Matokeo ya Kidato cha Sita kwa Mwaka 2019 yametangazwa rasmi leo

Haiwezi kutumika kama case study maana intake yake haina tofauti na special school zingine. Waingie hata top 200 za form 4 ambako ni shule ya kata tu ndio tuwasifie
Kama kweli unachosema una uhakika na cho unafikiri ni kwa nini hiyo shule inaruhusiwa kuchukua intake kama ya special school wakati sio special xul? Je maamuzi ya selection ya wanafunzi anafanya nani na vigezo vipi vinaangaliwa?
 
Haya matokeo yameleta furaha kwa vijana na shule zilizofanya vzr. Na ktk hilo hata wazazi wa watoto waliofaulu wamepata faraja sambamba na walimu wa shule zilizofaulisha vzr.
Lakini kupitia matokeo hayo tupo wazazi wa vijana na vijana wetu (wanaoingia kuanza kidato cha tano) ambao tumeumizwa matokeo hayo hata kabla ya watoto wetu kuufikia mtihani wenyewe!
Mtoto aliyefaulu kutokea shule ya kata kwa kiwango Div I,kuchaguliwa akasome Advance shule ya Nyamunga ambayo imekuwa ya mwisho kitaifa,hakika ni dhamiri ya wazi ya kummaliza kabisa. Na kwa bahati mbaya zaidi,huyu ni kijana anayetokea kwenye uduni wa maisha ambaye ameamua kujipigania ili baadaye aikomboe familia yake lkn anakatishwa tamaa mapema kabisa.
Naomba nisieleweke km napingana na serikali kuwapeleka watoto kwenye hizo shule..hapana!! Ila nafikiri serikali itatakiwa kuzimulika sana hizi shule na endapo ufaulu wao mbovu umetokana na miundombinu isiyosahihi,basi angalau itufute machozi kwa kuchukua hatua za haraka kurekebisha na kuziwezesha kuingia kwenye ushindani wa ufaulu mzuri.
Inatia huruma kuona mtoto amepambana licha ya kusoma shule ya kata ambazo nyingi tunajua mapungufu yake,akatoka na division I kisha umpeleke akasome A'level shule ya mwisho kitaifa. Ambayo tafsiri ni kuwa na yeye akafeli.
Nina imani ya kutosha na mh. Jafo na Mh. Ndalichako kuwa hili wameliona na watatengeneza mambo mapema na siyo kuishia kuzipongeza zilizofanya vzr pekee.
 
Shukran mkuu nlikuwa nachek guide book nimeona kozi mbali mbali ila sijagundua kwa vyuo vya dsm kozi gani haina competition kwa pass zake ili apate kwa uhakika chap...
Andaa pesa ya chuo, halafu akimaliza chuo ndo umpe mtaji wakati akiwa amepevuka zaidi na ana upeo mkubwa zaidi.
 
Mkuu shule za serikali elimu kichwa chako zote majanga labda special school huwa zina motisha kidgo lkn msuli upo pale pale hata upelekwe wap kwa A level
Haya matokeo yameleta furaha kwa vijana na shule zilizofanya vzr. Na ktk hilo hata wazazi wa watoto waliofaulu wamepata faraja sambamba na walimu wa shule zilizofaulisha vzr.
Lakini kupitia matokeo hayo tupo wazazi wa vijana na vijana wetu (wanaoingia kuanza kidato cha tano) ambao tumeumizwa matokeo hayo hata kabla ya watoto wetu kuufikia mtihani wenyewe!
Mtoto aliyefaulu kutokea shule ya kata kwa kiwango Div I,kuchaguliwa akasome Advance shule ya Nyamunga ambayo imekuwa ya mwisho kitaifa,hakika ni dhamiri ya wazi ya kummaliza kabisa. Na kwa bahati mbaya zaidi,huyu ni kijana anayetokea kwenye uduni wa maisha ambaye ameamua kujipigania ili baadaye aikomboe familia yake lkn anakatishwa tamaa mapema kabisa.
Naomba nisieleweke km napingana na serikali kuwapeleka watoto kwenye hizo shule..hapana!! Ila nafikiri serikali itatakiwa kuzimulika sana hizi shule na endapo ufaulu wao mbovu umetokana na miundombinu isiyosahihi,basi angalau itufute machozi kwa kuchukua hatua za haraka kurekebisha na kuziwezesha kuingia kwenye ushindani wa ufaulu mzuri.
Inatia huruma kuona mtoto amepambana licha ya kusoma shule ya kata ambazo nyingi tunajua mapungufu yake,akatoka na division I kisha umpeleke akasome A'level shule ya mwisho kitaifa. Ambayo tafsiri ni kuwa na yeye akafeli.
Nina imani ya kutosha na mh. Jafo na Mh. Ndalichako kuwa hili wameliona na watatengeneza mambo mapema na siyo kuishia kuzipongeza zilizofanya vzr pekee.
 
Hivi wakuu samahanin kidogo.

Taifa linapotangaza asilimi za watu waliofanya vizuri wanaaanisha kufanya vizuri huko ni kwa wale walianzia divisn ngap hadi ngap na waliofanya vibaya ni kundi lipi hadi lipi..

Maaana mashndwa kuelewa kabisa kila nikipiga mahesabu idadi ya watahiniwa na idadi ya nafasi wazi vyuoni naona kama mzani hauwez balance kama vile watu watakosa vyuo.

Maaana nimeangalia juu juu tu hapa...kwenye guide book ya tcu.

Vyuo vyoote jumla vitachukua watu form six leaver kama elfu 88 hivi.

Then waliofanya vizuri pia kitaifa kwa mwaka huu tu ni elfu 80.

Sasa je ukichanganya na waliokosa mwaka jana... Ongezea na waliofanya mitihan nnje ya nchi... Ongezea na wengineo naona kama idadi ya waliopass itazid idadi ya nafasi wazi za vyuo.

Mwenye uelewa anipe mwanga kidogo.

Nilikuwa katika harakati za kuangalia kama woote wenye sifa ni lazima watapata vyuo kwa kozi walizoziomba.

Msaada hapo ufafanuz kidogo wakuu
 
Mkuu shule za serikali elimu kichwa chako zote majanga labda special school huwa zina motisha kidgo lkn msuli upo pale pale hata upelekwe wap kwa A level
Ni kweli uyasemayo,lkn iangalie tofauti kubwa iliyopo kati ya hizo shule. Zingine walau kaunafuu kapo. Sasa kweli shule ya Advance zero zinakuwa nyingi kuliko waliofaulu.....haya ni majanga!
 
Kama kweli unachosema una uhakika na cho unafikiri ni kwa nini hiyo shule inaruhusiwa kuchukua intake kama ya special school wakati sio special xul? Je maamuzi ya selection ya wanafunzi anafanya nani na vigezo vipi vinaangaliwa?
Hapo mimi sijui maana o level hawana performance ya kutisha. Mimi ninachoamini wale wanafunzi wanaopelekwa kisimiri ni wanafunzi bora hata kama ukiwapeleka shule ya Minaki watatoboa tu . Ubora na uchache wao plus comb wanazosoma unaifanya shule iendelee kuwa bora
 
Fanya research yako tena upate findings za kutosha ili uweze kusema na kushauri vizuri Mkuu.
 
Wana samahani.

Hivi kuna chuo kinatoa kozi ya cyber security & intelligence kwa tanzania...
Maana nimechek guide book hakuna...

Au kozi yeyote inayohusiana na izo mambo?

Pili kuna tofauti kati ya kozi ya disaster management na social protection?

Maana hii diaster nimeichek pia sijaziooona kabisa ....
 
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.
Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.

Katibu mtendaji huyo amesema kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani , watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.

Dk Msonde amesema watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 80,216 waliosajiliwa, watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99,44 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 33,883 sawa na asilimia 99.57 na wavulana 45,887 sawa asilimia 99.35. Watahiniwa 446 sawa na asilimia 0.56 hawakufanya mtihani.

Amesema watahiniwa wa kujitegemea kati ya11,082 waliosajiliwa, 10,231 sawa na asilimia 92.32 walifanya mtihani na watahiniwa 851 sawa na asilimia 7.68 hawakufanya.

“Jumla ya watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamefaulu,” amesema Msonde

Watahiniwa Kumi bora Kitaifa kwa masomo ya Sayansi kuanzia namba moja hadi kumi ni

1. Faith Nicholous Matee (St. Marry’s Mazinde Juu-PCB)
2. Herman Pauline Kamugisha (Kisimiri-PCM)
3. Levina Calist Chami (St. Marry Goretti-PCM)
4. Benius Eustace (Mzumbe-PCB)
5. Augostino Issaya Omari (Ilboru-PCB)
6. Satrumin Arbogast Shirima (Temeke-PCB)
7. Khalid Hussein Abdallah (Feza Boys-PCM)
8. Assad Y. Msangi (Feza Boys-PCM)
9. Peter Jovenal Riima (Kibaha-PCM)
10. Augustine J. Kamba (Feza Boys-PCM)

Wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kwa masomo ya Lugha na Sanaa ni
1. Victor G. Mtui (Feza Boys-EGM)
2. Paula Nelson Lujwangana (St. Marry’s Mazinde Juu-HKL)
3. Blandina Kessy Nyage (St.Marry’s Mazinde Juu-HGL)
4. Eva J. Shitindi (Machame Girls-HKL)
5. Ruhinda Benedicto Machimu (Geita Adventist-HKL)
6. Anita Zacharia Massawe (St.Marry Mazinde Juu-HKL)
7. Karimu Kassimu Muhibu (Nyangao-HKL)
8. Anold Andrea Msuya (Manyara-HKL)
9. Latifa Mohamed Mrosso (Ahmes-HKL)
10. Eliibariki Desidery Baliyanga (Lukole-HKL)

Waliofanya vizuri Kitaifa kwa masomo ya Biashara ni

1. Astone Stevin Ngaeje (Kibaha-ECA)
2. Gift M. Mwakikusi (Tusiime-ECA)
3. Emmanuel P. Chila (Alpha-ECA)
4. Athumani Magadula William (Umbwe-ECA)
5. Stephano Y. Dismas (Kibaha-ECA)
6. Robert John Tano (Scolastika-ECA)
7. Shabani H. Shabani (Kibaha-ECA)
8. Dotee A. Zuberi (Galonos-ECA)
9. Ernest P. Game (Kibaha-ECA)
10. Deogratias Ladislaus Msilinga (Kibaha-ECA)

Katika matokeo hayo Shule Kumi bora zilizoongoza Kitaifa ni

1. Kisimiri (Arusha)
2. Feza Boys (Dar es Salaam)
3. Ahmes (Pwani)
4. Mwandet (Arusha)
5. Tabora Boys (Tabora)
6. Kibaha (Pwani)
7. Feza Girls (Dar es Salaam)
8. St. Marry’s Mazinde Juu (Tanga)
9. Canossa (Dar es Salaam)
10. Kemebos (Kagera)

Shule Kumi zilizofanya vibaya Kitaifa ni

1. Nyamunga (Mara)
2. Haile Salassie (Mjini Magharibi)
3. Tumekuja (Mjini Magharibi)
4. Bumaangi (Mara)
5. Butuli (Mara)
6. Mpendae (Mjini Magharibi)
7. Eckernford (Tanga)
8. Msimbo (Katavi)
9. Mondo (Dodoma)
10. Kiembe Samaki A (Mjini Magharibi)
SOON TUKIENDA NA RECORD HIZI TUTAONA MAPINDUZI YA SHULE ZA SERIKALI ZIKIRUDI KATIKA WADHIFA WAKE. GOOD STARTS!!
 
Wana samahani.

Hivi kuna chuo kinatoa kozi ya cyber security & intelligence kwa tanzania...
Maana nimechek guide book hakuna...

Au kozi yeyote inayohusiana na izo mambo?

Pili kuna tofauti kati ya kozi ya disaster management na social protection?

Maana hii diaster nimeichek pia sijaziooona kabisa ....
Nafikiri UDOM wana hiyo taalauma japo inaweza isiwe kwa namna unavyoiita wewe ndio maana hujaiona kwenye guide book, lakini taaluma inayohusiana na hayo mambo ya cyber security pale itakuwepo tena ina miaka sio chini ya mitatu.
 
Shukran mkuu wanaweza wakawa wanatumia jina gani...

Alafu na hii international maritime laws na air traffic controller
 
Fanya research yako tena upate findings za kutosha ili uweze kusema na kushauri vizuri Mkuu.
One thing I know for sure ni kuwa kisimiri inachukua wanafunzi waliofanya vizuri sana form 4. Hiyo pekee inaiondoa kwenye shule za kata. Shule za kuilinganisha nazo ni kibaha, Ilboru, mzumbe na Tabora boys maana hizo ndio admission criteria zao zinafanana. Kama ingekua mazingira ya shule ndio sababu basi na form 4 ingefanya vizuri. Hebu nipe findings zako wewe zitakazoidisqualify hoja yangu.
 
Achana naye huyo mbishi tu.....kisimiri tahasusi mbili PCM na HKL na HKL advnce hawafeli ...PCM wenywe Single digit O level hapo unategemea nn???

Back
Top Bottom