Matokeo ya kidato cha nne yanatoka lini ?

lobikoki loti

Member
Dec 5, 2014
69
27
Motokeo ya form 4 2014 lini?na pia wataripoti shule lini!? kwani kuna wanaotaka kusoma kozi ya kompyuta miezi mitatu ila sasa wanapata wasiwasi kama mda utaruhusu ,nawasilisha wakuu ;.
 
Kuripoti shule ni mwezi wa saba mwakani, km ni computer akasome tu maana bado ana muda wa kutosha mtaani
 
Wewe dogo umewahi kuona lini, mtihani umefanyika mwezi wa 11 halafu unaanza kuuliza matokeo mwezi wa 12? Tulia, subiri vipimo vya Dokta Msonde. Kama ni Komputa, nenda ukasome salama!
 
Na utitiri wenu vishule vya kata kila siku bado mnataka wawasahihishie na kuwatangazia kwa muda uleule wa miaka ya sisi!! Hapo bado hamjawaumiza vichwa watu wa watu kwa mituhuma yenu ya udanganyifu kwenye vyumba vya mitihani.
Unadhani mpaka watangaze kumfutia mtu matokeo ni kazi ya siku moja?
Halafu mara nyingi wenye viherehere vya kutaka kujua passmark ni ngapi, mara mitaala hatupewi madarasani mara ooh matokeo yamecheleweshwa...huwa kichwani sifuri. Wenyewe waliopigilia misonge ya nguvu wapo kimyaa wanajiamini...
 
povu lote hilo la nini mkuu? dogo ameuliza swali rahisi na ameshajibiwa (na wenye busara zao). maelezo yoote haya ya nini? halafu kumbuka miaka "yetu" unaiyosemea hapa mchakato mzima wa mitihani mwanzo mwisho ilikuwa ni "manual" mwanzo mwisho! kaazi kweli kweli!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom