Matokeo ya mitihani darasa la saba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya mitihani darasa la saba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Feb 21, 2010.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,788
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  [FONT=Times,Times New Roman][SIZE=+3]Matokeo ya mitihani darasa la saba serikali ieleze:[/SIZE][/FONT]


  [FONT=Times,Times New Roman][SIZE=+4]Je, Waislamu ni taahira au kuna agenda ya siri[/SIZE][/FONT]
  • [FONT=Times,Times New Roman][SIZE=+2]Waliotahiniwa Waislamu 71% Wakristo 29%[/SIZE][/FONT]
  • [FONT=Times,Times New Roman][SIZE=+2]Waliochaguliwa Waislamu 21% Wakristo 79%[/SIZE][/FONT]
  SERIKALI ilitakiwa ieleze ni sababu zipi zinazopelekea watoto wa Kiislamu wanaochaguliwa kwenda kidato cha kwanza wawe wachache sana ikilinganishwa na idadi ya watahiniwa.

  Akizungumza Bungeni Februari 2, 1999 Mbunge wa Kigamboni Mh. Kitwana Kondo alisema kwamba kwa mwaka 1998 watoto Waislamu waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoa wa Dar es Salaam walikuwa asilimia sabini na moja (71%) wakati Wakristo walikuwa 29% ya watahiniwa wote.

  Hata hivyo, akasema kwamba waliokuja kuchaguliwa kwenda
  sekondari Waislamu walikuwa asilimia ishirini na moja (21%) wakati Wakristo waliochaguliwa walikuwa asilimia sabini na tisa (79%).

  Kutokana na kielelezo hicho, Mh. Kitwana Kondo alihoji: "ama Waislamu ni wajinga, ama akili zao hazifanyi kazi " ama mtu akiwa Muislamu basi wewe huna kitu au kuna kitu". Kwa hiyo, akaitaka serikali itoe maelezo.

  Katika utangulizi wake, akiielezea nukta hii Mh. Kitwana Kondo alikariri ahadi ya Mh. Rais ya kuyashughulikia matatizo ya kielimu ya Waislamu ambapo pia alishauri wafadhili wajenge shule zaidi badala ya Misikiti, lakini akamtaka Waziri wa Elimu atoe ufafanuzi juu ya jambo hili.

  Kwamba je, watoto wa Kiislamu kutochaguliwa kwenda kidato cha kwanza ni kwamba Waislamu kwa asili yao wanazaliwa wajinga au zipo juhudi za kuwakandamiza.

  Wakati huo huo, Mh. Kitwana Kondo ameliambia Bunge kwamba yapo mambo ambayo yanapangwa na serikali ambayo yanaweza kuleta mfarakano katika jamii yetu, jambo ambalo Mh. Rais amelikemea.

  Akitoa vielelezo alitaja suala la siku ya Ijumaa ambapo katika baadhi ya maofisi na mashule ratiba za kazi hazizingatii haki ya Waislamu kwenda kuswali.

  Ameiomba serikali itoe agizo kwamba shughuli zote za kazi na masomo zisimame saa sita na kama ni kuendelea ziendelee baada ya saa nane.

  Mfano mwingine aliotoa Mh. Kondo ni tabia ya serikali kuchelewesha usajili wa taasisi za Kiislamu bila sababu zozote za msingi. Alieleza kwamba taasisi moja ya Kiislamu ijulikanayo kama Baraza la Maimamu toka iombe kusajiliwa ni miaka mitatu bado haijasajiliwa.

  Aidha, alisema kwamba wakati mwingine Waislamu hudaiwa walete kibali cha Bakwata wanapoomba kusajiliwa, akahoji je, hiyo ni sheria ya serikali au matakwa tu ya wakubwa.

  Suala lingine aliloligusia kama kielelezo cha Waislamu kutokutendewa haki na hivyo kuhatarisha amani ya nchi, ni tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali na hasa katika taasisi za elimu kuwazuia mabinti Waislamu kuvaa hijab. Amesema hiyo ni amri ya Qur’an (33:30-31)na ni lazima iheshimiwe.

  Akizungumzia suala la mitihani ya kidato cha nne kufanyika mwezi wa Ramadhani, Mh. Kitwana Kondo alisema kwamba hiyo ni moja ya chehe za kuleta mfarakano. Hata hivyo akasema kwamba baada ya manung’uniko Waziri wa Elimu alitoa maelezo ambayo yaliwaridhisha Waislamu.

  Hata hivyo, akashangazwa na kuhoji dhamira ya wale wakubwa waliosema kwa jeuri na takabari kwamba watoto wa Kiislamu wakitaka kufanya mtihani wafanye na wasipotaka basi. Hakufafanua ni mkubwa gani huyo.

  Mh. Kitwana Kondo alisisitiza kwamba hao wasiojali hisia za Waislamu na wanaotoa kauli hizo za jeuri ndio wasio itakia kheri nchi yetu.

  Ila kwa upande wake na wengine wanaokuja na kusema hadharani ndio waitakiao mema nchi.

  Aliwaomba viongozi wa serikali na hasa Mawaziri kumsaidia Mh. Rais kutekeleza dhamira na ahadi yake ya kuyashughulikia malalamiko ya Waislamu. Mh. Kitwana Kondo alipata fursa ya kuyasema yote hayo katika kipindi cha kujadili hotuba ya Mh. Rais Mkapa aliyoitoa Bungeni mwaka jana.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,427
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Nyie best tatizo lenu mnachanganya mambo, mara nyingi kama siyo zote mnang'ang'ania madras. Siyo mbaya madras ila wenzenu wanakwenda kudiscuss au pengine tuition (ingawa i don't recommend) nyie mwakazana na JU ZUU zinazowaletea utaahira. Fuateni sylabus muone kama hamtakamua kwanI hapa university nnakosomea tunao watoto wa kiislamu wanakamua kipindi dunia nzima. Nyie mnakazana kusema elimu dunia ni batir unadhani wataacha kufeli? Suala kubwa hapa ni scale of preference. Ukicheki mashule ya wakristo kimatokeo ukiondoa shule za mama Lwakatare (labda kwa kiingereza) wanafauru na ukicheki Islamic seminaries wanavuta mkia tu. So angalieni mnafundisha nini manake ukienda kufanya Necta huwezi ulizwa namna ya kujilipua. Pia angalieni waalimu wenu kama wamequlify, ikiajili mtu kwa kuwa anaswali mara tano kwa siku hata kama ni muuza vitumbua hana profession ya uticha unatugemea nini? Au ni mke wa shekhe hana elimu unadhani atafundisha nini?
   
 3. K

  KGM Senior Member

  #3
  Feb 21, 2010
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  HAWA NAOO. kwani mtume MUD yeye alikuwa na elimu gani wakati hata kusoma alikuwa hajui. KUTOKUWA NA ELIMU KWA MWISLMU NI sunnah SHEKH wewe hujui???????////
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,427
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Kama kazi wasubiri ya upendeleo maalum!
   
 5. K

  KGM Senior Member

  #5
  Feb 21, 2010
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  we acha tu, yaani hawa jamaa wanakera sana. Wanaichafua dunia kila mahala walipo wao ni malalamiko tu. Mimi sasa hivi nafikri dawa ni kutokuwa na suluhu nao, vinginevyo tutaumia sana. Unaona hata vitu vya umma kama chuo cha tenesco waliprwa kwa kuendekeza ujinga wao
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,316
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mimi naamini kuwa mafanikio katika elimu yanaanzia nyumbani. Vijana wote wa kikristo na kiislamu wanauwezo unaofanana kabisa. Ni jambo rahisi tu jamii kuahmua kuwa zinataka kujenga familia za aina gani. Bahati mbaya ni kuwa watoto wakiwa wadogo hawana nafasi ya kujihamulia, na hapa ndipo ninapozungumzia nafasi ya wazazi, kabla ya kumwangalia mwalimu na serikali. Vijana wengi wanapofikia umri wa kujihamulia wanajikuta nafasi ndiyo hiyo ishayoyoma na kubakia na nyoya za mkiani!
   
 7. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumia mda mwingi kufikiri namna ya kubadili hizo figure, hata ukiweza waislam waliofanya mtihani 80% waliochaguliwa 80%. Kulalamika ni dalili za inferiority, Na kwa wale wanamahesabu wazuri, Waislamu 71% Wakristo 29%
  Waliochaguliwa Waislamu 21% Wakristo 79%. ili kubalance idadi sawa ya wanafunzi wanaoenda elimu ya sekondari kati ya Waislamu na Wakristo, nadhani hayo na makadirio sahihi kabisa.
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Waisilamu wanamatatizo ya kisaikolojia!
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mahmoud,
  Waislamu waliotahiniwa inawezekana ni 71% na waKristo 21% lakini huu ni uwiano wa walio TAHINIWA tu, kutahiniwa si lazima matokeo yake yawe kufaulu.

  Hizi takwimu zako chanzo ni kipi? Kwa sababu sidhani kama wakati wa kutahiniwa watoto wanaulizwa dini yao. Au kunatakwimu za maoanisho kati ya matokeo ya mtihani na taarifa za mtoto wakati alipoandikishwa shule?
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,734
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Umenena Nono tatizo la watoto wengi wa kiislamu (si wote) ni kuwa wazazi wao wenyewe hawana au elimu yao ni ndogo. Watoto hawana guidance au support nyumbani. Kama hawabaguliwi katika kuandikishwa mashuleni watabaguliwaje katika matokeo ya mtihani? Wazushi tu.
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hii. Na ndo maana kule Nigeria mwaka jana walifanya maandamano kupinga elimu dunia waliyoiita elimu ya magharibi na kutaka shule yao iwe ni madrasa tu. Sasa unategemea nini hapo? Lakini yote haya ni kutokana na mwanzilishi wa dini mwenyewe hakujua kusoma wala kuandika sasa unategemea wafuasi watakuwaje?
   
 12. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  Naona unavuka mipaka, ndugu zetu hawana uvumilivu na uwezo wa kujenga hoja. Mi sichangii hapa, nisije chomewa kibanda changu bure!!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...