MATOKEO YA MITIHANI YA KITAIFA SOMO LA LUGHA YA KIINGEREZA.

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Mar 25, 2012
462
343
Wanajamvi,awali ya yote tumshukuru muumba kwa yote hasa nyakati hizi za dhiki kuu.Nimekaa,nimetafakari na nikahitimisha kwa kujihoji mambo kadhaa ambayo yamo katika 'mwenendo wa somo la Lugha ya Kiingereza' hasa katika ngazi ya msingi na sekondari.Kwa kadri ya uzoefu wangu(kama mwalimu na mtaalamu wa masuala ya elimu) somo la Lugha ya kiingereza linakabiliwa na changamoto kubwa hasa kwa upande wa 'walimu wa somo la Lugha ya Kiingereza).Pana raslimali watu chache sana 'iliyoajiriwa na Serekali' ili kusimamia,kuongoza na kuratibu ufundishaji wa somo la lugha ya kiingereza.Kama mnavyofahamu,somo la Lugha ya Kiingereza ndilo somo 'mtambuka' linaloingiliana na masomo mengine hasa 'sekondari'.Ubovu wowote katika somo hili unapelekea 'kudhorota' kwa masomo yote yanayolitegemea.Matokeo ya kitaifa yamendelea kuonesha kwa kudhihirisha 'ufaulu duni' katika somo hilo na hivyo kupelekea ufaulu duni katika masomo mengine.Kwa kadri ya uzoefu wangu,mwanafunzi anaye-feli somo la Lugha ya Kiingereza huwa anafeli pia masomo mengine yanayotegemea Lugha ya Kiingereza katika uwasilishwaji wake.Kwa bahati mbaya sana,viongozi wetu wamekuwa wakiona kufeli huko kwa wanafunzi katika masomo mengine hasa 'Sayansi' kunasababishwa na upungufu wa walimu wa masomo hayo tu bila kutazama kwa kina juu ya msingi wa mawasiliano hasa 'Somo la Lugha ya Kiingereza' ambalo ndilo kiungo kikuu.Tukumbuke kuwa,msingi wa masiliano ni Lugha.Bila Lugha hakuna mawasiliano na kwa hivyo hakuna kuelewana.Niseme tu kwamba moja kati ya watu wenye 'tatizo la Lugha ya Kiingereza' ni walimu wa masomo ya 'Sayansi'.Hili halina ubishi.Kiingereza kibovu kiko kwa hawa watu hasa huko sekondari 'zetu'.Kutokana kukosekana kwa msingi wa Lugha ya uwasilishwaji wa masomo ndiyo maana hata ufahamu juu ya masomo yanayoitwa 'nyanga' au 'mawe' umekuwa duni kuliko duni yenyewe.Iwapo viongozi wetu wanahitaji kusaidia taaluma ya 'watoto wa mama n'tilie' hawana budi kujisahihisha na kutoa 'AJIRA KWA WALIMU WA SOMO LA LUGHA YA KIINGEREZA ' na siyo kuajiri walimu wa Sayansi pekee ambao nao ni 'chanzo cha tatizo'.Waache kuwatenga walimu wa ENGLISH LANGUAGE wenye shahada,stahahada na astashahada.Walimu hawa ni wachache mno kuliko hata walivyo wa Mathematics,biology,chemistry na physics.Wametumia muda wao,nguvu,akili na raslimali fedha kuwekeza kwenye hili somo ili siku moja 'wawatumikie' watanzania.Nitoe rai kwa wahitimu wa fani ya ualimu hasa Somo la Lugha ya Kiingereza kupaza sauti na kujenga hoja juu ya mstakabari wa somo hili kwa kushawishi AJIRA zipatikane ili kunusuru hali ya somo na hali zetu pia.Serikali ikisikie kilio hiki japo kipo kwenye 'maji' na kwa lengo zuri la kuinua taaluma.Wahitimu wa somo hili tangu mwaka 2015 hadi sasa 2018 hakuna aliyeajiriwa wala serekali kutangaza nafasi za ajira kwa walimu wa somo hili ukiachilia mbali wale wanaopangiwa bila nafasi hizo kutangazwa 'wazi kwa kila mtu' na hili linauma sana hasa kama wewe ni mhitimu wa fani hii.Hii inatupatia taswira kuwa tumefikia hatua ya 'kubaguana na kupeana ajira kwa kujuana' na kama taifa si jambo jema.Washairi katika "Diwani ya Chekacheka" katika shairi la KUNANINI HUKO NDANI wanatuasa kugawana japo kidogo kilichopo.'Wanyonge Mmetuangusha.SAYANSI BILA KIINGEREZA NI SAWA NA TUNGULI BILA MITISHAMBA.Ahsanteni sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom