Matokeo ya Law school of Tanzania, kati ya wanafunzi 500+ walio-clear masomo yote ni 22 tuu!

Kuna wakati haya mambo hutokea, inawezekana kuna makosa ya ufundishwaji, ysahihishaji au uelewa wa wanafunzi ktk somo fulani au kuna somo limekazwa ziadi. Hii naifananisha na habari niliyopewa mwaka jana pale udsm kuwa wanafunzi zaidi ya 600 walisap CL. Swali la kwanza kuuliza linafundishwa na nani ! Nikajibiwa Kadeghe karudi baada ya kutolewa ktk ukuu wa wilaya ya Songwe. Nikapata moja ya jibu kuwa huyo si mtu mzuri.
 
Walimu wanafanya elimu ionekane ngumu Tanzania halafu hakuna matokeo chanya ya elimu husika
 
madogo someni acheni kujambajamba mitandaoni/

we umetoka itilima unakuja Dar unaanza oh mliman city mara sjui beach mara sjui madem wa sinza=

Tena walimu wenu wawajibishwe kwa kuachia hiyo idadi,vïĺaza mno bora waliosoma IJA
 
Jamani matokeo yametoka, kati ya wanafunzi 500+ walio clear masomo yote ni 22!
Hapa kuna tatizo nasi weak students kama mtu anavyoweza kudhani. Kuna tatizo katika teaching and examining/exam set up!.
Yani hao 22 ni first sitting ama pamoja na wa supp??
 
Wewe userious wa mtu kimasomo unaupima kwa macho au unakipimo gani had useme hawako serious? Ama unadhan kukaa karibu na mahakama ndo kujua sheria?
Jamaa kaongea ukweli wewe how comes unadisco bana yani masomo matano yote core unapata F hapo kuna mawili kama sio kilaza basi hauko serious!
 
Havard school of law ni ya kawaida sanaa na hata ukifaulu pale hauwii kitu, kwa marekani ili uwe advocate lazima ufanye mitihani ya Legal Bars ambayo ufaulu wake ni mdogo sanaaa hata mawaziri kibao walishafeli, na kubwa kuliko yote kwao ni ile New York Legal Bars Examination hadi mtoto wa J.Kennedy aliwai kudunda mara zote alizofanya...
Bora umemuelekeza huyo haelewi kitu....
Hakuna mtihani unaogopewa ktk fani ya sheria America kama Bar Exams.....
Namshauri akacheki movies hizi My Cousin Vinny, The Rainmaker na hii series ya Suits halafu ataelewa namaanisha nini
 
Nop, wakifanya supplimentary wanaweza toka japo si wote. Fursa kwa degree holder ya law ni nyingi itategemea na mtu mwenyewe anapendelea wapi
Acha kudanganya wewe unaonekana umedisco law school...sasa hivi degree ya law haina ishu tena ni kama kuishia form 4 utafanya kazi gani sasa ama kubebea watu mafaili yao unaona nayo kazi??
Kwa mtu anayesoma law....kama huna muhuri na cheti cha law school achana na hiyo fani unajipotezea muda...
Cheti kitakufanya uwe state attorney/RM
Muhuri utakua kwenye private practice..
Sasa niambie iyo degree utaitumia kwenye fursa gani??????
 
Kikubwa hapa ni mfumo wa kikoloni unaotutesa sikuzote kama umepita pale utajua siri iliyopo lakini kama hujafika ni kweli unaweza ukadhani wanafunzi ni vilaza cha muhimu lazima wajitolee wahanga kadhaa na kutengeneza hoja ili kusaidia kizazi hiki na kijacho kwani kuna zaidi ya ukoloni pale LST na inawezekana wenye mamlaka hawajui au wanalindana.
 
me huwa sielewi
hivi law huwa ni ngumu sana au wanafunzi ndio Vilaza?
Wanafunzi ndo vilaza Mkuu ndo mana unaona mabush lawyer wengi mtaani wengi wanaingia kwenye iyo fani wakiamini kuna ina hela sana ndo lakini wanasahau ni fani inayohitaji competency ya hali ya juu otherwise utaonekana kituko....
 
Ndiyo maana nasema kuna tatizo na ufundishaji na utungaji mitihani. These so called professors wanataka kuifanya fani ya uwakili kuwa "eti" ngumu! Wapuuzi wakubwa. Haiwezekani watoto wote wakafeli, tatizo liko kwao walimu! We have to raise alarm!
Mkuu yawezekana kuna tatizo mahali ila sio kubwa kushinda ile fact kua tatizo kubwa lipo kwa wanafanzi....we inawezekana ukapata F katika masomo core 5 ambapo ndo unadisco...ina mana una F kumi na tano...nakataa tatizo sio la walimu hapo
 
Back
Top Bottom