Matokeo ya kufuzu AFCON 2021, Misri yalazimishwa sare, Rwanda wafungwa ugenini na Comoro wawatambia Togo ugenini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Katika mechi za kuwania kufuzu michuno ya AFCON 2021 zilizochezwa usiku huu imeshuhudiwa Misri wakidroo kwa bao 1-1 dhidi ya Kenye ambapo goli la Misri lilifungwa na mchezaji Kahraba dakika ya 42 na mnamo dakika ya 67 mchezaji Olunga alisawazisha na kuufanya mchezo huo kuisha kwa sare ya bao 1-1.

aidha, mechi nyingine iliwakutanisha Mozambique na Rwanda ambapo wageni Rwanda wamekubali kichapo cha goli 2-0. Magoli ya Mozambique yalifungwa na Mexer dakika ya 28 na Telinho dakika ya 30. Mpaka mwisho wa mchezo huo Mozambique 2-0 Rwanda.


Ama mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Togo na Komoro, ambapo Togo akiwa nyumbani amekubali kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na mchezaji Selemani dakika ya 51.

Michezo mingine ya kuwania kufuzu michuano hiyo itaendelea kesho katika viwanja mbalimbali. Miongni mwa michezo itakayofanyika kesho ni pamoja na ule wa Taifa stars dhidi ya Equatorial Guinea utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.

1573759830630.png
 
Ngoja tuwasubiri kichwa cha mwendawazimu watatuletea vituko gani...
 
Back
Top Bottom