimi naona tunapoteza muda na gharama nyingi zinazoweza kuepukika.

mbaya zaidi sensa yenyewe iligomewa na baadhi ya watanzania hivyo matokeo ya idadi yatakuwa sio sahihi.
billion 140 inatumika kukamilisha ili zoeli ingawa makarani wengi waliaandamana kudai pesa zao.
 
Kama alilala nyumbani kwangu halafu mpewa taarifa alipewa majina na umri wa kwangu bado hao wahesabuji hawako makini, manake watakuwa ni wapumbavu kama inavyoashiria kwako
Mpewa taarifa hana kosa hapo, sasa kama ameambiwa hivyo ulitaka apate wapi uthibitisho mwingine? Usahihi wa taarifa unamtegemea zaidi mtoa taarifa, kama alisema kuna mwanaume alilala hapa, basi mpewa taarifa hana sababu ya kuleta ubishi! Pole sana, ila na wewe ukipata mnyonge mmegee wake!
 
Bravo JK kwa kumteua Hajjat Amina Saidi kwa vile ni mtaalam aliyebobea wa takwimu
 
Hadi sasa imetumika 124 bilioni katika utekelezaji wa sensa,taarifa za kina mfano wilaya fulani au kijiji fulani kuna watu kadhaa zitatolewa siku za usoni.
 
Kama tuko 50m basi wale Jamaa zangu wa......kataa kuhesabiwa tuwape ile 25m, wanaofuatia wako 15m na wale wa mwisho wako 10m. Tukate mzizi wa fitina!!
 
Hadi sasa imetumika 124 bilioni katika utekelezaji wa sensa,taarifa za kina mfano wilaya fulani au kijiji fulani kuna watu kadhaa zitatolewa siku za usoni.

pamoja na pesa iyo kutumika ikumbukwe kuwa kuna baadhi ya makarani walilipwa pesa ndogo kinyume na makubaliano.
 
Back
Top Bottom