Matokeo ya Kidato cha Sita kwa Mwaka 2019 yametangazwa rasmi leo

Hili suala la shule ina wanafuzi 50 kuwekwa kundi moja na shule yenye wanafunzi 270 nadhani halijakaa vzr. Kungekuwa na utratibu mwingine wa kupanga haya matokeo maana ukiangalia shule yenye wanafunzi 270 unaweza kukuta (kwa mfano) kuna dv One 140, halafu yenye wanafunzi 60 ikiwa na dv 45. Lakini wakiziweka kwa rank utaambiwa yenye wanafunzi 60 iko juu.
 
Ukizitenganisha unaongeza ufaulu wa hiyo shule yenye watoto wengi?.
 
Tukianza na mwaka Jana Tu.

Anthony mulokozi.

Mwaka huu waliofaulu arts wavulana na wasichana wanne wametoka kagera

Bado science kuna wawili
Ripoti ya mwaka huu matokeo ya kidato Cha 6 kilimanjaro tumeendelea kuwaburuza kagera Kama ilivyo Ada
Hakuna mwaka ambao kagera inaipita kilimanjaro kwenye form four au six pamoja na kwamba kilimanjaro tunaongoza kuwa na shule nyingi kuzidi mkoa wowote ule
Cc
kunde ekaka
 
Attachments

  • Screenshot_20190712-125005.jpeg
    Screenshot_20190712-125005.jpeg
    63.7 KB · Views: 22
Ripoti ya mwaka huu matokeo ya kidato Cha 6 kilimanjaro tumeendelea kuwaburuza kagera Kama ilivyo Ada
Hakuna mwaka ambao kagera inaipita kilimanjaro kwenye form four au six pamoja na kwamba kilimanjaro tunaongoza kuwa na shule nyingi kuzidi mkoa wowote ule
Cc
kunde ekaka
Unaongelea form six?
Zaidi ya wanafunzi waliomaliza form six huwa sio wa mkoa husika!!

Au unajifanya hujui?

Mfano kamugisha wa pili kitaifa amesomea kisimiri Arusha lakini ni mwenyeji wa kagera.

Toa ushamba wako hapa
 
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.
Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.

Katibu mtendaji huyo amesema kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani , watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.

Dk Msonde amesema watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 80,216 waliosajiliwa, watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99,44 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 33,883 sawa na asilimia 99.57 na wavulana 45,887 sawa asilimia 99.35. Watahiniwa 446 sawa na asilimia 0.56 hawakufanya mtihani.

Amesema watahiniwa wa kujitegemea kati ya11,082 waliosajiliwa, 10,231 sawa na asilimia 92.32 walifanya mtihani na watahiniwa 851 sawa na asilimia 7.68 hawakufanya.

“Jumla ya watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamefaulu,” amesema Msonde

Watahiniwa Kumi bora Kitaifa kwa masomo ya Sayansi kuanzia namba moja hadi kumi ni

1. Faith Nicholous Matee (St. Marry’s Mazinde Juu-PCB)
2. Herman Pauline Kamugisha (Kisimiri-PCM)
3. Levina Calist Chami (St. Marry Goretti-PCM)
4. Benius Eustace (Mzumbe-PCB)
5. Augostino Issaya Omari (Ilboru-PCB)
6. Satrumin Arbogast Shirima (Temeke-PCB)
7. Khalid Hussein Abdallah (Feza Boys-PCM)
8. Assad Y. Msangi (Feza Boys-PCM)
9. Peter Jovenal Riima (Kibaha-PCM)
10. Augustine J. Kamba (Feza Boys-PCM)

Wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kwa masomo ya Lugha na Sanaa ni
1. Victor G. Mtui (Feza Boys-EGM)
2. Paula Nelson Lujwangana (St. Marry’s Mazinde Juu-HKL)
3. Blandina Kessy Nyage (St.Marry’s Mazinde Juu-HGL)
4. Eva J. Shitindi (Machame Girls-HKL)
5. Ruhinda Benedicto Machimu (Geita Adventist-HKL)
6. Anita Zacharia Massawe (St.Marry Mazinde Juu-HKL)
7. Karimu Kassimu Muhibu (Nyangao-HKL)
8. Anold Andrea Msuya (Manyara-HKL)
9. Latifa Mohamed Mrosso (Ahmes-HKL)
10. Eliibariki Desidery Baliyanga (Lukole-HKL)

Waliofanya vizuri Kitaifa kwa masomo ya Biashara ni

1. Astone Stevin Ngaeje (Kibaha-ECA)
2. Gift M. Mwakikusi (Tusiime-ECA)
3. Emmanuel P. Chila (Alpha-ECA)
4. Athumani Magadula William (Umbwe-ECA)
5. Stephano Y. Dismas (Kibaha-ECA)
6. Robert John Tano (Scolastika-ECA)
7. Shabani H. Shabani (Kibaha-ECA)
8. Dotee A. Zuberi (Galonos-ECA)
9. Ernest P. Game (Kibaha-ECA)
10. Deogratias Ladislaus Msilinga (Kibaha-ECA)

Katika matokeo hayo Shule Kumi bora zilizoongoza Kitaifa ni

1. Kisimiri (Arusha)
2. Feza Boys (Dar es Salaam)
3. Ahmes (Pwani)
4. Mwandet (Arusha)
5. Tabora Boys (Tabora)
6. Kibaha (Pwani)
7. Feza Girls (Dar es Salaam)
8. St. Marry’s Mazinde Juu (Tanga)
9. Canossa (Dar es Salaam)
10. Kemebos (Kagera)

Shule Kumi zilizofanya vibaya Kitaifa ni

1. Nyamunga (Mara)
2. Haile Salassie (Mjini Magharibi)
3. Tumekuja (Mjini Magharibi)
4. Bumaangi (Mara)
5. Butuli (Mara)
6. Mpendae (Mjini Magharibi)
7. Eckernford (Tanga)
8. Msimbo (Katavi)
9. Mondo (Dodoma)
10. Kiembe Samaki A (Mjini Magharibi)
Hongereni wadogo zetu mliofanya vizuri katika mtihani wenu wa kidato cha sita.
 
Unaongelea form six?
Zaidi ya wanafunzi waliomaliza form six huwa sio wa mkoa husika!!

Au unajifanya hujui?

Mfano kamugisha wa pili kitaifa amesomea kisimiri Arusha lakini ni mwenyeji wa kagera.

Toa ushamba wako hapa
Baada ya kuburuzwa unatoa sababu mfu Nan kakwambia wanaosoma advance wote Ni wagen wa mkoa husika? Wewe kubali kushindwa tu kagera haijawahi ipita kilimanjaro kielimu tangu Uhuru Jana si mlikuwa mkitaka hii ripoti? Sasa nawawekea mnaleta longo longo hahaha
 
Minimum qualifications ni 4 points ambazo ni DD, huyo ana CE ambazo ni C= 3, E= 1,jumla 4 points. Chuo naamini atapata.
Sifa siyo kuwa na pointi nne tu, bali unakuta wameainisha kabisa kuwa kila somo una at least D. kwa hiyo japo CE inakupa hizo pointi 4, lakini kwa kigezo cha pili cha kuwa na at least B mbili kinakuangusha. Kwa mfano ukiwa na A & S , japo una zaidi ya pointi 4, lakini kigezo cha kuwa na angalau principle mbili kinakuangusha.
 
Hawa madogo nao wamalize kusoma... Dingi niko anti-book tunachanganyana akili tu.

Huyu vipi huyu... Niandae pesa au nimkabidhi mtaji.

General studies - E.
History - S
Kiswahili - D
Language - D

Ni dvsn 3 ya 14.
Andaa pesa ya chuo, halafu akimaliza chuo ndo umpe mtaji wakati akiwa amepevuka zaidi na ana upeo mkubwa zaidi.
 
Hivi mnajua Kisimiri - Arusha ni shule ya Kata!! Nafikiri inafaa kutumika kama case study kwa shule nyingine za kata nchini walimu wakajifunze mbinu pale Kisimiri.
Haiwezi kutumika kama case study maana intake yake haina tofauti na special school zingine. Waingie hata top 200 za form 4 ambako ni shule ya kata tu ndio tuwasifie
 
Baada ya kuburuzwa unatoa sababu mfu Nan kakwambia wanaosoma advance wote Ni wagen wa mkoa husika? Wewe kubali kushindwa tu kagera haijawahi ipita kilimanjaro kielimu tangu Uhuru Jana si mlikuwa mkitaka hii ripoti? Sasa nawawekea mnaleta longo longo hahaha
Endelea kujifariji wakati kila mtu anajua kagera ndo chimbuko la wasomi wengi Africa mashariki na kati
 
Dah kasema ataomba udaktari tu et anataka afuate nyayo zangu !

Private lakini si uhakika ?
Private ni uhakika ili mradi pochi yako ni ya uhakika pia!!!! Aombe Kariuki, ni chuo kizuri mno ila ada yake ni zaidi ya 5M, kabla ya mahitaji mengine kama chakula, malazi, stationary na pocket money.
 
Kwangu Mimi shule iliyotisha ni St Mary's mazinde! Wanafunzi zaidi ya 200 alafu wanaingia top 10???? Mkuu wa shule nampa Big up!
Wewe una akili sana!!! Hiyo kwa kigezo cha ukweli ndiyo iliyopaswa kuwa ya kwanza halafu kibaha ilipaswa kuwa ya pili.
Inashangaza shule yenye DIVISION ONE 58 na wanafunzi 60 kuwa ya kwanza na yenye DIVISION ONE 143 na wanafunzi zaidi ya 170 kuwa ya pili. Zote hazina 0, IV japo kibaha ina III tatu.
Unategemeaje mtu aliyebeba mzigo wa kilo zaidi ya kilo170 ashindane kwenye mbio na mtu aliyebeba mzigo wa kili 60!!! Halafu mwenye kilo kidogo akatangulia kwa sekunde 2 zaidi ya mwenye kilo nyingi, halafu ukaamini ushindi wake ni halali!!!
 
U
Hili suala la shule ina wanafuzi 50 kuwekwa kundi moja na shule yenye wanafunzi 270 nadhani halijakaa vzr. Kungekuwa na utratibu mwingine wa kupanga haya matokeo maana ukiangalia shule yenye wanafunzi 270 unaweza kukuta (kwa mfano) kuna dv One 140, halafu yenye wanafunzi 60 ikiwa na dv 45. Lakini wakiziweka kwa rank utaambiwa yenye wanafunzi 60 iko juu.
Ni ajabu na kweli
 
Endelea kujifariji wakati kila mtu anajua kagera ndo chimbuko la wasomi wengi Africa mashariki na kati
Hahaha ripoti Jana uliitaka naiweka Leo unaruka ruka hahaha Kilimanjaro ndio nyumban kwa elimu,nyie kagera na ukubwa woote mnazidiwa idadi ya shule na ka mkoa kadogo kieneo kama kilimanjaro tena kwa mbali,haihitaji PhD kuelewa nan ni chimbuko la elimu hapo
 
Ni aibu Kwa mkoa wenye shule zote hizo lakini hakuna hata moja top ten.

Huyu mtu chini unamuona?ni mwenyeji wa Bukoba.

Juzi Kati amewaburuza wanachuo wote wa Frederick university huko ulaya.

Ni best student .

Mkuu kubali Tu nitakuletea kibao maana mabest students nitakuporomoshea wote hapa.

tapatalk_1562956023496.jpeg
tapatalk_1562956045809.jpeg
 
Back
Top Bottom