Matokeo ya kupangwa kwenye chaguzi yameondoa ari ya kujiandikisha

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Mashindano yoyote huleta msisimko kama kuna ushindani na washindani wenye kushindana kwa kwa vigezo huku masharti yakizingatiwa....
Matokeo ya kupangwa hupunguza mumkari na kuondoa msisimko wa shindano lolote... Upendeleo, mabavu, uonevu na rafu huku kukiwa na upendeleo wa wazi huwafanya washiriki, wapambe wao, wafuasi na mashabiki wa kawaida kuona kwamba hakuna maana ya kushiriki tena kama mashindano Kama hayo yakitokea....
Uchaguzi wetu wa serikali za mitaa umekosa msisimko kabisa kutokana na sababu tajwa hapo juu... Uandikishaji wa wapiga kura ni mbovu na wa kiwango cha chini
Watu wanaona hakuna haja ya kujiandikisha kwakuwa hata kama watapiga kura... Matokeo yanajulikana... Kila mtu anapotezea sasa....
Matangazo ya kuhamasisha uandikishaji haupaswi kuwa na viashiria vya upande fulani... Tunazidi kufeli...
IMG-20191013-WA0064.jpeg
 
Mkuu alisema "mkurugenzi nimekupa gari, nyumba,mshahara na mambo mengne kibao alaf Leo unitangazie mpinzani kashinda Haiwezekani" hapo uchaguzi hakuna watu wameshapangwa
 
Mkuu alisema "mkurugenzi nimekupa gari, nyumba,mshahara na mambo mengne kibao alaf Leo unitangazie mpinzani kashinda Haiwezekani" hapo uchaguzi hakuna watu wameshapangwa
Na kale kapumbavu kakuu ka wilaya moji hivi mamake kamesema ole wake atakayemtangaza mpinzani hata kama ameshinda! Nchi hii imejaa majitu mapumbavuuuu!!
 
Mkuu wa wilaya gani, weka wazi mkuu watu wajiandae kisaikolojia.

Kuna mkuu wa wilaya moja mkoa wa Dodoma ana domo kama bakuli huku meno yakiwa yameoza! Eti anasimama hadharani kusema wapinzani hata wakishinda wasitangazwe! Ujinga kabisa huo! Enzi hizi walitakiwa akina Mwamwindi kila wilaya ili mtu akiongea ujinga tu anafyatuliwa!
 
Kuna mkuu wa wilaya moja mkoa wa Dodoma ana domo kama bakuli huku meno yakiwa yameoza! Eti anasimama hadharani kusema wapinzani hata wakishinda wasitangazwe! Ujinga kabisa huo! Enzi hizi walitakiwa akina Mwamwindi kila wilaya ili mtu akiongea uinga tu anafyatuliwa!
Mkuu muweke hapa tumpe sure
 
KWA NINI WANANCHI HAWATAKI KUJIANDIKISHA?

Na Thadei Ole Mushi.

Mawazo yangu binafsi!!

Mwaka Jana mwezi wa kumi Katibu mkuu ccm Dr Bashiru alilalamika wapiga kura kupungua kwenye chaguzi za marudio, Dr Bashiru alinukuliwa akisema wapiga kura wanaojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia Hamsini ya waliojiandikisha.

Namuona Mh Jafo naye akiingia kwenye issue ile ile kuwa zoezi la kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nao unasua sua. Hapa ndipo watafiti wanapotakiwa kufanya utafiti kwa nn wananchi hawataki kushiriki uchaguzi?

Ninapredict factor NNE hapa.

1.Chaguzi za marudio za mradi wa jiuzulu, unga mkono, gombea tena, shinda kwa lazima ni factor mojawapo ya wananchi kuchoshwa na chaguzi. Wananchi wa naona hata wakipiga kura kuna watu wapo mahali wanamatokeo yao tayari.

2. Hakuna Elimu iliyotolewa ya kutosha kati ya uandikishaji wa daftri la kudumu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2020 na daftari hili la ukaazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Zoezi lilianza kabla ya Elimu hii ya kutofautisha kutolewa.

3. Mikutano ya vyama vya siasa kuwa na zuio za hapa na pale kumeshusha morali ya Demokrasia nchini. Mwanachama wa Chadema wa kawaida was Mbinga kwa miaka minne hajawahi kukutana na mwenyekuti wake wa chama kwenye mkutano. Mwenyekiti hana ruhusa ya kufanya mikutano akienda Mbinga atafanyia mikutano ndani na hapa atakutana tu na viongozi. Kwenye maandishi kikatiba tunatumia mfumo wa vyama vingi ila practically ni kimoja kinaoparete kwa mwavuli wa udola na kukagua utekelezaji wa ilani.

4. Vijana ndio chachu ya chaguzi zote duniani.... Hakuna uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya vijana wanaosaka ajira usiku na mchana na viongozi wa kuchaguliwa. Mwitikio wa vijana ni mdogo sana, angalia kwenye media utaligundua hili sana.

Tunakoelekea.

Pamoja na population yetu kuobgezeka idadi ya wapiga kura itazidi kupungua. Lazma tulifanyie kazi eneo hili.

Agizo la waziri.

Waziri Jafo amesema atapeleka dokezo kwa Mh Rais kwa mikoa ambayo uandikishaji utadorora ikiwezekana waadhibiwe. Mh Rais naye kashakubali kuwa atawashughulikia. Wakuu wa mikoa wataanza kuhaha kuomba watu wajiandikishe ili wasikutane na rungu la mh Rais.

Wanaweza kujiandikisha lakini je watapiga kura ? Hili ni eneo jingine.

Ole Mushi.
0712702602
 
Mashindano yoyote huleta msisimko kama kuna ushindani na washindani wenye kushindana kwa kwa vigezo huku masharti yakizingatiwa....
Matokeo ya kupangwa hupunguza mumkari na kuondoa msisimko wa shindano lolote... Upendeleo, mabavu, uonevu na rafu huku kukiwa na upendeleo wa wazi huwafanya washiriki, wapambe wao, wafuasi na mashabiki wa kawaida kuona kwamba hakuna maana ya kushiriki tena kama mashindano Kama hayo yakitokea....
Uchaguzi wetu wa serikali za mitaa umekosa msisimko kabisa kutokana na sababu tajwa hapo juu... Uandikishaji wa wapiga kura ni mbovu na wa kiwango cha chini
Watu wanaona hakuna haja ya kujiandikisha kwakuwa hata kama watapiga kura... Matokeo yanajulikana... Kila mtu anapotezea sasa....
Matangazo ya kuhamasisha uandikishaji haupaswi kuwa na viashiria vya upande fulani... Tunazidi kufeli... View attachment 1231641
Umeongea kweli ila wasivyo haya watajitoa ufahamu na kujiona washindi waache wazungu waje kutushangaa tu kwa kweli hakuna namna
 
Ntapigaje kura wakati sie tuliochagua wapinzani tunatengwa na mkuu? Acha nchi nzima viongozi wawe CCM ndio afurahi. Maendeleo yatakuja viongozi wote wakitoka CCM. Tutakua donor country.
 
*Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali*

Kila mmoja wenu ahakikishe watumishi wake wote wamejiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mtumishi ambaye hatajiandikisha ni kosa la kinidhamu na atachukuliwa hatua kwa kukiuka Maadili ya Utumishi wa Umma.

Hivyo baada ya uandikishaji kupita *uhakiki utafanyika* kubaini wale wote ambao hawakujiandikisha kwa hatua zaidi. Tafadhali mjulishe na mwingine.
 
Back
Top Bottom