Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,469
- 728

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kina mpango wa kukata kiu ya waliomisi uwepo wa Dk. Willibrod Slaa bungeni kwa kumuingiza kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika wakati wowote.
CHADEMA, kinajipanga zaidi kumuingiza Slaa bungeni kupitia Jimbo la Hanang ambalo tayari kimekwishawasilisha pingamizi mahakamani kutaka matokeo yaliyomtangaza Mary Nagu (CCM) mshindi yabatilishwe.
Habari za uhakika zinasema kuwa endapo mahakama itabatilisha uchaguzi wa Hanang, Slaa atagombea katika uchaguzi mdogo na kuna uhakika wa asilimia mia moja kwamba atashinda.
Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA alilikaririwa akisema mjini Dodoma hivi karibuni kuwa aliyegombea Hanang, Rose Kamili tayari ni Mbunge Viti Maalum, kwahiyo Slaa anaweza kugombea na kushinda.
Nafasi ni kama hizo, kuna uchaguzi mdogo unakuja, Slaa akigombea sehemu yoyote atashinda, alisema Mbunge wa ubungo mheshimiwa John Mnyika