Matokeo ya mitihani ya NECTA: Kupima ubora wa ufaulu : Shule binafsi zisichanganywe na za serikali

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,017
3,656
Nimeangalia matokeo ya sekondari kwa miaka mitatu mfulilizo nikagundua yafuatayo
1. Shule bora (zenye matokeo mazuri) ambazo huongoza kitaifa ni shule binafsi.
2. Wanafunzi bora kitaifa pia hutokea katika shule hizo hizo binafsi.
3. Pengine na waalimu bora wapo mkondo huohuo.
Hii ina maana kwa shule za serikali ni vigumu kujua shule bora ni zipi katika mazingira yaliyopo. Kwa nini kusiwe na fair grounds katika ushindani kwa kuweka makundi angalau mawili ? Nikiwa na maana shule binafsi zichuane kivyake,vivyo hivyo na kwa zile za serikali? Kwa kufanya vile huenda ikawapa ari zaidi shule na waalimu upande wa shule za serikali.
 
Mnaanza kuwaza namna ya kupanua magoli ili mfiche aibu inayowakumba kila mwaka.Hata ukikusanya mazezeta yote,ukifanya mchujo bado utapata zezeta wa kwanza na wa mwisho,sasa ukipata zezeta wa kwanza utamsifu kuwa yeye ni "jiniaz?"

Ubora wa kitu hupimwa kwa kukilinganisha na vitu bora na si dhaifu,acha washindanishwe wote ili aliye bora awe bora toka miongoni mwa walio bora,tunataka uhalisia na si maigizo.

Mmezoea kuchakachua kura za wananchi na kujitangaza mmeshinda kwa kishindo,sasa mnataka mjitafutie sifa kuwa mmefaulisha kwa kishindo kumbe ni hadaa tupu?
 
Kwa hiyo na mitaala itofautishwe?? Enbu wacha hivo hivo ili wahusika waone dhambi hii wanayowafanyia watz wanyonge itakavyowatafuna mbinguni
Sina maana mitaala itofautishwe. Chukulia mfano wa mashindano ya mpira wa miguu. Timu hupangwa kwa madaraja na hushindanishwa kwa madaraja hayo hayo,ambapo sheria za mpira hutumika zilezile kwa madaraja yote. Mfano EPL,First League n.k. Haiwezekani Shule za Kata tunazozijua ,ulinganishe na kama zile aina ya Feza Boys then uje ulaumu waalimu wa Shule za Kata hawafanyi kazi! Kwa nini usibuni njia fair ya ushindani ili unapotaka kulaumu wote turidhike!
 
Mnaanza kuwaza namna ya kupanua magoli ili mfiche aibu inayowakumba kila mwaka.Hata ukikusanya mazezeta yote,ukifanya mchujo bado utapata zezeta wa kwanza na wa mwisho,sasa ukipata zezeta wa kwanza utamsifu kuwa yeye ni "jiniaz?"

Ubora wa kitu hupimwa kwa kukilinganisha na vitu bora na si dhaifu,acha washindanishwe wote ili aliye bora awe bora toka miongoni mwa walio bora,tunataka uhalisia na si maigizo.

Mmezoea kuchakachua kura za wananchi na kujitangaza mmeshinda kwa kishindo,sasa mnataka mjitafutie sifa kuwa mmefaulisha kwa kishindo kumbe ni hadaa tupu?
Naomba ujaribu kuielewa hoja yangu na hali halisi ya shule zetu. Kwa nini unaoita "jiniazi" na "mazezeta" hutoka aina ya shule zile zile kila mwaka?
 
Nimeangalia matokeo ya sekondari kwa miaka mitatu mfulilizo nikagundua yafuatayo
1. Shule bora (zenye matokeo mazuri) ambazo huongoza kitaifa ni shule binafsi.
2. Wanafunzi bora kitaifa pia hutokea katika shule hizo hizo binafsi.
3. Pengine na waalimu bora wapo mkondo huohuo.
Hii ina maana kwa shule za serikali ni vigumu kujua shule bora ni zipi katika mazingira yaliyopo. Kwa nini kusiwe na fair grounds katika ushindani kwa kuweka makundi angalau mawili ? Nikiwa na maana shule binafsi zichuane kivyake,vivyo hivyo na kwa zile za serikali? Kwa kufanya vile huenda ikawapa ari zaidi shule na waalimu upande wa shule za serikali.
Shule binafsi na za serikali wanafabya mitigani ile ile. Sasa kwanini watofautishwe? Hata kama ukisema zitofautishwe bado hata hizo za binafsi zinatofautiana maana nyingine nazo si nzuri zinazidiwa na za serikali.
 
Hahahaha daah watanzania bhana. Zamani ilboru, mzumbe, kibaha, kilakala, etc zlvyokua znaongoza si wangekua wanaztenga pia na za private?
Sasa sahivi private znaongoza imekua shida?
Na haitaishia hapo na baadae mtasema na shule za kata matokeo yatoke kivyake....
Ishu ni kuboresha elimu kwenye shule za serikali, hamna miujiza mingine.
Nukta.
 
Naomba ujaribu kuielewa hoja yangu na hali halisi ya shule zetu. Kwa nini unaoita "jiniazi" na "mazezeta" hutoka aina ya shule zile zile kila mwaka?

Wanatoka Shule zilezile kila mwaka kwa sababu ya kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaaluma,tunapeleka sekondari wanafunzi wasio na sifa,tunaona fahari kulihamisha darasa zima toka Shule ya msingi na kulipeleka sekondari huku tukijuwa fika kuna watoto ambao hawakustahiri kuwa hapo.

Wakati Shule binafsi zikitilia mkazo Mitihani ya kutathmini uwezo wa wanafunzi na kuamua ni nani anayestahiri kupanda ngazi toka darasa moja hadi jingine,serikali inaleta sanaa kwenye jambo hilo la muhimu hadi kupelekea kuingilia kati na kujaribu kuwazuia wenye Shule binafsi wasifanye hivyo.

Aina ya Mitihani inayotumiwa kutahini watoto haiwajengei watoto uwezo wa kufikiri,haiwezekani mtoto wa darasa la VII Mitihani yake yote iwe ya kuchagua,tunauwa uwezo wa watoto wetu na kuwafanya wawe mabingwa wa "kubet majibu" badala ya kutumia akili kukokotoa majibu.

Tumepiga marufuku masomo ya ziada mashuleni kwa kigezo cha Elimu bure,wakati Shule binafsi kila uchwao wana Mitihani ya tathmini ili kuwawezesha kufahamu uelewa wa wanafunzi wao na kujipanga kuwasaidia.Hizo na nyingine nyingi ndiyo sababu za Shule zetu kufanya vibaya.
 
Shule inakuwa ya kwanza kitaifa idadi ya wanafunzi 50 wote wanapata div one shule kama mzumbe wana div zaidi ya 75 two 30 sasa vipi unailinganisha na wenye idadi ndogo
 
Huo sio ushindani...

Basi kama ni hivyo na mitihani watungiwe tofauti..na mitahala iwe tofauti
 
Shule inakuwa ya kwanza kitaifa idadi ya wanafunzi 50 wote wanapata div one shule kama mzumbe wana div zaidi ya 75 two 30 sasa vipi unailinganisha na wenye idadi ndogo
Hujaona Marian schools wanafunzi 160... Div 1 ni 120...?
 
Shule inakuwa ya kwanza kitaifa idadi ya wanafunzi 50 wote wanapata div one shule kama mzumbe wana div zaidi ya 75 two 30 sasa vipi unailinganisha na wenye idadi ndogo
Kwa maana yako hii na kama nimekuelewa tukubaliane vigezo vya ushindanishi wa ufaulu vibadilishwe.
 
Sina maana mitaala itofautishwe. Chukulia mfano wa mashindano ya mpira wa miguu. Timu hupangwa kwa madaraja na hushindanishwa kwa madaraja hayo hayo,ambapo sheria za mpira hutumika zilezile kwa madaraja yote. Mfano EPL,First League n.k. Haiwezekani Shule za Kata tunazozijua ,ulinganishe na kama zile aina ya Feza Boys then uje ulaumu waalimu wa Shule za Kata hawafanyi kazi! Kwa nini usibuni njia fair ya ushindani ili unapotaka kulaumu wote turidhike!
Watu wengi wana uelewa potofu kuwa shule za private kinachowafanya wanafunzi wafanye vizuri ni walimu na madarasa mazuri. Wanasahau kuwa shule hizo kwanza huchagua wanafunzi wale wazuri kabisa kujiunga na shuke zao.

Kuna wakati nilenda St. Marian kumpeleka mtoto kwaajili ya mtihani wa kujiunga na hiyo shule. Wanafunzi waliokuwepo pale wangechukuliwa wote, basi kungeweza kupatikana hata mikondo 8. Na hao wote walioenda kufanya mtihani walikuwa na matumaini kuwa wangechaguliwa kwa sababu walikuwa wanafanya vizuri kwenye shuke walizotoka lakini walichaguliwa wa kutengeneza mikondo miwili tu. Hao waliotengeneza mikondo miwili ina maana ni the best of the best.

Walimu wanapata urahisi hata katika ufundishaji katika shule hizi kwa sababu wanafunzi wenyewe huwa tayari ni wanafunzi wenye uwezo kimasomo. Hata wazazi wenyewe huwapeleka watoto wao private schòls wale wanaoona wana uwezo kimasomo.

Mazingira yaamebadilika. Zamani wanafunzi wenye uwezo kimasomo walienda government schools, na wale wenye uwezo mdogo walienda private schools. Leo hii watoto wenye uwezo mkubwa kimasomo wanaenda private schools. Ni pale ambapo mzazi hana uwezo wa kuzifikia gharama ndipo humpeleka mtoto wake mwenye uwezo mzuri kimasomo kwenye shuke za serikali. Wazazi wanakuwa na mashaka kuwa watoto wao wenye uwezo kimasomo wakienda government schools, wanaweza kuua vipaji na uwezo wao ambao unastahili kupaliliwa na kuendelezwa.
 
Mnaanza kuwaza namna ya kupanua magoli ili mfiche aibu inayowakumba kila mwaka.Hata ukikusanya mazezeta yote,ukifanya mchujo bado utapata zezeta wa kwanza na wa mwisho,sasa ukipata zezeta wa kwanza utamsifu kuwa yeye ni "jiniaz?"

Ubora wa kitu hupimwa kwa kukilinganisha na vitu bora na si dhaifu,acha washindanishwe wote ili aliye bora awe bora toka miongoni mwa walio bora,tunataka uhalisia na si maigizo.

Mmezoea kuchakachua kura za wananchi na kujitangaza mmeshinda kwa kishindo,sasa mnataka mjitafutie sifa kuwa mmefaulisha kwa kishindo kumbe ni hadaa tupu?
duuh mkuu umeongea kwa hisia sana

Watu wengi wana uelewa potofu kuwa shule za private kinachowafanya wanafunzi wafanye vizuri ni walimu na madarasa mazuri. Wanasahau kuwa shule hizo kwanza huchagua wanafunzi wale wazuri kabisa kujiunga na shuke zao.

Mazingira yaamebadilika. Zamani wanafunzi wenye uwezo kimasomo walienda government schools, na wale wenye uwezo mdogo walienda private schools. Leo hii watoto wenye uwezo mkubwa kimasomo wanaenda private schools. Ni pale ambapo mzazi hana uwezo wa kuzifikia gharama ndipo humpeleka mtoto wake mwenye uwezo mzuri kimasomo kwenye shuke za serikali. Wazazi wanakuwa na mashaka kuwa watoto wao wenye uwezo kimasomo wakienda government schools, wanaweza kuua vipaji na uwezo wao ambao unastahili kupaliliwa na kuendelezwa.
Nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom