Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Concrete, Dec 31, 2012.

 1. C

  Concrete JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,608
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar Rais Jakaya Kikwete atazindua matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi August, 2012.

  Nimeona nifike mwenyewe pasipo kupenda baada ya lengo langu la kupata huduma kwenye ofisi za umma leo kushindwa baada ya kutokukuta wahusika karibu wote kisa ni kwamba wameagizwa wote waende kuhudhuria tukio hili tena wamepewa na posho!!

  UPDATES
  *Tukio lilitakiwa lianze kufanyika toka saa mbili asubuhi lakini mpaka sasa(saa nne na nusu) rais hajafika japokuwa watu wameshafika, hakuna cha maana zaidi ya burudani nzito ya Muziki inayoporomoshwa kwa fujo(Kama Bonanza)

  *Rais ameshafika na tukio limeanza kwa mratibu wa sensa kitaifa na mwakilishi wa UNFDA kutoa hotuba fupi.

  *Waziri wa fedha Mgimwa, Balozi Seif Idd, Pinda nao wametoa hotuba za shukrani na mchakato wa sensa ulivyokwenda.

  *Rais sasa anaongea, anasema matokeo ya leo ya sensa ni ya awali(General) mengine yatatoka baadaye mwezi wa Pili mwakani(Details eg. Ratio of male and Female) kisha mwezi wa nne(At district level)

  Tanzania ina jumla ya watu 44,929,002!

  - Tanzania Bara 43,625,434
  - Zanzibar 1,303,568

   
 2. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Ni katika viwanja vya mnazimmoja. Mzee wa kaya yuko na "mtoto wa mkulima". Ni uzinduzi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012

  Kawasili na unapigwa wimbo wa taifa tayari kwa mzee wa kaya kuzindua matokeo ya sensa.

  Vilevile TBC wanarusha!!

  UPDATES TO COME!!!!!

  Hivi jamani sherehe hizi ni ulaji wa watu au nini? Si mkuu wa kaya angeita wanahabari na kutangaza tu tuko watanzania kadhaa basi!

  Matumizi ya vigogo wote waliokuja leo plus maandalizi, posho(sitting allowance), kulipa vikundi vya burudani, upambaji, nk.
   
 3. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,234
  Likes Received: 1,773
  Trophy Points: 280
  asante kwa kutukumbusha mkuu.ngoja tufuatilie
   
 4. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,872
  Likes Received: 1,747
  Trophy Points: 280
  tutajua ukweli tuh

  kama ni uchakachuaji ama la
   
 5. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pesa ni matumizi. Hayo ndiyo matumizi ya pesa. Hili ni tukio muhimu, na ni lazima ligharimu, kwani mlitaka mambo yafanyike bila gharama?????????
   
 6. B

  Baba mtata JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2012
  Joined: Dec 6, 2012
  Messages: 280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lina umuhmu gani?
   
 7. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,908
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mungu ibariki tanzania.kikwete amefanya mambo makubwa sana.. hili la sensa,kitambulisho cha uraia na katiba mpya...TUTAMKUMBUKA
   
 8. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,872
  Likes Received: 1,747
  Trophy Points: 280
  Is it possible for this country to be the middle income country by 2020??

  kwa ufisadi kama huu,ni maigizo tuh
   
 9. Daudi Safari

  Daudi Safari Verified User

  #9
  Dec 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Ngoja tusubirie sensa, mimi nakumbuka nilihesabiwa mara tatu kwenye vituo tofauti
   
 10. C

  Concrete JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,608
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Tukio la UZINDUZI halina umuhimu wowote lakini Sensa yenyewe ina umuhimu katika kupanga mipango ya kimaendeleo.
   
 11. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,234
  Likes Received: 1,773
  Trophy Points: 280
  uchakachuaji wa nini sasa? ukiwa na fikra hasi kwa kila kitu hatimae utakuwa ukiona vitu hasi kila wakati.
   
 12. K

  Keben JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2012
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Mtaani kwetu hatuku hesabiwa.
   
 13. M

  Mbogo Junior Senior Member

  #13
  Dec 31, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Viongozi karibu wote wa serikali wamehudhuria matokeo ya sensa ya watu na makazi. Lakini makamu wa kwanza hayupo, hii imekaaje?. Hausiki au yuko safari.
   
 14. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,574
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180
  Wewe si ndiyo wale mliokataa kuesabiwa.
   
 15. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,234
  Likes Received: 1,773
  Trophy Points: 280
  na kwanini ukakubali kuhesabiwa zaidi ya mara tatu?ninyi ndo kikwazo cha maendeleo ya nchi hii.wewe unadhani usipotoa taarifa kama ushahesabiwa,karani yeye angeota kwamba wewe tayari?yaani watu wengine bwana?
   
 16. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,234
  Likes Received: 1,773
  Trophy Points: 280
  na mengine kama kukuza demokrasia nchini ni miongoni mwa mabo mema aliyojitahidi kuyasimamia.
   
 17. Ngalangala

  Ngalangala JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Na huyo msoma utenzi kalipwa sitting allowance??
   
 18. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Matokeo yanzazinduliwa jamani kuna nini katika nchi hii! mie nilitegemea yatangazwe kama wanvofanya kwa matokeo ya mitihani sasa duuu!

  Na kama wanazindua watakaa siku ngapi hapo mnazi mmoja wakiendelea na maonyesho au uzinduaji kaaaaaaaaaazi kweli kweli!
   
 19. betlehem

  betlehem JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 7,234
  Likes Received: 1,773
  Trophy Points: 280
  hujaeleweka.
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  Dec 31, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,809
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Sisi wote tulikuwa kazini msichana wa kazi ndiye aliyetoa takwimu zote za watu 7 wa familia yangu
   
Loading...